Unajua maana ya neno 'uchwara'? Unajua kwa nini ni neno linalochoma kunako?

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,961
2,000
Tunaishi nyakati ambazo siasa zetu zimetawaliwa na coded messages na matukio yanayohitaji tafakari ya juu kuweza kuyang'amua.

Nikitolea mfano wa haraka haraka ni hili jina 'Watu Wasiojulikana'. Hili ni jina ambalo kwa juu juu linaleta maana fulani ya 'watu walioshindwa kutambulika'. Lakini maana halisi ya jina hilo, na walilolitunga walijua hilo ni, 'watu ambao kawaida huwa hawatambuliki'. Ni coded name iliyofichwa kwenye maneno ya kawaida kabisa. Ni kama vile walikuwa wana insult intelligence yetu. Umenipata?

Tuje kwenye mada yangu. Neno 'uchwara' limepata umaarufu mkubwa miaka ya karibuni. Ni neno ambalo limekuwepo kwa muda mrefu ila lilififia ila nyakati tunazoishi limeliibua tena. Sina haja ya kuelezea kumhusu nani hili jina limekuwa linatumia sana. Sijui wangapi mmewahi kuwaza hasa kwa nini hili neno limeudhi baadhi ya watu. Nipo hapa kuelezea maana aliyodhamiria mnenaji na kwa nini ni neno linaloudhi.

Wengi wanachukulia tu maana yake ni 'mtu fake'. Hii ni maana ya juu juu sana. Katika mazingira fulani hiyo maana inaweza kufit lakini kama lilivyo jina 'watu wasiojulikana', ni muhimu sana kuelewa ujumbe nyuma ya maneno hayo ili kutambua uzito wake.

Naweza kulilinganisha neno 'uchwara' na neno la kiingereza la 'wannabe'. Merriam-Webster inatoa tafsiri mojawapo ya wannabe kuwa ni:

a person who wants or aspires to be someone or something else or who tries to look or act like someone else

Kwa maana nyingine ni mtu ambaye angependa aonekane au awe ni mtu fulani lakini hana kipaji, utajiri, werevu, swagga, karama au uwezo huo.

Kama mtu umedhamiria kuwa mtu fulani kweli kweli na umewekeza nguvu nyingi kuwa hivyo halafu mtu akakwambia wewe ni 'xyz uchwara', ni kauli inayochoma hasa. Inamfanya mlengwa ajione myonge sana. Mtu anamkumbusha nguvu zote alizodhani anazo kumbe hazitampa kile alichokuwa anataka. Anachukulia kwamba those are fighting words!

Pay attention.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom