Unafiki wa viongozi wa CHADEMA huu hapa

Unafiki wa viongozi wa CHADEMA huu hapa

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,901
Reaction score
20,417
1. Walikuwa wanapinga ufisadi na sasa wanaukumbatia na kuwakumbatia mafisadi. Fisadi Mkuu ndo mgombea wao wa Urais.

2. Walikuwa wanasisitiza kura za siri wakati wa Bunge Maalum la Katiba lakini wao wanatumia kura ya wazi kwenye Uteuzi wa mgombea Urais.

3. Walisema hawapokei makapi ya CCM na sasa wanayapokea na wanahamasisha yaendelee kujiunga na CHADEMA. Mengine yamepewa mpaka nafasi ya kugombea nafasi ya Urais, ubunge na udiwani.

4. Walisema kuwa CCM ni chama cha Wazee lakini kwa sasa wanamsimamisha mzee na mgonjwa kuwa mgombea Urais.

5. Walisema kuwa wafuasi wa CCM mitandaoni wanatukana sana lakini kwa sasa wao ndo wanaongoza kwa Kuporomosha matusi.

6. Walisema kuwa wanaohama CHADEMA ni wasaliti lakini wanaohamia CHADEMA ni wazalendo.

7. Wanasema Lowasa alikuwa mchafu ndani ya CCM lakini amekuwa msafi ndani ya CHADEMA.

8. Walisema CCM iondoke madarakani kwa sababu inakumbatia ufisadi na mafisadi lakini wao wanafadhiliwa na mafisadi na wauza unga.

9. Walisema CCM imechoka hivyo iondoke madarakani wakati wao wapo hoi bin taaban na karibuni watapelekwa ICU.

10. Walisema CUF ni CCM B wakati wao wanashirikiana na CCM B na kumsimamisha mgombea Urais kutoka CCM.
 
Naona sindano ya DSM na Mbeya imekuingia ipasavyo lakini bado dose yenye hajaanza mwaka huu lazima utajifungua kabla ya wakati.
 
Katika vyama vya kijuha chadema wanaongoza sijui wanawaza kwa kutumia akili za upande gani katika kichwa.
 
Katika vyama vya kijuha chadema wanaongoza sijui wanawaza kwa kutumia akili za upande gani katika kichwa.

Mkuu, sidhani hawa hata hiyo akili ya kufikiri wanayo. Nadhani hawa wanajiendea tu ka gari lililofeli breki mteremkoni
 
Nyie ndo wakulaumiwa.baada mlete sred za magufuri mnaongelea cdm na eddo.Pombe magufuri vijana wa buku saba lumumba wamekusaliti.
 
Najuta kusoma upuuzi kama huu.japo mimi ni team magufuli na mwana ccm ila umeandika pumba kabisa
Bora nihamie ukawa maana mbeya na dar na arusha pamesisimika tutakomaje ccm?
 
chadema /ukawa ndo tumani pekee la watanzania
 
Hata hii pia haitamsaidia Magufuli. Inakuwaje Lowassa ni fisadi lakini Kikwete na wenzie wameshindwa kumchukulia hatua?
Sina sababu ya kukujibu wewe kwa vile umeamua kujitoa ufahamu. Unajua kuwa Lowasa ni fisadi ila unaamua kumkumbatia. Wasalimie Arusha
 
Ukawa hawana vijana wa kujenga hoja nzuri ili kupinga hoja za vijana wa CCM, matusi na lugha chafu haitasaidia kuwaeleza vijana wa CCM hazma za Ukawa kwa taifa letu Tajiri lakini bado huonel
 
Ukawa hawana vijana wa kujenga hoja nzuri ili kupinga hoja za vijana wa CCM, matusi na lugha chafu haitasaidia kuwaeleza vijana wa CCM hazma za Ukawa kwa taifa letu Tajiri lakini bado huonel
Umenena mkuu. Hawa vijana wa CHADEMA na UKAWA wanachojua ni matusi tu. nje ya hapo hawana uwezo kabisa. Nimewawekea mada hii kwa point nilidhani watajikita kujenga hoja kwa kila point. Kumbe wapi! Bora nirudi kwenye mikeka ili niwachanganye kabisa
 
Hata hii pia haitamsaidia Magufuli. Inakuwaje Lowassa ni fisadi lakini Kikwete na wenzie wameshindwa kumchukulia hatua?

Kwa hadhi aliyokuwa nayo bwana mamvi katika Jamii na serikali kwa wakati ule kumfukuza katika nafasi ya uwaziri mkuu ilikuwa ni hatua tosha kabisa.
 
Back
Top Bottom