Unahitajika msaada wenu,kwenye mahusiano haya jamaniii!!!

mchajikobe

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
2,652
1,238
Kuna jamaa yangu mmoja na ni mtu wangu wa karibu sana,anampenzi wake wa kike ambaye ameshamtambulisha hadi kwao,ila kunamambo ambayo yanamtokea jamaa huyu ambayo amejaribu kuniomba ushauri,na naomba wana JF wenzangu mumsaidie kwa ushauri,siku moja alimpigia simu huyo mpenzi wake na kujuliana hali,mpenzi wake akamwambia kuwa yupo nyumbani kwake(yaani kwa huyo mwanamke),baadae akakutana na huyo mwanaume wake mitaa ambayo wote sio yakwao,lakini huyo mwanamke alikuwa ameongozana na mwanaume mwingine,na mara alipomuona yule mwanaume wake ghafla alishtuka na kuzuga kwa kumuuliza vipi mbona upo mitaa hii,hatuagani?kipindi hicho yule mwanaume mwingine alendelea na kwenda kumsubiri yule mwanamke mbele,mwanamke akamwambia yule mtu wake nafika hapo mbele na kumfuata yule mwanaume bila ya kumtambulisha na kuendelea na safari.Siku nyingine wakati wamekaa pamoja ikaingia msg kwenye simu ya mwanamke,ikiwa imedisplay jina la aliyetuma na msg ilisomeka kuwa nakupenda sana,mwanaume alipo muuliza huyu ninani,binti akajibu simjui nilikutana naye tuu barabarani,sasa kama nikweli walikutana barabarani yanini alisave namba yake?Sasa juzi mwanamke kampigia simu huyo mpenzi wake kuwa anahitaji mpenzi wake aende kwake,jamaa kweli kaenda kwa huyo mwanamke alipofika akakuta huyo binti anaelekea maliwatoni,wakakaa takribani masaa matatu wakiendelea na mambo yao,baada ya kumaliza jamaa anataka kuondoka,hisia zikamtuma apige simu ya yule mwanamke ili kuona kama inaita,alipopiga akagundua kuwa yule mwanamama alikuwa ameweka zile namba za call barring,alipoulizwa uliziweka mda gani akasema nilipomaliza kuongea nawewe na ukasema unakuja,akimuuliza kwanini uliweka binti anasema aliamua tuu,jee hapa kunausalama kwa huyu jamaa yangu au?Naombeni ushauri wenu juu ya hili swala!!!
 
Hapo hakuna usalama maana binti inaonekana anakaanga samaki wengi ndani ya chombo kimoja tena kwa wakati mmoja. Jamaa yako mwambie aangalie mambo mengine maana akioa mtu kama huyo, amani ndani ya nyumba itakuwa fumbo lisiloweza kufumbuliwa.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Hapo hakuna usalama maana binti inaonekana anakaanga samaki wengi ndani ya chombo kimoja tena kwa wakati mmoja. Jamaa yako mwambie aangalie mambo mengine maana akioa mtu kama huyo, amani ndani ya nyumba itakuwa fumbo lisiloweza kufumbuliwa.
The unseen is illustrated by the seen.
Tatizo nikwamba mapenzi yamemlevya yaani anampenda sana huyu binti,nimeshamshauri lkn anaamini kuwa huyu binti atabadilika tuu!!!
 
Vitu vingine viko wazi sana, haviitajia kutumia nguvu kuvielewa. Mwambie achukue hatua mapema, ataingia pabaya!
 
Ukiwa kwenye mapenzi mazito kamwe huwezi kushaurika ilishanitokea mimi kipindi cha nyuma niliwachukia rafiki zangu wote niakona wananionea wivu maana atm card nilimpa demu wangu eti ndio awe anapanga mipango wazazi wangu mwaka mzima hata vocha ya simu sikuwapa nikawaambia na majukumu tulikulaje raha ni safari za hapa na pale sikuwa na kitu kichwani kinachoitwa saving fanya maendeleo yaani mwanamke alikuwa ananiambia we mjinga mbona umechelewa namuambia im sorry yaani sijui nilikuwa nimefanywaje mpka nilijishangaa ila siku yaliponitokea gharama za kuomba msamaha kwa niliowakosea ilinicost nilionaje aibu?? Kwa hiyo huyo kaka yupo kwenye hicho kipndi atajakuja kuona madhara yake huku is too late
 
Tatizo nikwamba mapenzi
yamemlevya yaani anampenda sana huyu binti,nimeshamshauri lkn anaamini
kuwa huyu binti atabadilika tuu!!!

Aisikilize kwa makini hiyo sauti iliyomtuma kwako kuomba ushauri ila kama bado anaamini atabadilika,haya!
 
Duuh pamoja na ishara zote hizo bado jamaa hataki kuukubali ukweli. Mwambie kama sio ukimwi anaoutafuta basi kifo kabisa.
 
Kama amelewa na mapenzi,why aombe ushauri ?
Anyways, nimejaribu kuchukua nafasi ya huyo dada kwanza,nikagundua, ameshajua anapendwa sana so atafanya atakalo,af pili ana wapenzi wengi,af tatu hampendi jamaa kutoka moyoni,anampenda only bcos amejua anapendwa so anatimiza wajibu ile style ya basi tu.
Pili,jamaa anaelewa baada ya kuhisi, kuwa gf hana mpenz mmoja,ila kutokana na mapenzi..amejifunika macho coz amemuamini sana uyo dada kuwa asingeweza kumcheat,so ameupa nafasi zaidi moyo wake kuliko akili.
Ushauri; achague mawili na yampe utayari kufanya maamuzi;ajiulize je nikijua ana mtu ninachukua uamuz gani?then amkalishe bibie kitmoto,apate ukweli.
All the Best.
 
Ataamua pale atakapo kuja mkumkuta yuko chali na mwengine ndio akili na uwamuzi utamrudia,akah hata wivu hana?
 
Back
Top Bottom