Unafiki wa Zitto Kabwe na suala la Posho - Lema

Unafiki wa Zitto Kabwe na suala la Posho - Lema

Status
Not open for further replies.
ni kweli lema ameamua kukigawa chama yaani wanafiki na wapambanaji wa kweli..

umeona eee huu ujingaaaaaa jamaa hana busara hata kidogo bora ccm waendelee kutawala kulioko kuwa na viongozi kama lema
 
Sasa hapa mnajiaibisha. Kuna haja gani ya kuvuana nguo hadharani kwa nyie viongozi?
Lema elewa kuwa Zitto ni kiongozi wako kwenye chama na Bungeni pia.
Kuna viongozi wa juu zaidi yenu ambao wangeweka mambo sawa.
Tatizo la Lema ni Ubabe usio na maana badala ya kujenga wewe unabomoa chama.
Nakumbuka uliwahi kugombana na aliyekuwa Mwenyekiti wa CDM Mkoa wa Arusha kuhusu kuuza vitu ambavyo vingeuzwa na chama.
Na pia kujitafutia wagombea udiwani wa kata nne uliopita badala ya vikao halali vya chama.
Ndugu lema usilewe umaarufu.
 
Dah! Sasa wewe Lema unaleta hapa hili ili iweje? Kama na wewe so kutafuta sofa ambazo hunazo. Lema Zitto sio daraja lako, hebu weka CV yako hapa tupime Kama wewe unakiwango cha kushindana na zitto. Acha chuki za kijinga. Unajiabisha buree, mtaiwa CDM kwa upumbavu wenu.
 
Last edited by a moderator:
LEMA,

Wewe ni mbunge wangu na nilishiriki kukupigia kampeni na kukuchagua vilevile ila nasikitika sana ninapoona unapoteza mda wa kumshambilia Zitto ambaye kimsingi anayoyafanya anayajua yeye na wananchi wa jimbo lake.

Ningefurahi kama ungekua unatoa ahadi kama hizi kujua matatizo ya jimbo lako angalia jalala lilipo tazama afya na maisha ya wananchi wako je unakumbuka ahadi ulizotuahidi watu wa Arusha? Umetekeleza ngapi? Unadhani zitto nae akija humu akianza kuzungumza mabaya na mabovu yako JF patatosha? Kwahiyo unataka kua mwenyekiti wa PAc ili ulipwe kama zitto? Namwelewa zito baada ya kuona anapokea malipo mengi aliamua kutoa kiasi ili wananchi wanufaike hoja yako utaitekeleza kama CHADEMA kitaingia madarakani kama kuachana na posho ndio ilikua hoja ya upinzani kwanini wewe na wengine wa upinzani bado mnachukua? Mimi naona unaleta majungu na huna hoja JIPANGE.

Zungumzia mambo yanayoendana na Cheo chako, Umri wako bado hujakomaa kisiasa kaka hivi hamjengi chama mnakibomoa chama!
 
Sasa ndiyo nimeamini kuwa kama uliwahi kuwa mhuni huwezi kuacha uhuni,kama ulikuwa mwizi hutaacha ,kama ulikuwa jambazi hutaacha ,kama ulikuwa mropokaji hutaacha safari moja huanzisha nyingine kazi bado ipo.
 
Kwani Zitto akikataa posho bungeni na kuchukua nyinginezo, ninyi wabunge wengine mnadhurika nini mpaka muanze kushusha hadhi ya CHADEMA kwa migogoro na kunyosheana vidole kusiko na tija?
 
Godbless J Lema nikwambie tu kuwa: two wrongs, don't make a right!

Hoja ya msingi ni kuwa wewe unatetea maslahi ya wabunge yaboreshwe zaidi ya hivi ilivyo sasa.

1) Tuambie wewe kama sio mnafiki, ni kwa standard gani ya maisha milioni 12 kwa mwezi haitoshi kwa mazingira ya Tanzania mbali ya mijiposho mingine ambayo unaijua wewe?

2) Wewe kama sio mnafiki, ungeungana na wabunge wengine wa CHADEMA kutetea kufutwa kwa hizo posho zenu na hizo nyingine wanazochukua hao akina Zitto.

3) Inaonekana una bif zaidi na Zitto kuliko hoja ya posho.
Ningekuelewa ungekuja na hoja ya kutaka kufutwa kwa hizo posho nyingine ambazo akina Zitto na wenzake wanapokea kwenye hivyo vikao ulivyovitaja. Na wala sio kudai na nyie muongezwe only kwa sababu wenzenu wanapata nyingi zaidi kuliko nyie.

4) Zitto njooujibu hoja hii - 700k per day! Hii ni kama sitting allowance ya Non Executive Directors kwenye vikao vya bodi mbali mbali za makampuni.

Kama Godbless J Lema anazungumzia Director's fee hiki kitakuwa ni kitu kingine na debate yake ni tofauti na posho za watumishi wa umma. Clarity inahitaji kwenye hili kabla ya kuwa na uwezo wa kuchangia.
 
Kwani Zitto akikataa posho bungeni na kuchukua nyinginezo, ninyi wabunge wengine mnadhurika nini mpaka muanze kushusha hadhi ya CHADEMA kwa migogoro na kunyosheana vidole kusiko na tija?

soma vizuri uone kama zitto apokei posho tena kubwa tu
 
Lema, unazidi kuzama kwenye tope tu bora ungekaa kimya.

Ndugu inamaana kauli ya Juzi ya Zitto kuhusu kushangaa wabunge kugombania posho hukuisikia?
Je mwananchi walipoandika mbunge wa chadema anayelilia posho hukuisoma?

Mimi naamini amejibu hoja za juzi na amejipambanunua kuwa yeye ni Mpenda posho na hatoacha.

Kifupi anatimiza ule msemo wa kuondoa Boliti kwako kabla ya kibanzi kwa jirani na mfano mzuri wa bomba la maji ameutoa.
 
Kuna mahali nimesema ni msimamo mzuri kutenda unachohubiri.Hivi kuna mbunge gani aliyewahi kugomea mshahara wake kwa kuwa haukatwi kodi?Mishahara ya wabunge haikatwi kodi na hakuna hata mmoja aliyewahi kugomea.I stand to be corrected!

Hata mishahara ya wabunge kwa kiwango cha sasa sijawahi kuona mbunge aliyetaka mshahara wake upunguzwe kama alivyofanya Mwl. Nyerere kwa kupunguza mshahara wake kutoka Sh. 5000 hadi Sh.4,500.

Je kinachofanyika ni uzalendo ama ni unafiki?

Nimeshangaa sana kusikia NSSF ambalo ni shirika la umma linatoa malipo ya aina hii.

Nakumbuka Dr.Ramadhan Dau alipoteuliwa kuwa mkurugenzi alisifiwa sana kumbe kuna maslahi tena?Duh

Nyie wanasiasa siyo watu kabisa! hamuwajui wananchi wakati wa matatizo yao bali mnawajua mkiwa kwenye vyombo vya habari
 
Chambua hoja ya mleta mada kwa facts kama alivyofanya.

Hakuna kutafuna maneno kinafiki maana hata mimi siasa za kinafiki siziwezi kabisa kabisa

hoja gani hayo aloandika yanasaidia nini katika kile ambacho wewe ben8 kila siku unakipgania zaidi ya kubomoa
 
Nakubaliana na aliyesema viongozi waliopo Chadema wamefikia "saturated point" ya kukiendeleza Chama, kwa hiyo kilichobaki ni falling-down kama wataendelea kuwa wao. Hii ni hatari sana kwamba 2015 CCM njia nyeupe? Sasa kama nyote ni watetezi wa wananchi, iwapo Zitto anachukua baadhi na ww unachukua zote, busara ni wewe walau kumfikia Zitto alipo kisha umtangulie kwa hatua moja mbele yake ili naye akufuate. mwendo uwe huo "Gradual" hadi posho zote mzifute, sasa kama hauko tayari kuachia hata hizo kidogo, ndio utazifuta kweli hizo Mheshimiwa GODbess Lema?
 
Last edited by a moderator:
Mh Lema yatosha sasa, hivi hamna vikao vya chama, ni kwanini unaamua kuyazungumzia haya hadharani?, najua umekwazika, lakini jaribu kupima upya hatua unazozichukua kuyaanika haya hadharani. Unatuvunja moyo sana isee, yaani sijui kama 2015 kama tutafika. Taafadhali tafadhali embu tafuta njia nyingine ya kutatua haya sio kwenye mitandao.

Yaani ni sawa baba na mama kugombana mbele za watoto pindi wanaponyimana! haipendezi hadharani namna hii!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom