Unafiki wa wazanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unafiki wa wazanzibar

Discussion in 'Sports' started by Bazazi, Feb 3, 2009.

 1. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,025
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Wajameni hebu angalieni hiki kipande cha taarifa ya gazei la habariLeo la tar 31/01/09 kuhusu mgogoro kati ya TFF na ZFA;

  Vyama hivi viwili vimekuwa vikitofautiana kila mara , inakuwa kama maji kupwaa na kujaa. Lakini tofauti na siku za nyuma, ambapo baadhi ya viongozi wa vyama hivyo walihusika ktk kutupiana lawama, safari hii sual la TFF na soka la Zanzibar liliibuka ktk kikao cha baraza la waakilishi.
  Ktk kikao hicho ilielezwa kuwa TFF haitendi haki kwa maendeleo ya kandanda Zanzibar, kauli ambayo ilitolewa na na nibu wazir wa habari, utamaduni na michezo-zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo wakati akijibu swali na Said khelef Ali (CCM, Bubwini) alyetaka kujua juhudi za SMZ ktk kuinua soka, ikiwemo ushiriki wa wachezaji wa Zenj ktk timu ya taifa.
  "Hatna furaha na jinsi TFF ilivyo, ninasema hili wazi kuwa Zenj haifaidiki naTFF, chombo hiki kinapaswa kusimamia pande zote 2. Lakini tutaendelea kupigania haki zetu dani ya TFF" alisema Naib waziri. Alisema Tff hasaidii zenj ktk mambo mengi ikiwemo fedha za kila mwaka toka FIFA, nahaishiriki ktk kutafuta wachezaji bora kwa ajili ta taifa stars.

  Alienda mbali zaidi aliposema TFF inafikiri ni ya Bara pekee na kwama mtizamo wa TFF kwa Zenj unamkatisha tamaa hata kocha Marcio Maximo kwenda huko kutafuta vipaji baada ya kuiona timu ya vijana ktk mihuano ya challenge huko uganda. Mambo mengine inayolalamikiwa TFF ni kuwa inapanga bajeti ya Maximo kzungka ikoa yote ya Bara pekee, haimpeleki ZANZIBAR"

  Wanajamii hivi hawa watu wanatuona watanganyika hatuna akili ya kutosha au vipi? Hivi michezo ni suala la muungano? je TFF ni ya muungano? Kwanini hela ya TFF ukiacha kuoka fifa zitumike kuinufaisha zanzibar ilhali wanachama chao ZFA?

  Wanajukwaa hasa kutoka Zanzibar naomba mnisaidie ktk maswali yangu hayo
   
 2. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,025
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Mhe Mod; hii mada ni ya hapa kwani mezungumzwa jengoni na sio michezo kama baadhi ya watu watakavyofikiria, plz usiihamishe.

  Wajameni hebu angalieni hiki kipande cha taarifa ya gazei la habariLeo la tar 31/01/09 kuhusu mgogoro kati ya TFF na ZFA;

  Vyama hivi viwili vimekuwa vikitofautiana kila mara , inakuwa kama maji kupwaa na kujaa. Lakini tofauti na siku za nyuma, ambapo baadhi ya viongozi wa vyama hivyo walihusika ktk kutupiana lawama, safari hii sual la TFF na soka la Zanzibar liliibuka ktk kikao cha baraza la waakilishi.
  Ktk kikao hicho ilielezwa kuwa TFF haitendi haki kwa maendeleo ya kandanda Zanzibar, kauli ambayo ilitolewa na na nibu wazir wa habari, utamaduni na michezo-zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo wakati akijibu swali na Said khelef Ali (CCM, Bubwini) alyetaka kujua juhudi za SMZ ktk kuinua soka, ikiwemo ushiriki wa wachezaji wa Zenj ktk timu ya taifa.
  "Hatna furaha na jinsi TFF ilivyo, ninasema hili wazi kuwa Zenj haifaidiki naTFF, chombo hiki kinapaswa kusimamia pande zote 2. Lakini tutaendelea kupigania haki zetu dani ya TFF" alisema Naib waziri. Alisema Tff hasaidii zenj ktk mambo mengi ikiwemo fedha za kila mwaka toka FIFA, nahaishiriki ktk kutafuta wachezaji bora kwa ajili ta taifa stars.

  Alienda mbali zaidi aliposema TFF inafikiri ni ya Bara pekee na kwama mtizamo wa TFF kwa Zenj unamkatisha tamaa hata kocha Marcio Maximo kwenda huko kutafuta vipaji baada ya kuiona timu ya vijana ktk mihuano ya challenge huko uganda. Mambo mengine inayolalamikiwa TFF ni kuwa inapanga bajeti ya Maximo kzungka ikoa yote ya Bara pekee, haimpeleki ZANZIBAR"

  Wanajamii hivi hawa watu wanatuona watanganyika hatuna akili ya kutosha au vipi? Hivi michezo ni suala la muungano? je TFF ni ya muungano? Kwanini hela ya TFF ukiacha kuoka fifa zitumike kuinufaisha zanzibar ilhali wanachama chao ZFA?

  Wanajukwaa hasa kutoka Zanzibar naomba mnisaidie ktk maswali yangu hayo
   
 3. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sio unafiki, ukiingia katika muungano bila pande husika kukubaliana japo mambo fulani fulani muhimu, ujue kutatokea migongano. Muungano ni kama ndo, unadhani ndoa ya kulazimishwa ni rahisi kudumu. Hapo ni katika michezo tu, yapo kibao mengine kwa mfano mgawanyo wa maliasili (madini, mafuta na gesi), teuzi za mabalozi nk. Hivyo muungano wa Zanzibar ni muhimu kuutumia tuelekeapo kwa Shirikisho la Afrika Mashariki, ama tutarudia kosa lile llile kama viongozi hawatapata maoni ya wananchi.
   
 4. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  NAdhani tatizo haliko TFF bali kwa ZFA na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutoelewa kuwa iwapo TFF ikitoa msaada au kuwa na programu ya soka Zanzibar ni hisani tu. Hii ni kwa Kuwa FIFA inaitabua TFF tu na si vyama vingine vinavyohusiana na TFF. Kwa maana hiyo ZFA/Zanzibar wakipata msaada wowote kutoka TFF ni hisani tu; ZFA ni wanachama wa CAF na ikiwa kuna programu au msaada wowote kutoka CAF basi wanapata kama vile wanavyopata TFF maana wako sawa mbele za CAF.

  Suluhisho ni ZFA na Serikali ya Zanzibar kutafuta kwa nguvu zote kutambuliwa na FIFA ili waweze kuwa wanachama.
   
 5. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Yakhe Bzazazi tusha wazaoea hawa ndugu zetu.Kulalama kwao ni jadi.Wanikumbusha wakati wa utoto nikitamani kuvaa kiatu namba 10
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Awali ya yote inabidi utuombe radhi sisi wazenj kwa kutuita wanafiki ilhali hujui chochote kuhusu mstakabala wa soka la Tz. Aidha maswali yako yote hapo juu yanaonyesha ni kwa namna gani hujui kinachoendelea katika TFF na ZFA. Lakini kwa kuwa unataka kufahamishwa nitakuelezea kwa ufupi tu, na iwapo unahitaji mengi unaweza kutembelea ukumbi wa Michezo hapa JF na kuna bandiko la kona ya Soka la Zenj na mabandiko mengine ambayo yanaelezea matatizo kati ya TFF na ZFA... Haya yote yapo ndani ya JF.

  ZFA ni sehemu ya TFF na inawajibika kupatiwa mgao wa FIFA ambao hupewa TFF kwa niaba yao. Jumla ya dola 250,000 hutolewa na FIFA kwa soka la TZ kila mwaka, na ZFA kwa muda wote imekuwa ikinyimwa fungu lake kutokana na mgao huo wa FIFA. Zaidi TFF imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya soka visiwani huo kwa kuvaa sura mbili mbili. Pale kwenye neema uamua kukaa kimya kama vile hakuna kitu kinachoitwa ZFA, aidha wanapokuwa na shida na hasa kama suluhisho litakuwa Zenj hujitia kuitambua ZFA. Unaweza kuangalia pale Maximo alipokuwa anahitaji kocha wa magolikipa wa Taifa Stars na alimpendekeza Mchezaji wa zamani wa Taifa Stars ambae ni mzenj na katika kipindi hicho alikuwa na kibarua cha kufundisha soka visiwani humo. TFF walikwenda mbio sana kumpata kocha huyo tena kwa njia zakinyamela. Sasa hapa unaweza kuona ni nani Mnafiki... Watu wa Bara ama Visiwani?

  ZFA ambayo bado kupata uanachama wa kudumu toka CAF, ambao ni muhimu ili kuweza kutambuliwa na FIFA hivyo kutokuwa na sababu ya kubanana na TFF. Hadi siku ambayo FIFA itaitambua ZFA, ni wajibu wa TFF kuona kwamba ZFA inapata mgao wake na ni wajibu wake kuona kuwa kuna uwiano sawa katika maendeleo ya soka katika sehemu hizi mbili za muungano.
   
  Last edited: Feb 3, 2009
 7. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwanza kichwa cha Thread hii si stahiki na baada ya kusoma posting ya huyo bwana aliyeleta hii thread nimepata mtazamo kuwa huyu bwana pengine anahitaji kueleweshwa au pengine ni fungu la wale wanaopenda kuongozwa na hisia zao.
  Nini unafiki uliopo hapa? Nafikiri suala la Muungano limeshazungumzwa sana na kuonekana udhaifu wake na kwa bahati mbaya upande wa Bara mara nyingi uko katika advantage. Suala la TFF na ZFA ni tatizo pia la muundo wa Muungano unaofanya Bara kutumia jina la Tanzania kwa manufaa ya Tanganyika pekee. Hakuna tofauti kati ya Tanzania na Tanganyika nakwa maelezo ya huyu ninayemnakili hapa hakuna mpaka uliotenganisha kati ya TFF na Bara bali ni kuendelea kutumia jina la Tanzania kwa manufaa ya upande mmoja. Hivyo Dola 15,000 kwa mwezi anazolipwa Maximo ni pesa za Bara au pesa za Tanzania ukijumuisha na Zanzibar? Huu ni ufafanuzi mdogo tu wa kuonyesha kuwa TFF ilibidi igawane na ZFA shughuli za soka. Kama ilivyo serikali zilizomo kwenye Muungano (SMT na SMZ) ndivyo ilivyo TFF na ZFA na kama kuna utaratibu wa matumizi ya pesa za Muungano kwa pande mbili basi panalazimka pia kuwepo na mpangilio wa matumizi kwa kile kinachokuja kwa jina la Tanzania kupitia TFF. Kuondosha kuzongwa na kupata uhuru kwaTFF kutumia itakavyo kwa manufaa ya Bara tu basi ipo haja kwa TFF kuacha unafiki na kuisaidia Zanzibar ijiunge kama nchi huru (Jambo ambalo TFF na Watanzania wengine hawako tayari. NAFIKIRI SI SAHIHI KUWAITA WAZANZIBARI WANAFIKI KWA HILI KWANI WANADAI HAKI YAO YA KIKATIBA>
   
 8. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alternatively. ni kuinyan'ganya majukumu TFF ambayo imeiyapora kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hiyo inaweza kufanyika kwa kuunda Chombo chengine huru cha Michezo chenye sura ya Jamhuri ya Muungano (tofauti na ZFA na TFF) ambacho kitachukuwa majukumu pamoja na yale ya uanacha wa FIFA na kuwajibika kwa niaba ya wanamichezo wote katikameneo la Jamhuri. TFF na ZFA zote zitabaki bila uanachama wa FIFA na zitaendeleza soka katika sehemu zao (Bara na Zenj) bila ya kubughudhiana na na kuingiliana.
   
 9. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawalalami ovyo. Wao ni nchi walioamua kwa makusudi kuingia katika Jamhuri ya Muungano. Wanapokosa haki zao za Ki-nchi lazima wazipiganiye.
   
 10. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145

  Kibu, kama ZFA ni sehemu ya TFF basi haina tofauti na TEFA na kwa uwa TFF inawajibika kitaifa na si kimkoa. Kuhusu ZFA kunyimwa fungu lake, una uhakika ni Dola ngapi na katika mgao huo kiasi hicho cha pesa huainishwa?

  Suluhu ni moja tu ZFA itafute uanachama FIFA kama ilivyofanya kuutafuta wa CAF
   
 11. M

  Mkuu Senior Member

  #11
  Feb 3, 2009
  Joined: Jan 1, 2007
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wakati walipo ambiwa hao hao Zanzibar sio nchi walipiga keleleeeee sana sasa je munaamini kama hakuna nchi hapo? kila kilakitu lazima mabwana wakubali kwanini musikubali moja tu kusuka au kunyoa kwani sasahivi hakuna majibu ya kuwajibu watu wenu katika kila idara
   
 12. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Bahati mbaya hamko tayari kwa hilo na hapa ndipo neno UNAFIKI linapostahili. Eti ZFA ni sawa na TEFA, ni sawasawa na wale wasemao Zanzibar ni sawa na Mwanza
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Na hasa mabwana wenyewe wakiwa njaa yao wanaijali hyata kusahau wake zao.
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Feb 3, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Michezo sio suala la muungano, katika hati ya muungano kuna baadhi ya mambo ambayo hutekelezwa na serikali ya jamhuri ya muungano na yaliyobaki hutekelezwa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar kwa upande wa zenji.Ndiyo maana utaona kuwa kuna wizara za michezo pande zote; zanzibar na 'tanganyika'. Zanzibara kuna waziri wake Juma shamhuna na naibu wake thabiti kombo ilhali 'tanganyika' kuna waziri wake mchukika na naibu wake bendera.
  Kwahiyo wazenji hawana sababu ya kulalama saaaana; kwanza wao ni nchi lakini pili wanayo wizara yao ya michezo, wanacho chama chao cha soka zfa. Badala ya wazenji kujadiliana kutafuta maelewano baina ya serikali yao na zfa wanabaki kuilaumu tff.Kila kukicha tunashuhudia ugomvi na malumbano baina ya zfa na shamhuna, ni lini watazungumzia maendeleo ya soka?wanategemea soka lao likue kimiujiza?
  Pamoja na mapungufu mnayoyaona kwa mleta hoja, suala la wazenji kuwa wanafiki halijifichi, na mifano ni mingi sana wajameni acheni kulalama.
  acheni migogoro mshirikiane kuinua soka la zenji.Kila siku ni zfa ni purukushani tu mara shamhuna mara maulid hamad mara hafidh tahir, yaani vurugu tupu.
   
 15. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,025
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Waheshimiwa iwe itakavyokuwa; bado tatizo langu lipo palepale kwanini Wazanzibar hupenda kulalamika sana bila kuangalia ukweli halisi? Bado naamini na najua kwamba TFF (na michezo kwa ujumla wake) sio suala la Muungano sasa TFF inazoroteshaje Soka la Wazenj? Ukiondoa FEDHA TOKA FIFA kipi kingine Wazenj wanataka Bara- TFF imlipie gharama maximo kwwenda Zenj kutafuta vipaji! nini kazi ya ZFA.

  Ni kwanini ndugu zangu Wazenj mnauhusudu huu msemo "CHAKO CHETU NA CHANGU CHANGU"? Nadhani wakati sasa umefika kuyaweka mambo sawa kama kuna ulazima wa kuwa na SMZ (au muungano kabisa- siipendi hii).

  Aidha nasikitika bado Wazenj hamjanishawishi hadi niweze kuomba radhi na kulifuta neno WANAFIKI. Hivyo bado nimesimama na mawazo yangu hadi hapo baadaye.
   
 16. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #16
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu Ndivyo Ilivyo, kuna usemi, tena toka kwa hao ndugu zetu usemao-CHANGU CHANGU,CHAKO CHETU.
  Msemo huu haukutoka bara!!
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  [FONT="Comic Sans MS[SIZE="2"][/SIZE]"]Njaa si kitu cha kuchezea. Leo wanalalamika kwa nini TFF haiko Zanzibar wakati kwenye mafuta ya alinacha hawataki kuingiliwa![/FONT]
   
 18. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #18
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Bazazi,

  wewe umeshafanya conclusion na kuwaita wanafiki. Nadhani huwatendei haki. Kwani hiyo kauli ya kiongozi mmoja ndo inawafanya wazanzibari wote wawe wanafiki? Unawaonea mkuu. Ingekuwa hivyo wabara wote tungekuwa wanafiki maana viongozi wetu wanapenda kutoa kauli tatanishi sana. Hivyo basi wewe mlaumu huyo waziri na siyo kuwabebesha mzigo wazanzibari wote.

  Harafu wewe unauliza swali kama michezo ni swala la muungano au la, well wapo wajuvi humu watakujibu...lakini kama ungependa kujua na ulikuwa hujui..kwa nini umefanya conclusion kwa ku-base kwenye facts ambazo hujui? Kama michezo siyo swala la muungano nadhani hata hao wabunge ingebidi wafanye homework yao kujua kama kweli TFF inamamlaka mpaka ZANZIBAR au la.. AND I want to give them benefit of doubt kwamba TFF inawajibika huko in one way or another... (si kuna kitu kinaitwa TAIFA STARS??). Anyway I dont know much.

  Fundi ukiangalia vyema hawa jamaa wanahaki ya kufaidi mafuta yao bila kuingiliwa na mafisadi wetu wa bara...... Hivi dhahabu wanafaidi chochote? (anyway hata wabara najua hatufaidi lolote)..labda wanaweza kujifunza makosa tuliyoyafanya ya kugawa raslimali zetu. Tatizo viongozi wenyewe ndo akina Karume..ndo wale wale kama wa kwetu! So hata wakikaa nayo, sijui kama watafaidi lolote.

  Yaani Zenji ina potential ya kuwa Monaco ya Africa..lakini ndo hivyo...uccm na uccm...ndo umewajaa hawa jamaa zetu. Just like we..in bara..So..vumilieni mkae na ndugu zenu wabara mgawane umaskini tuu!
   
 19. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #19
  Feb 3, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Kitu nachokiana hapa ni uzembe tu. Mimi kama mpenzi wa soccer, mpaka sasa nasikitishwa jinsi ya chombo chenyewe kinavyoendeshwa.

  Pamoja na malalamiko yalitoka Zanzibar, sioni kama hiki chombo kimewahi kuendeleza soccer Tanzania bara.

  Kuna vyombo vingi tu vya kitaifa ambavyo havifanyi kazi kwa ufanisi. WaZanzibar wakivilalamikia, wanaonekana wanafiki. Lakini swali la kujiuliza je hivi vyombo vina manufaa gani sisi watanzania bara ?

  Haya masuala ya kutafuta umoja ambao unawaziba watu uhuru wa kusema unaturudisha nyuma.
   
 20. S

  Sabri-bachani Member

  #20
  Feb 4, 2009
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
   
Loading...