Unafiki wa TCU

WW FIKRA ZAKO NI NDOGO SANA HASA KWA KARNE HII
Kumbe mtu mwenyewe wa July, 2016. Sihangaiki na wewe. Ni mgeni mno katika ujenzi wa hoja ndio maana unajificha katika kichaka cha"blanket statements." Ungetoka kidogo ukaenda katika nchi za wenzako ukaona mfumo wa elimu ulivyo. Ni mawazo hafifu kudhani kila mtu lazima afike chuo kikuu. Hii sio UPE. Halafu ni aibu kulilia upanuzi wa magoli ili hata kama hauna sifa uingie. Pambana upenye katika viwango vilivyowekwa na sio kusubiri huruma. Kwenye elimu hakuna huruma ebo!
 
Mkuu, mimi sijaelewa jambo katika utetezi wako. Hivi graduates kuwa watu wanadhalia ni sheria au mapungufu yaliyopo katika elimu inayotolewa katika vyuo vikuu husika? Unaonaje huyu graduate akiwa well equiped kwa nadharia na vitendo? Umesema watu wa diploma ndio hasa watendaji, hivi mwalimu mwenye degree na mwenye diploma wewe unapendelea nani amfundishe mwanao. Mbona kwa nchi kama Finland mbona hata mwalimu wa shule ya msingi ana masters? Tatitzo kuna baadhi ya watu bado wanaishi katika fikra za enzi ya chuo kikuu kimoja cha UDSM.
 
Napenda ujenzi wako wa hoja kwa kuwa una lengo la kujenga. Hoja yangu ya msingi ni kutoruhusu upanuzi wa magoli ilimradi tu wengi wasome chuo kikuu. Kama wote wakikidhi vigezo vilivyowekwa, ni ruksa tu kwenda chuo kikuu. Ila tusilalamike ili viwango vishushwe. Hiyo inakuwa sio elimu bora bali bora elimu. Na huyo "graduate" anayengia kwa kutegemea upanuzi wa magoli (kwa maana ya viwango hafifu), competency yake inakuwa chini kuliko hata huyo wa certificate au diploma. Karibu tuendelee kuelimishana
 
Je, ni kweli mtu aliye na E mbili ambapo E umeiita ni principal pass amefeli? Huoni kama umeongeza sharti ili umwache hata aliyefaulu?
 
Je, ni kweli mtu aliye na E mbili ambapo E umeiita ni principal pass amefeli? Huoni kama umeongeza sharti ili umwache hata aliyefaulu?
Huyo anakuwa hajafeli. Lakini ushindani ukiwa mkubwa anaachwa nje ya system. Kumbuka hapo zamani kama hauna point 5 kutoka katika masomo matatu, usingeweza kuingia chuo kikuu. Hivi vigezo huweza kubadilishwa kutokana na mahitaji ya wakati husika. Labda tu cha kulaumu, ni muda gani unafanya mabadiliko ili wadau wajiandae kukabiliana nayo ipasavyo.
 
Bora ulivyomfafanulia kuna wengine wana elimu lakin hawajitambui
 

Ha ha ha a duh
 
Povu kwel limekutoka.
Lakn mm n mmoja wapo wa dhao la shule izo za kata unazosema hazina mazingira na vitu rafk katka elimu.
Lakn katka shule yetu wote tuna vigezo vya kwenda chuo.
Acha kujisijisifia na kujiona geneus subiri uende huko ukakione cha moto
 
Asante kwa kubali kama umaskini si kigezo cha kufeli wala kufaulu kwa mtu....
Sasa hapo kwenye afya na furaha ndugu yangu, Je ni kweli wanaofeli hawana afya nzuri pia wanahudhuni?
Kumbuka hoja yangu mwanzo haikupinga mackin hafaulu ila mackin wapo aina mbili una wazazi wote hamna pesa lakini una furaha ila huna wazazi unalelewa na tabu unapata pia kumbuka ckusema kuwa ni wote wenaokosa furaha na na uzima ndo wanafeli BAADHI ya watu nahic mgumu wakauelewa hatuongelei kufeli na kufaulu tunaongelea kufaulu vizuri
 
Hiyo point 5 ilikuwa ni wakati wa uhaba wa vyuo vikuu. Ni kama ufaulu wa kwenda sekondari ulivyokuwa wakati wa shule za sekondari chache. Mimi nakumbuka wakati huo mtihani wa darasa la saba ulikuwa na mitihani mitatu. Lugha, Hisabati na Sayansi. Kila mtihani ulikuwa na jumla ya alama 50, bila kuwa na jumla ya alama 140 ulikuwa hugusi sekondari. Baada ya kuongezeka shule za sekondari, alama ziliendelea kushuka nasikia siku hizi mtoto akiwa na alama 70 za masomo 5 anaenda sekondari. Sasa kwa nini huko nako tusiseme turudi kulekule? Unajua ndugu yangu, ifike mahali elimu itolewe kwa mtazamo wa kuwaelimisha watu ili elimu hiyo iwasaidie katika maisha yao binafsi na si kutoa elimu kwa ajili ya kuwaza kuwatumia tu.
 


Hujielewi hata!
mara umaskini....gia angani ukabadili ikawa ni afya na hudhuni sasa imekua wazazi...
Binti, atakaye cha uvunguni sharti ni moja tu! ainame.
Soma ufikie viwango vilivyowekwa vinginevyo....
 
Karibu Jf!
Huyo mgeni anatakiwa awe anapita hapa JF tu bila ku "comment" chochote ili ajifunze jinsi hoja zinavyojengwa. Vinginevyo ataishia kutoa "sweeping statements" muda wote ambazo hazimpi sifa ya kuwa "Great thinker".
 
Huyo mgeni anatakiwa awe anapita hapa JF tu bila ku "comment" chochote ili ajifunze jinsi hoja zinavyojengwa. Vinginevyo ataishia kutoa "sweeping statements" muda wote ambazo hazimpi sifa ya kuwa "Great thinker".


Na bila shaka huyu ni mmoja wa wahanga wa mabadiliko katika sekta ya elimu.
 
Hebu fikiria mkuu, mimi nimfanya biashara nataka nipate elimu ya business administration au marketing, huoni kama nitafika mahali nitakabwa na vigezo vilivyowekwa vya juu kwa ajili ya kuwapata wale wanaotafutwa kuwa waajiriwa wazuri wenye nadharia nyingi kichwani?
 
Geukia mjini namba inasomeka vizuri bila chenga.
 
Hahaha! Umenifurahisha ndugu. Kumbuka kuna fursa ya kurudia mtihani ili kupata vigezo vinavyohitajika. Si rahisi kuweka vigezo ambavyo vitakidhi matakwa ya kila mmoja wetu. Bado pia kuna fursa ya kuanzia diploma, na baadaye ukatumia ufaulu wa diploma kujiunga chuo kikuu. Kwa kujielimisha zaidi, soma falsafa ya Plato na Socrates kuhusu elimu.
Samahani nime copy na ku paste tu, hivyo mpangilio si mzuri.

"Sound education system: selectively prepares the younger generation for differentiated future roles according to their abilities. enhances the general thinking abilities of people in a society. promotes individual happiness for the development of a just government. In a society, people’s intellectual abilities are naturally divided into three groups; golden boys, silver boys and iron boys.;

So, the education system should sift them for providing education that matches their abilities. Golden boys (the bright ones): their education should fit positions of philosopher kings, rulers, policy makers and planners. Responsible in making the society to be calm and prosperous. Silver boys, the less bright group but physically fit: would be trained to be defenders of people as well as supervisors for ensuring that the policies made are followed.

The iron boys, the dull ones were to be prepared for intellectually less demanding jobs; farmers, carpentry or iron smiths. For Plato, education is a practice of discovering and confronting the challenges of everyday living in the areas and positions in which each one would be best trained".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…