Unafiki wa serikali huu hapa hebu oneni

NGOWILE

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
454
258
Wadau ni muda mrefu sana serikali yetu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imekuwa ikihubiri juu ya kufanya siasa katika vyuoni vyetu vikuu hasa vile vya serikali.Na hata raisi wa nchi alipohudhuria mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Dodoma katika hotuba yake aliwaasa wanafunzi kutojihusisha na siasa mpaka watakapomaliza elimu yao.Aliwaasa wanafunzi kuwa wanawasiasa wakiwahitaji wawambie wanasoma kwanza.Katika hali ya kawaida unapomkanya au kumuasa mtu juu ya kitu chochote unatakiwa wewe kuwa mfano kwake juu ya jambo husika (ROLE MODEL) Katika hali ya kushangaza chama tawala CCM na serikali yake vimeshindwa kuyasimamia kile wanachosema wanafunzi wasijihusishe na siasa hasa wale wa vyuo vikuu.Hili linajidhihirisha wazi pale CCM ilipoanzisha mkoa maalum wa vyuo vikuu ambapo kila chuo kitakuwa tawi kichama,hii ni siasa ya waziwazi tofauti na wanavyohubiri kwenye majukwaa ya kisiasa.Chakushangaza ni kuwepo kwa bango kubwa lililoandikwa CCM katika eneo la chuo kikuu cha DODOMA (UDOM) ambacho ni cha serikali yaani watanzania wote bila kujali imani na itikadi zao za kisiasa.Iweje hili bango liwepo kama sio unafiki? Picha ya bango hilo nimeatach na thred hii wadau muone na mtoe maoni yenu.Najua wapo watakosema chuo kile kimetokana na CCM kwani nkimeanzishwa kwenye Jengo lake (UKUMBI WA CHIMWAGA) Ukweli jengo lile sio la CCM bali ni la watanzani wote wakiwemo wakulima na wafugaji wa nchi hii kwani walichangia ujenzi wake enzi za chama kimoja kwa hiyo ni haki yao na wala siyo fadhila ya CCM.Kama kweli serikali hii ipo serious ninaomba bango hili liondolewe mara moja ndani ya chuo hiki cha serikali.
 

Attachments

  • DSC00922.JPG
    DSC00922.JPG
    1.3 MB · Views: 155
Toa ufafanuzi kidogo plz cause picha hiyo tu bado haioneshi unafiki wa serikali kama thread yako inavyoeleza.
 
Mwanzisha mada kwa maelezo yako umesema kuwa chuo kipo ulipokuwa ukumbi wa CCM CHIMWAGA. Kwa kuangalia tu inaonekana kuwa chuo kimelikuta bango. Kichotakiwa kufanyika kwa sasa ni Serikali kuweka wazi kuwa chuo ni mali ya CCM au ya Serikali?. Kama wakijibu ya CCM watuwekee Fund ya CCM iliyotumika kujengea na inayotumika kuendeshea chuo.

Kama wakisema cha serikali basi wanatakiwa kuondoa alama za vyama vya siasa. Kwai vyama vingine navyo vianaweza kuja na mabango yao na kuyaweka pembeni ya bango la CCM, itakuwa vurugu.

Ninachokiona hapo ni watu kupuuzia kusafisha site ama kwa makusudi kwa kuona hakuna haja, ama kwa kutokujua.
 
Naomba watokee wahuni fulani usiku walibomoe bango hilo tuone iwapo serikali ya CCM itafanya nini! Wanaudhi sana hawa nyiyiemu kwa unafiki usio mipaka.
 
Oyaa, unafki ni hali ya kusema usilotenda, kama hukumuelewa mleta mada nahisi kichwa yako iko na hitilafu kidogo, 'magamba feaver' perhaps
Toa ufafanuzi kidogo plz cause picha hiyo tu bado haioneshi unafiki wa serikali kama thread yako inavyoeleza.
 
Back
Top Bottom