UNAHISI NI LAZIMA KUVAA NGUO MPYA WAKATI WA SIKUU....

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
207
453
Dar es Salaam. Ni lazima kuvaa nguo mpya wakati wa sikukuu? Ni swali linalotawala nyakati za sikukuu za mwisho wa mwaka, ambapo kwa wengine bila kuvaa nguo mpya, mwaka unakuwa haujaisha.

Japo imezoeleka kwa watoto kudai mavazi mapya nyakati hizi lakini watu wazima wanasema kwao sikukuu ni kila siku wapo baadhi hupendelea kuvaa nguo mpya nyakati za sikukuu.
Akizungumzia dhana ya nguo mpya nyakati za sikukuu, Mwanasaikolojia Ramadhani Masenga kutoka Mental Hygine Instute ya Dar es Salaam amesema, kwa kawaida kuvaa nguo mpya siku za sikukuu ni utamaduni ulioanza miaka mingi iliyopita


“Sababu ya kuja na suala hilo kwanza nguo mpya huwasilisha ufahari na furaha juu ya siku husika.
“Yaani mhusika au wahusika wakivaa nguo mpaka hujihisi na kujiona wamefanya jambo kubwa katika siku maalumu kitu kinacho chochea furaha na amani kwenye nafsi zao,” amesema.
Msaikolojia huyo amesema, nguo mpya ni ishara ya kuonesha kuachana na shida na matatizo ya siku zilizopita.
Amsema lengo la wahusika kuvaa nguo mpya ni ni ishara ya kutaka kila kitu katika maisha yao kipendeze na kuvutia sawa na upya wa nguo zao.
“Kitu kingine nguo mpya katika jamii zetu hususani kwa watoto huchangia kuonesha umaalumu wa siku husika na kusaidia kufanya akili zao zihamasike kwa furaha,” amesema.
Louis Samweli mkazi wa Mabibo Dar es Salaam mzazi wa watoto wawili amesema, mtu mzima kuwaza kuvaa nguo mpya nyakati za sikukuu ni jambo lisilo na maana.
Lakini amesema kwa watoto, nguo mpya kwa nyakati za sikukuu zinawaondolea unyonge.
“Kwa watoto sikukuu ina maana kubwa, mtoto anaporudia nguo na kuchangamana na wenzake hata uchangamfu wake hauwi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom