Mchango wao ni wa kawaida sana ambao hata mtanzania mwingine akipewa nafasi anaweza akafanya tena zaidi ya wao walivofanya, so stop expanding this mada
Mbona unakuwa na roho ya kichawi! Hao Watanzania unao wasema walikuwepo mbona Reli ya kati hatukuona ikibeba abiria mpaka Mwanza? Mbona sijawahi ona meli za kimataifa zikikamatwa kwa wizi wa samaki? Sijawahi sikia Mtanzania mwingine akimwambia Rais wa nchi kwaujasiri mkubwa bila unafiki awemkali kwa watendaji wazembe mbele ya hadhara!
Sitaki malumbano lakini nachokuambia hao akina Magufuli na Mwakyembe wanafanya kazi za kawaida ambazo hata waTanzania wengine wakipewa nafasi wanaweza kufanya tena zaidi ya hao ndugu.
-Magufuli ameuza nyumba za umma kipindi cha Mkapa mpaka sasa mawaziri wengine ni juzi wametoka kwenye mahoteli ya kifahari tuliyowapangishia kwa kuwa walikosa nyumba za kuishi za hadhi ya uwaziri
-Mwakyembe mnafiki mpaka leo hajawaeleza waTanzania kwa nini report ya Richmond hakuisoma yote eti kwa kuhofia serikali kutikisika sasa inatikisika sasa
Kwangu wote wanafiki tu, treni hiyo ya reli ya kati wewe unaisema ipi? Si tena kabla ya Mwakyembe tulikuwa tunaenda bara kutokea Dar mara tatu kwa wiki sasa hivi ni mara mbili tu.TAZARA imemshinda zile kumbi za kusubiria wasafiri na zile za kupumzikia kusubiri kusafiri sasa zimegeuka kuwa kumbi za harusi, sendoff na kitchen party sasa nimsifie kwa lipi?NARUDIA TENA WAPO WATANZANIA WANAOWEZA KUFANYA VIZURI TENA ZAIDI YA HAWA MWAKYEMBE NA MAGUFULI
Haya kwasababu Magufuli alitoka nyumbani kwake nakutangaza kuuza zile nyumba bila ridhaa ya wakuu wake basi anastahili lawama zako yeye binfsi,vilevile Mwakyembe kama aliikuta Reli inasafari tatu kwa wiki na sasa ina safari mbili basi naye anastahili lawama zako! Na kwakuwa wewe na hao wenzako mnauwezo wa kuleta mabadiliko ndani ya muda mfupi,nitamshauri mkuu wangu wa nchi akupe nafasi,tunawahitaji sana watu kama wewe!