Unaijua siri ya kiganja chako??

Unaijua siri ya kiganja chako??

nitajuaje kama kiganja changu ni kirefu,cha kati ama kifupi?? Kupimo halis ni kipi? Au tunatumia rula kupima? Nijuze mkuu
 
Ndo maana yake mkuu,haya ya kusema hiki ni kirefu inategemea umekilinganisha na kipi.

Unaweza kulinganisha na huyu ukakuta chako ni kikubwa kinima ila ukilinganisha na mwingine unakuta nikidogo!! .......
 
Mbona hapo kwenye namba tatu umetaja wanaume tu? Inamaana wanawake nao hawana hizo tabia?
 
UJUE 'HEART LINE' KATIKA KIGANJA CHAKO.



Nashukuru ujumbe ulieleweka kwa wengi na nashukuru kwa kuitikia kwenu kuokoa maisha kupitia sanaa hii ya kisayansi.

Leo nimekuja na watu wengine ambao mstari wa heart line unaovigawa vidole na kiganja umejikunja ukaingia kati ya kidole cha shahada na kidole cha kati.

Watu hawa kwanza ni watanashati na wanawake ni warembo na wacheshi sana. kama ulifungua ile link niliyokupa ushuhudie wameelezwa kuwa "they fall in love easly" ikimaanisha kutapeliwa, kudanganywa, kuzulumiwa, na vitu kama hivyo ni kitu cha kawaida kwao.

Ni kawaida kabisa kila ukutanapo na mtu wa aina hii kukupa mikakati mipya ya maisha yake kwa kuwa ile aliyokusimulia mwaka jana imefeli kuzaa matunda.

Wanawake mimba zinaharibika, wapenzi wanawakimbia kila kukicha,ndoa zinavunjika, kazi mbaya kila siku kwa kuwa kila likitokea tatizo yeye ndiye anayetolewa sadaka. Biashara zinaanza vizuri hazichukui muda zinakufa na mambo kama hayo.

Wanaume wanabaki kuoa kila kukicha maana wamekimbiwa, kazi na biashara mpya kila siku maana mipango hainyooki n. k. Kifupi hawa watu wanakuwa ngazi za kuwanufaisha wengine.

Mbaya zaidi utakuta kuwa hata waathirika wa UKIMWI wengi ni hawa wenye mstari huu kwa kuwa wamebadili wapenzi mpaka wamekalia migongo kwa kuchoka.

Hatari ni nyingi ukiacha UKIMWI na maisha mabovu kila kukicha. Jiangalie vizuri kama mstari huo katika kiganja chako umeingia kati ya shahada na kidole kati basi basi nitafute nikuokoe na majanga haya kabla huja "fall in love easly" na kuingizwa mkenge tena.

Kwa wale wanaodhani kuwa huu ni UCHAWI napenda kuwatuliza kuwa huu sio uchawi bali ni elimu tu ya kawaida inayohitaji macho mazima kuona, akili ya kawaida kusoma, na kiganja cha kusomwa tu basi.

Wazungu wao wapo mbele katika taaluma hii na kama huamini basi fungua hiyo link hapo chini uone.
 
palm-reading-diagram.jpg
 
Yoote hii ni statistics ambayo inahusishwa na ushirikina na fortune tellers ambao maneno yao ni uongo na hayana shahidi wwt.
Ndo maana unakuta watu wasio na dini hukata tamaa ya maisha kwa kufuata upuuzi huu na wengine kufikia kuyamaliza maisha yao eti kwa sababu kasomewa kiganja kaambiwa hana bahati au hatozaa tena.
Bata wakubwa hawa! Wao wanauwezo gani wa kuona kesho.? Zaidi ni kuibiana tu. Na kuharibu maisha ya watu.
 
Back
Top Bottom