Nachotaka kukushauri ni kuwa usipotoshwe na huruma yako kwake, ishi naye kama wewe.... Yaani usibadilishe tabia zako au maisha yako kwasababu yake,una haki ya kukasirika, kugomba, kucheka, kutania nk
Kwanini nasema hivi....
1. Itasaidia kukulinda wewe binafsi usije kuharibika kisaikolojia, msaada mwema ni ule usiokuwa na madhara kwako.
2. Huwezi kumsaidia kwa staili hiyo, kuna wakati hata naye anaweza akahisi unapretend.
3. Matatizo mengine yanatatulika kwa nguvu ya Mwenyezi Mungu tu, hivyo elekeza nguvu kwenye ibada pia.
4. Na km tatizo ni saikolojia imeharibika basi jua huna huo utaalamu wa kulimaliza, linahitaji wataalamu wa afya ya akili.