Unahitaji mtoto wa Kambo au Kumuasili?

Dkt. Gwajima D
Ni wazo zuri sana na nimelipenda bila pasi na shaka.
Naomba kuuliza, je, utaratibu huo pia unahusisha katika uasili kwa watoto pacha?

Pia, katika vigezo vikuu vya kuasili, ni lazima kutakuwa na kimoja au viwili ambavyo viko strong na ndio mara nyingi ninyi kama wizara huwa mnaangalia kwa umakini sana.
Unaweza kubainisha vigezo vikuu?
Yamkini, ninajua hayo yaliyoorodheswa, ila hujasemea suala la umri, mazingira yapi ni rafiki sana kwa uasili wa mtoto/watoto.
Na je, naruhusiwa kuasili kuanzia watoto wangapi?
Na pia, hata wa kariba lingine mf. wa kikorea, wa kizungu etc, almradi tu nimemkuta kituoni?

Asante.
Naomba niyachukue maswali yenu yote kesho Kamishna wa Ustawi ayajibu vizuri kisha nitapandisha hapa majibu yote. Wengine nao waulize tu. Ahsanteni Sana kwa mwitikio wenu🤝
 
Naomba niyachukue maswali yenu yote kesho Kamishna wa Ustawi ayajibu vizuri kisha nitapandisha hapa majibu yote. Wengine nao waulize tu. Ahsanteni Sana kwa mwitikio wenu🤝
Nawe asante sana mkuu kwa uwepo wako hapa Jamii forums.
Nina imani wengi wetu tumepata ABC's ambazo huenda hatukuwa na uhakika nazo au maelezo ya kina.
Nami nikutakie kazi njema na wasaa mzuri wa kututumikia sisi watanzania kupitia Wizara yako tukufu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye makundi maalum.
Asante.
 
Muda ni Mwalimu mwema kwa Kila swali. Tuzidi kupambanua kile Mungu ameweka ndani yetu, muda wetu ni mfupi na unapita kasi, saa inakuja ya kuuona uso wake na kupimwa kwa mizani yake. Nakutakia Heri na Baraka za Mungu. 🤝
🙏
 
Asante mama kwa muongoza huu... Mungu akubariki. Maana kuna mtoto ni natamani kumchukua ila nilikuwa sijui naanza wapi
Naomba kuuliza hivi unapeleka ombi baada ya kutaka kumchukua mtoto fulani au unapeleka maombi wao ndo wanapoint mtoto yeyote wanayemtaka unapewa !
 
Ila we mama ni smart sana,na hapa umewasaidia wengi maana walikuwa hawajui wanaanzia wapi.Salute!Doctorate uliisotea.
 
Hongera mama! Nawaza tu

hivi yule wangu wa nje hatuwezi tukampa lift akaja home kama mtoto wa kambo /kuathiri(wife ajue hivo), ila Mimi najua nimeleta mwanangu, kwa hatua zotezote kama alivoainisha mama yetu pale,

wizara itakuwa imetukomboa wanaume
 
Hii program ni nzuri sana kuwasaidia watoto kupata malezi ya familia na kuwa na nyumbani kwao. Hakuna kitu kibaya kama mtoto kukua akiwa hajui kwao ni wapi, hajui nani wa kumwita baba nani wa kumwita mama.

Pongezi sana kwako na kwa wizara kwa kulitambua hili mheshimiwa waziri.

Naomba kuongezea pia nguvu ziongezwe pia eneo la mafunzo kutoa elimu kwa mabinti wanaojiingizia katika mahusiano na kupata watoto kabla ya ndoa na hatimae kupata watoto bila baba kuwapo karibu hii pia ni changamoto ambayo inatakiwa kufanyiwa utatuzi wa kudumu kupitia elimu ya madhara ya kuzaa watoto nje ta ndoa yaani uzazi bila mpango.
 
Hili neno kambo lina ladha na vimelea vya unyanyasaji, mateso kutokuwepo amani na furaha, nashauri litafutwe neno jingine kama inavyoanza kuzoeleka kwa maneno Mama, Baba, Kaka wa hiari
Ni mtazamo na fikra zako tu, nadhani wewe ndie unatakiwa kubadilika na kupewa elimu kuhusu matumizi sahihi ya neno kambo.
 
Wasaalam Wana Jukwaa wote.

Kwa aliyebarikiwa neema ya Kulea watoto kwa malezi ya kambo au kumuasili kisheria awe wake;

UTARATIBU;

Baada ya kuwasilisha maombi Halmashauri;

1. Afisa Ustawi wa Jamii atakutembelea na kufanya tathmini.

2. Taarifa itawasilishwa kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii Wizarani.

3. Iwapo hakuna hoja pingamizi, Kamishna atatoa kibali kwa mwombaji kumtambua mtoto.

4. Afisa Ustawi wa Jamii ataendelea kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya familia iliyomtambua mtoto na kuanza kumlea malezi ya kambo.

5. Taarifa ya maendeleo ya malezi ya kambo baada ya mathalani miezi sita hivi itawasilishwa tena kwa Kamishna, kwa ajili ya kuthibitisha kuwa maendeleo ya malezi ya kambo ni mazuri, hakuna changamoto hivyo, kibali cha kwenda mahakamani kuomba ridhaa ya Kuasili mtoto huyo kitatolewa.

Hakuna malipo yoyote epuka ulaghai wa wasio waadilifu.
well done waziri dr.gwajima
 
Back
Top Bottom