Unahitajika ushauri/mawazo kuokoa hili penzi

Unahitajika ushauri/mawazo kuokoa hili penzi

Mwanamke aliyekwisha kuwa na mahusiano hasa akapata mtoto na mtu halafu akamuumiza, anahitaji upendo wa kidogokidogo usilazimishe akupende gafla! Anachotaka ni awe na imani na wewe akuone kwamba wewe sio kama wale.
Muoneshe upendo, kuwa karibu naye akikuamini utakuwa na maisha matamu na familia bora.
 
Habari za jpili wadau,bila kupoteza muda naomba nielezee sababu za kuomba ushauri/mawazo,japo mtanisamehe mm sio mwandishi mzuri twendeni hivyohivyo.


Iko hivi mwaka huu kwenye mwezi wa 5 niliamua kuvunja ukimya kwa kuanzisha mahusiano na mwanadada mmoja,kwakweli huyo dada nilimwelewa sana ni mtu anaonekana ana vision kuhusu maisha,mwanzoni mwa mahusiano nilishindwa kumwelewa sababu ni mtu ametulia sana yaan mkimya,hio hali ilikuwa inaniumiza sana unajiuliza huyu mtu hafurahii haya mahusiano au ana tatizo gan?!,iko hivi usipomtafuta basi na yy haangaiki kukutafuta,unampigia sim hapokei,baadae akipokea namwuliza hujakuta missed call mbona hukunicheki kujua sababu za kukutafuta bado majibu yake bado yanakuwa hayajitoshelezi/hayaridhishi,kuna siku nilimwuuliza je unanipenda na upo serious kweli unahitaji tujenge familia?,jibu lake ni ndio nakupenda na nipo serious kweli kweli,nilimweleza hio hali ya kuwa mkimya siifurahi kama kuna tatizo niambie,alichojibu aliniambia ndio hivi nilivyo,kwa kifupi hayupo romantic,unajitahidi kumwandikia sms za mahaba lkn majibu yake unachoka,utamtext sms nzuuri lkn atajibu "ASANTEE AU POA",Mpaka huwa najuliza wale wanaopotiwa kwenye status na wapenzi wao huwa wanafanyaje,kuna wakati nilimbana nikamwuliza kama una mtu anakuweka busy niambie tuu nicheki ustaarabu mwingine lkn alikataa katakata na yy kuniuliza kwanin simwamini?kuna siku nilimwita mahali akaja nikamsuprise kwa kumpeleka dukani nikamwambia achague sim sababu alikuwa na sim ya torch,lkn bado hakuonyesha kufurahia hio zawadi,tatizo lingine yupo busy sana ukiuliza sababu anadai kwao amebaki yy na mamaake ndg zake wengine wameolewa na wanaume wana maisha yao mbali na nyumban,so yy ndio wa kumsaidia bimkubwa biashara na shughuli za nyumban,

Tusaidiane mawazo/ushauri...,kiukweli nimemwelewa sana na nnahitaji awe mama wtt wangu ila kinachonipa wasiwasi ni hiyo tabia yake.


NB:Amejaliwa kupata mtt mmoja wa kike nimejitolea kuubeba huo msalaba lkn naona unataka kunishinda kwa tabia yake
Atakuwepo anayejibiwa vizuri we hajakuchukulia serious kabisa kadandia tu akifika kituon ataachia aendelea na safari
 
Mwanamke aliyekwisha kuwa na mahusiano hasa akapata mtoto na mtu halafu akamuumiza, anahitaji upendo wa kidogokidogo usilazimishe akupende gafla! Anachotaka ni awe na imani na wewe akuone kwamba wewe sio kama wale.
Muoneshe upendo, kuwa karibu naye akikuamini utakuwa na maisha matamu na familia bora.
Hilo ndio ninaloamini mkuu
 
Atakuwepo anayejibiwa vizuri we hajakuchukulia serious kabisa kadandia tu akifika kituon ataachia aendelea na safari
Mkuu ndio unaniumiza kbs,ukizingatia nimempenda kutoka moyon
 
Mkuu kama unampenda kweli usimuache..tumia muda wako kujua ana tatizo gani?na huyo mwanamke kama ni mchaga itachukua muda sana kuwa unavyotaka awe.

Hamishia upendo kwa mtoto wake ataanza kuona wivu na ataamini unampenda kweli nayeye ataanza kukuonesha hisia unazotaka akuoneshe..
 
Mwanamke aliyekwisha kuwa na mahusiano hasa akapata mtoto na mtu halafu akamuumiza, anahitaji upendo wa kidogokidogo usilazimishe akupende gafla! Anachotaka ni awe na imani na wewe akuone kwamba wewe sio kama wale.
Muoneshe upendo, kuwa karibu naye akikuamini utakuwa na maisha matamu na familia bora.
Tatizo mm nahisi nnaweza kupoteza muda kumbe mwenzangu ana mtu anamuwaza,nakumbuka kuna siku nilifanya kumfokea sababu ya huo ukimya wake,baadae akaniambia mm nikimuuzi hawezi kuniambia ila atalia basi hasira zake zitaisha
 
Mkuu kama unampenda kweli usimuache..tumia muda wako kujua ana tatizo gani?na huyo mwanamke kama ni mchaga itachukua muda sana kuwa unavyotaka awe.

Hamisia upendo kwa mtoto wake ataanza kuona wivu na ataamini unampenda kweli nayeye ataanza kukuonesha hisia unazotaka akuoneshe..
Ni mchaga kweli mwenyeji wa rombo
 
Pole sana, hiko kitu kinakera sana hasa pale unapoonyesha upendo wa hali ya juu kwa mtu alafu yeye anachukulia poa tu. Inakera na sijui hata unawezaje kuvumilia hyo hali
 
Je? Ww na ww ni single baba, kama na ww sio usijaribu , na hapo kwangu naona utafundishwa maisha na yy na sio mnafundishana kama ww huha mtoto.
 
Ni mchaga kweli mwenyeji wa rombo

Ninaye mmoja wa aina hiyo hadi sasa nipo naye kama mchepuko..
Wanapenda kweli ila ndio wapo hivyo sasa ukimkuta aliyewahi kuumizwa kwenye mapenzi kasumba yake ndio hiyo...

Ni wakimya sana pia hawapo romantic hata kidogo,hata kunako 6*6 wamezubaa sana lakini ndio anakupenda hivyo..

Mimi uvumilivu ulinishinda nikaamua nimpandishe cheo awe mchepuko nikapata mwanamke mwenye mtoto,maisha matamu tu..

Huyo wako usimuache jaribu kuwa naye karibu sana utajifunza mengi
 
Je? Ww na ww ni single baba, kama na ww sio usijaribu , na hapo kwangu naona utafundishwa maisha na yy na sio mnafundishana kama ww huha mtoto.
Single father wa mtt mmoja mkuu
 
Pole sana, hiko kitu kinakera sana hasa pale unapoonyesha upendo wa hali ya juu kwa mtu alafu yeye anachukulia poa tu. Inakera na sijui hata unawezaje kuvumilia hyo hali
Kweli mkuu hamna kitu kinakera kumpenda then yy haonyeshi kuthamini penzi lako
 
Niwahi kuwa na mmoja wa aina hiyo hadi sasa nipo naye kama mchepuko..
Wanapenda kweli ila ndio waoo hivyo sasa ukimkuta aliyewahi kuumizwa kwenye mapenzi kasumba yake ndio hiyo...
Ni wakimya sana pia hawapo romantic hata kidogo,hata kunako 6*6 wamezubaa sana lakini ndio anakupenda hivyo..

Mimi uvumilivu uliniahinda nikaamua nimpandishe cheo awe mchepuko nikao mwanamke mwenye mtoto,maisha matamu tu
[emoji3][emoji3][emoji3]Rombo kitandani wana shida gani???
 
Upo sahihi kbs mkuu,najaribu kumwonyesha upendo wa dhati kbs,lkn ataendelea na hio hali sina budi kumwacha,mpaka kuna muda najiuliza huyu amenifanyaje mwisho wa siku nagundua ni upendo wangu kwake
Achana naye! Utapata shida ukimweka ndani. Wanini single mother? Siku akikutana na mzazi mwenzie atamgegeda wakumbushie.
Single mother SI wazuri WA Kuoa utakuw kwenye risk Sana!
Kwa nini ulee mtoto WA mtu.
Achana naye hiyo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom