Unahitaji utajiri wa fasta? Pitia hapa

Unahitaji utajiri wa fasta? Pitia hapa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,991
Reaction score
831,558
Habarini ndugu zangu wa JamiiForums,

Mada hii ni maalum kwa wale wanaotaka utajiri wa haraka bila kujali madhara yake

Kabla sijaendelea na muktadha wa mada lazima niwaambie na mlitambue hili kwa hakika Dunia hii ndugu zangu ni katili tena ni katili hasa na viumbe wake ni watu wabaya na wenye rohombaya hasa.

Usisadiki kamwe wala kuaminishwa na stori za vijiweni za mafanikio ya wengine kupitia uchawi, ushirikina au ulozi.

Kumbuka hili kwenye kila fanikio la mtu nyuma yake kuna sehemu ya siri ambayo kamwe hatakuwa tayari ku share nawe hata umpe nini kumbuka sana hili na lizingatie

Sasa basi hiki kitu kinachoitwa utajiri ninini? Utajiri ni kuwa na makaratasi mengi sana yanayoitwa pesa. Ukiwa na haya makaratasi maalum mengi mengi sana ndio unaweza kuwa na uwezo wa kufanya chochote utakacho kwa matamanio ya kawaida ya kibinadamu.

Tunatofautiana kiwango cha wingi wa umiliki wa haya makaratasi maalum yaitwayo fedha au pesa au shekeli na kwa kadiri unavyoyamiliki kwa wingi ndio uchoyo ubinafsi ubahili na rohombaya unavyokutamaki ni jambo la kiasili mno.

Pesa haina rafiki..pesa haina utu..bali pesa hujisimamia yenyewe...ndio maana unaambiwa ya kwamba PESA HUENDA KWENYE PESA..
Pesa ina mikondo yake
Pesa ina mifereji yake
Pesa ina formula zake
Pesa huambukiza pesa, kwa hiyo ukihitaji pesa ni lazima uwe na pesa na hili sio utani wala sio maskhara!

Tafuta kwanza kianzio ndio upate kiendelezo chake kwa njia hizohizo!

Usitegemee wala usijidanganye kama kuna njia za mkato kwenye utajiri. Huo utajiri ili kuupata unahitaji pesa pia, pesa nyingi, pesa za kuharibu na kuangamiza ili upate maradufu yake!

Utajiri unaoitwa wa mkato ama haraka unahitaji makafara makubwa, hakuna kitu kinakula pesa kama haya makafara, lakini ni lazima umpate mtakatifu mwenye dhambi la sivyo utaishia kupigwa.

Hakuna cha bure duniani na kila mtu ni mhitaji. Usidanganywe na waganga wa mitandaoni na wale wanaotoa pesa za majini. Majini hayaendeshwi na kiumbe dhaifu aitwaye binadamu.

Katika hali hiyo uliyo nayo na changamoto ulizonazo kwenda kwa mganga akupe dawa ya utajiri ni kujitia dhambi bure na kumfaidisha mganga.

Utajiri wa pesa ni mali ya mkuu wa anga na ili uupate ni lazima utoe sadaka kubwa. HAKUNA CHA BURE DUNIANI. Kishapo uingie mikataba yenye masharti magumu na mazito.

Matajiri wetu kila mmoja ana siri yake binafsi na wana siri za jumla kulingana na kiwango cha ukwasi wao.

Kama bado hata hela ya kujihudumia inakupiga chenga usijihangaishe kutafuta utajiri huu wa shortcut. Utaishia maumivu ya kutapeliwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom