Unajua Matengenezo Gani Yalikuwepo IPP media Weekend Hii?

nurbert

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
1,887
427
Week end Hii wengi tulizikosa Eatv, Itv,capital kupitia Satelote Dish zetu
Leo asubuh Nlikua na Nmetulia home nikaona nivema nitumie my time kucheza na Dish maana nlibakiwa na chanel za mozambique tuu
Nkaona nizitafte upya pia TBc, star Tv na Ch 10 ambazo ziliweka mgomo tangu mwez wa 6

Baada ya Kurekebisha v2 na kuanza kusearch upya nikapata Chanel zote Vzuri ila chanel 10 bado imenigomea mpaka sasa na Iman tv imeshika ila hakuna any broad casted program..

Nikaamua nirudi kwenye IPP kuona walikua wanafanya Mabadiliko ghani Mpaka tukose Matangazo yao Kwa siku mbili !! Pili ilikua ni kwa Wote.. Yaani vin'gamuzi mpaka free to air Dishes nikaja kuona mabadiliko haya

•mabadiliko katika Audio
kama ww sio mtundu sana wa kugusa gusa receiver au decoder yako hili tengenezo bas utakua hulaligundua... Sijajua kwa wanao tumia Mpeg4 ila mm bado na tumia DVB [digital broadcast video] so hii pale kwenye audio ilikua kwa chanel za ipp inakubali kwenye stereo na right ila ukiweka left zilikua hazitoi sauti ila now any output saut inatoka iwe stereo au left au right .. Hii ilikua inakost kwa kias flan hasa kam unaangalia tv moja ya msumbiji ambayo ukiweka stereo basi sauti inaingiliana na redio moja hivi so itakubidi uweke left ambayo ndo inatoka audio ya tv.. So at the time ukirudi ipp zilikua hazitoi saut so mpaka uchange tena.. Ila now wame fix hili tatizo

•kuziweka Ea radio, Radio 1, Capital radio katika mfumo wa satelite kwa maana hiyo hizi ndio radio za kwanza za tz kuingia kwenye mfumo wa Satelite

Hapa naweza kuwa sijaeleweka vizuri au nimewachanganya baadhi ya wadau wasio elewa hii kitu!!

Hakukua na redio hata moja kwenye mfumo wa satelite [sina uhakika kwa watumiaji wa mpeg4 maana mm n DVB]
kilichokuwepo pale nikua Tv za tz watu huwa wanaweka radio katika Audio.. Kama una DSTV utakua umenielewa maana pale huwa tunakua na chanel ina audio mbili yaani kama ynaangalia mpira unaweza chagua mtangazaji awe wa lugha either English, french au portgues.... Ila video inakua hiyo hiyo wala huhitaji kubadili chanel... So chanel za tanzania huweka audio redio zake mfano now ukienda Tbc unaweza sikiliza tbc taifa, tbc fm, clouds fm na kitambo ilikuwepo Sibuka redio ila ilitolewa.. So zile sio Satelite redios ila ni Audio codecs za tv ila sisi ndo huwa tunaweka kama Redios kutokana na u duni wetu katika tecnolojiaaa. Kwa sasa kuzipata redios zile itakubidi u click ile button imeandikwa Tv/Redio ndipo uweze kusikiliza redio Zile

Kuna baadhi Ya Watu hawaja updates hizi redio so unachotakiwa kufanya ni ku scan upya [unaweza scan mannualy transponder yao tuu na ukazipata hizi redios!!!

kuhusu kua redio za kwanza kwenye satelite sina 100 percent maana kwenye Ku band nina redio ya gospel ni Ya kiswahili Ila sijathibitisha kama Ni ya Tanzania na imeandika tu Radio haijaweka jina lake.. Huwa napata hisia ni ya Kenya

Regards
 
Safi mkuu kwa ufafanuzi maana nimekuelewa,kwhy kwa ss sina haja kuweka kuangalia picha tu hlf nasikiliza redi0....
 
hongera kwa ugunduzi huo kaka kumbe ndio maana nikiweka radio inakatakata...sana kwa sasa ni kule kule tv/radio
 
Kuscan manual trasponder ndo kufanya nini?jaribu kusimplfy maelezo wengi hawajui jinsi ya kuscan.
 
Kuscan manual trasponder ndo kufanya nini?jaribu kusimplfy maelezo wengi hawajui jinsi ya kuscan.

Mkuu Hii Nmeshindwa Kuiwekema Maelezo Kutokana Na Humu Nadhan Kila Mtu Anatumia decoder Au Receiver Ya Aina Yake So Hazifanani!! Ila Kwa Baadhi Unaenda Menu then Instalation!! pale Kuna antena Setting, automatic seach au manual search!! So ukiingia hapo manual search ndo utacheza na transponder tuu [ile namba frequency ya Chanel then ukiingia kwenye Automatic unacheza na satelite nzima na unaweza ku mark chanel kadhaa]
 
Mkuu naona kwa tz ipp ndo wakwanza kuingiza mfumo huo, ila wenzetu wa Ke kitambo sana.
 
nikupongeze kwanza mtoa mada kwa hayo uliyoibaini. Utafiti usio rasm unaonyesha kuwa wa2 wengi sana wanafikiri kuwa wanao2mia decoda ya antenna ndio wanaopata matangazo ya digital na wenye madish ni analogia. Pili ningependa ufahamu pia hata rcva za mpeg4 ni DVB pia tofauti ni kwamba ya kwako ni DVB-S1 na za mpeg4 ni DVB-S2. S inamaanisha satellite, 1 ni first generation na 2 ni second generation. Na chochote kinachonasa kwenye ungo na kukipokea aidha kwa njia ya video, sauti au data ni cha kisatelaite. Sasa utawezaje kusema kwamba hizo radio ulizozitaje hapo juu kuwa hazikuwa za kisatelaiti. Ukipata bahati ya kusikiliza Rfa na radio uhuru watakuambia wanapatikana pia kwenye satelaiti. Unajua ukiwa decoda ya Ting AAL-003 ya ungo utaona ukifungua ATN na CH10 kwenye interface ya audio utazikuta radio uhuru na magic fm respectively. Hata huko unakosema zinapatikana bado wana2mia tp zilezile. Walichobadilisha ni format tu na c vinginevyo. Kwa ujumla nimefurahishwa sana na mada yako. Naruhusu kukosolewa.
 
Asante kwa kunielimisha mkuu!! Nmeelewa na now nmeongeza ujuz wa masuala ya Satelite!! Thanks sana
 
Back
Top Bottom