Maneno yako kweli kabisa lakini hadi hapo tutakapo pata ushahidi toka upande wa madai ndipo tunaweza kumsafisha.. Binafsi simuamini yeyote ndani ya CCM na sababu kubwa ni kwamba hawaendi sherehe bila ndizi mfukoni hivyo sii rahisi kumsafisha mwenye ndizi ya kwamba hakwenda kwenye sherehe kutafuta kula..Duh Mkuu Nape, inatosha maana hamna majibu now you can see my point mara kwa mara Kwa Mwenyekiti wa CCM taifa kwamba awe anawalazimisha Viongozi wa CCM kuja kujibu hoja hapa JF itapunguza sana majungu. SALUTE!
nadhani kilio cha wananchi haswa sio Wabunge tu, wala sio swala la ongezeko bali kama nakumbuka ni swala zima la sitting allowance winazoliopwa watumishi wote wakiwa wanatumikia majukumu walokabidhiwa..Mathlan Nnauye anapokwenda ktk vikao vya CCM hulipwa posho hizi? mfanyakazi mtumishi wa serikali anapokuwa katika vikao vya wizara yake hulipwa posho hizi juu ya mshahara anaopokea?...kama kweli Nnauye hajawahi kupinga posho hizi isipokuwa pale walipoongeza inamweka palepale sawa na wengine wanaunga mkono posho hii.
Malipo ya sitting allowance ndio sio halali na wananchi tunapinga malipo haya..Hapa ndio swala lilipoanzia na limekuja pata uzito zaidi pale posho hii lipoongezeka kutoka 70,000 kwenda 200,000, na Zitto na wajumbe wa Chadema walipinga hata utoaji wa posho ya Tsh 70,000 toka kikao kilichopita kabla, na kama sikosei Zitto hazipokei hata hizo Tsh 70,000.. Je yeye Nnauye hapokei sitting allowance.. Je amewahi kuzikana ama kutoa rai zifutwe! na kama anaafiki na anapokea kwa nini atazame ongezeko la posho hizo kuwa haramu lakini sii kilio cha wananchi kinachoanza na utoaji wa posho hizo iwe kwake ama kwa mtumishi yeyote ambaye anawagharimu walipa kodi kwa kazi anayolipwa mshahara. hayo mengine kusema kweli sina wala shauku nayo zaidi maana sii kilio changu.