Unafiki wa Nape, CCM kuhusu ongezeko la posho kwa wabunge huu hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unafiki wa Nape, CCM kuhusu ongezeko la posho kwa wabunge huu hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzito Kabwela, Dec 16, 2011.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Mara kadhaa tumeshamshauri Nape aachane na ujinga ujinga wake anaouendeleza lakini amekuwa hasikii.
  Na wenye akili tulimshauri awe makini sana anapoamua kutumika lakini bado amekuwa mbishi.
  Wengi tunaofuatilia siasa za Tanganyika na Zanzibar tunaelewa kuwa Nape hana Muda mrefu ataingia kwenye recycle bin ya siasa.
  Juzi juzi alikurupuka kupinga ongezeko la posho kwa wabunge ambapo kina Mtatiro walimwambia aache unafiki. Zitto akamtetea. Zitto ana sababu zake za kumtetea Nape na si lengo la sredi hii kumjadili Zitto.
  Ona sasa ya Nape:
  1. Analipwa Mshahara wa Zaidi ya Shilingi Milioni 2 kwa mwezi
  2. Amepewa gari Land Cruiser VX la gharama za sh Mil 180
  3. Amepewa wasaidizi wanaolipwa na Chama
  4. Anapewa MAFUTA, NYUMBA na MATIBABU BURE (Hapa nina maana kwa gharama za Chama)
  4. Anaposafiri, hutia kibindoni posho na fedha ya kujikimu zaidi ya shilingi 135,000/=
  5. Mara nyingi (karibia zote) anaposafiri mikoani, pamoja na kupewa kitita cha safari toka Makao makuu ya chama, bado anako kwenda hulipia malazi na chakula.  Kwa upande mwingine, makatibu wa ngazi za kata hulipwa posho ya Shilingi 10,000/- kwa mwezi na Makatibu wa Matawi hulipwa Shilingi 5,000/- kwa Mwezi.

  Iko wapi dhamira ya Nape ya kupinga ongezeko la posho kwa wabunge? Nani asiyejua kuwa posho wanazolipana kwenye sekretarieti ya CCM ni kodi za wavuja jasho wa Tanzania?
  Source: Uchunguzi wangu binafsi ambao ni wakweli. Nape aje hapa akanushe.
  Nawasilisha.
   
 2. A

  AzimiolaArusha Senior Member

  #2
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45

  Mimi nafikiri tusinyoosheane vidole, tutafute ufumbuzi wa matatizo yetu kwa mustakabali wa nchi yetu wenyewe, Kambi ya upinzani bungeni ilishauri mfumo wote wa posho uangaliwe upya na ubadilishwe!!! Issue sio posho za Nape au Wabunge, tuangalie maeneo yote kuanzia idara, halmashauri, wizara na organs nyingine za serikali watumishi wa uma wanavyofuja na kupoteza hela na kujilimbikizia mali kwa posho ambazo ni hela za uuma, yaani kodo zetu, Waalimu wamesahaulika, polisi ndo usiseme, manesi ndo kabisaa, makatibu kata na tarafa ndo usiseme, wanafunzi vyuoni wanagoma kila leo mikopo hakuna na wengine wamekosa mikopo, madaktari ndo kabisaa wanakimbilia kwenye hospitali binafsi na nje ya nchi kwa sababu ya ujira kidogo!!!!! SERIKALI YA CCM SIKIENI KILIO CHA WATANZANIA, TUNAHITAJI MFUMO WOTE WA KODI UANGALIWE UPYA KWA MASLAHI YA TAIFA SI CHADEMA WALA CCM WALA NCCR N.K!!!!!!!!!!! MAWAZIRI SIKIENI, WABUNGE SIKIENI, VIONGOZI SIKIENI LA SIVYO TUTAWAHUKUMU KWA MATENDO YENU 2015!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Habari kama hiyo nimeona mbele ya gazeti la Mtanzania leo, sijui kama ndio hiyo lakini zinafanana sanaaaa.
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Hivi bado Nape anaujasiri wa kuongea mbele ya waandishi wa habari??
   
 5. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kujibalaguza tu lakini hana jipya.
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Habari hii ilitoka katika gazeti la RAI la jana..
   
 7. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sijaona ubaya wa Nape hapa zaidi ya wewe kutaka kupanda kwa Posho iwe agenda ya Magwanda yani watanzania wengine wasiongee! Nape yupo huru kutoa maoni yake kama Mtanzania na ana haki ya kutoa tamko kupitia Chama chake na CCM wana haki ya kupinga ongezeko hilo la posho,kinacho umiza hapa nyie Magwanda mlitaka kuhodhi hii agenda ya kupanda posho iwe ya Kwenu! Yanapofika masuala ya kitaifa kila mtu ana haki kusimama kidete! Ndio maana nyie Magwanda huwa hamumuelewi Zitto kabisa! Zitto ni Mpenzi wa Tanzania kuliko nyie waumini wa vyama! Ma-vyama yenu yatapita Tanzania itabaki na Watanzania!
   
 8. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hata mimi nashangaa ingekuwa enzi zile virusi vyake vingeshajazana hapa kumtetea.
   
 9. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  hapo ndugu unachoshangaa ni nini? mshahara wa milion 2 mbona ni wa kawaida? hata hizo stahili nyingine ni za kawaida sana. kwani vyama vingine vinalipaje makatibu wenezi wa kitaifa? mfano CDM au NCCR Mageuzi? nilisikia Dr Slaa kama katibu alikuwa analipwa salary Tshs 10 million sijui kama ni sahihi.

  sasa unafananisha kiongozi wa kitaifa na viongozi wa kata/matawi? hiyo haipo duniani kote
   
 10. j

  jigoku JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Mlengo wa kati ifike mahala tuache unafiki na kuongea kwa kufurahisha genge,na hasa unapochangia hoja nzito kama hii,hivi kweli kwa akili yako kuna mtu ndani ya CCM anaweza kusimama na kapinga posho?hivi agenda hii ya posho ni ya leo?haukumbuki hata waziri mkuu Pinda aliwahi kuitetea?hata spika aliwahi kuitetea,wabunge wote wa CCM walikuwa na wanaendelea kuitetea,leo watu wanapotoa hoja ya kusema Nape ni mnafiki mtu anapobisha anasikitisha watu,Nape atatoka wapi na ananguvu gani ndani ya CCM kukataa posho?kauli ya Nape ilikuja baada ya wakubwa kuona upepo umevuma vibaya,mapokeo ya watanzania juu ya suala la posho yalikuwa negatively,ili kulinda turufu ya kisiasa ndio maana CCM wakaituma spika yaoya kusemea itangaze msimamo wa chama cha CCM juu ya suala la posho.tusidanganyane hapa huo ulikuwa ni unafiki tu,utawezaji kumtenga Pinda na msimamo wa CCM,utawezaje kumtenga madam speake Makinda na msimamo wa CCM kuhusu posho?tusiwe waseamji kwa ajili ya kufurahisha genge,aje kwanza waziri mkuu atuambie alipokuwa anaitetea hoja ya posho ilikuwaje na leo anapoipinga amegundua kitu gani,na hao wabunge wa ccm watuambie msimamo wa chama ndo uko hivyo je pale awali walipokuwa wanashabikia ilikuwaje?na hata sasa ilikuwa ni kulinnda turufu ya kisiasa tu lakini ni hatua gani kama chama tawala watafanya?
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Hapa sisi tunahitaji habari, kama wewe uliiona mbona hukuileta hapa? unadhani kila mtu ana access ya kuyasoma hayo magazeti?
   
 12. r

  raffiki Senior Member

  #12
  Dec 16, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ndio bongo kila idara....Ushauri kwa Dr. Slaa na wenzake,wamyamaze kama Dr.Salim na Magufuli,hakuna haja ya kupinga kitu tena shv...watulie kbs nichi iende kama itakaavyooenda na sie wananchi tuuumie ipasavyoo hata kila kitu kiuzwe wapeane posho sawa tu...ikifika 2014 wananchi ndio wataelewa kwann wanaelezwa nchi wezi ndio wanajifanya wanawatetea
   
 13. H

  Honey K JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mzito Kabwela,
  Nikushukuru kwa kunukuu huu uzushi na uzandiki na kuuleta hapa! nilipouona Rai sikushangaa wala kustuka ila niliupuuza sawa na kukanyaga sisimizi, you dont feel, lakini hapa nitajibu kwani sasa nahisi unataka kukuzwa, kule sikuhizi Rai hata Kibamba halifiki so haikunipa tabu.
  ..Kwanza mwenye ushahidi wa mshahara wangu alete hapa ili tuanze na huo!
  .. Sijawahi kulipwa posho zilizotajwa na mwenye ushahidi nazo azilete hapa!
  .. Gari ninalo nadhani bei ni zaidi ya iliyotajwa, dhambi yake nini???!!
  .. Sina wasaidizi wanaolipwa na CCM, kwa taarifa ninajitosheleza naweza mpaka kuchapa kazi zangu mwenyewe huyo msaidizi wa nini? Sitetemeki mikono kama mafisadi sihitaji...msaidizi
  .. Nimelazwa juzijuzi hospital Kairuki mission nendeni kaangalieni kalipa nani?!! sijazoea kulipiwa/kufadhiliwa kama alivyodekezwa Mzito Kabwela na wanaoishi mjini kwa fitini na pesa za kifisadi kama wasimamizi wale..
  HUU NI UZUSHI ULIOKUBUHU!! ONENI AIBU KUZUSHA MAMBO KAMA MBWEHA WANAOTAFUTA MADUME


   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Haya Wadau Nape ndio huyo amejibu hoja moja baada ya nyingine, kwahiyo mwenye ushaidi aulete hapa, otherwise hizi taarifa hizi si sahihi, ingawa najuwa CCM wana style yao ya kulipana mapesa bila kuwepo kwenye mfumo rasmi.
  N:b: Mimi binafsi sina muda wakusoma gazeti la Rai maana ni gazeti la wanafki na wazushi wakubwa, pili siwezi kununuwa gazeti la Rai ili niendelee kumtajirisha huyu mwizi Rostam, pesa alizotuibia zinamtosha.
   
 15. H

  Honey K JF-Expert Member

  #15
  Dec 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jigoku,
  NADHANI UMEKURUPUKA KURUSHA MANENO MAKALI BILA KUFIKIRI KWANZA! HIV UNAMJUA ALIYEANZISHA HOJA YA WABUNGE KUONGEZA POSHO?UNAPOSEMA MSIMAMO WA WAZIRI MKUU UNAUJUA KWA POSHO HIZI AU UNACHANGANYA MAMBO???? HUU NI ULIMBUKENI KUJARIBU KUDANGANYA WATU KUWA HIZI POSHO NI ZA WABUNGE WA CCM!!! NITAJIE MBUNGE MMOJA WA UPINZANI AMBAYE AMEACHA KUCHUKUA POSHO KWA KISINGINZIO HICHI KUWA HATUTAKI HIZI POSHO!!!
  SITETEI POSHO LAKINI, NASISITIZA SWALA LA POSHO SI LAMKICHAMA, NI KILIO CHA WATANZANIA WOTE BILA KUJALI ITIKADI ZAO...
  QUOTE=jigoku;2985985]Mlengo wa kati ifike mahala tuache unafiki na kuongea kwa kufurahisha genge,na hasa unapochangia hoja nzito kama hii,hivi kweli kwa akili yako kuna mtu ndani ya CCM anaweza kusimama na kapinga posho?hivi agenda hii ya posho ni ya leo?haukumbuki hata waziri mkuu Pinda aliwahi kuitetea?hata spika aliwahi kuitetea,wabunge wote wa CCM walikuwa na wanaendelea kuitetea,leo watu wanapotoa hoja ya kusema Nape ni mnafiki mtu anapobisha anasikitisha watu,Nape atatoka wapi na ananguvu gani ndani ya CCM kukataa posho?kauli ya Nape ilikuja baada ya wakubwa kuona upepo umevuma vibaya,mapokeo ya watanzania juu ya suala la posho yalikuwa negatively,ili kulinda turufu ya kisiasa ndio maana CCM wakaituma spika yaoya kusemea itangaze msimamo wa chama cha CCM juu ya suala la posho.tusidanganyane hapa huo ulikuwa ni unafiki tu,utawezaji kumtenga Pinda na msimamo wa CCM,utawezaje kumtenga madam speake Makinda na msimamo wa CCM kuhusu posho?tusiwe waseamji kwa ajili ya kufurahisha genge,aje kwanza waziri mkuu atuambie alipokuwa anaitetea hoja ya posho ilikuwaje na leo anapoipinga amegundua kitu gani,na hao wabunge wa ccm watuambie msimamo wa chama ndo uko hivyo je pale awali walipokuwa wanashabikia ilikuwaje?na hata sasa ilikuwa ni kulinnda turufu ya kisiasa tu lakini ni hatua gani kama chama tawala watafanya?[/QUOTE]
   
 16. K

  Keil JF-Expert Member

  #16
  Dec 17, 2011
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nnauye Jr.

  Naomba tujulishe basi aliyeanzisha hoja ya wabunge kudai posho. Maana hapa JF kila kitu huwa kiko wazi, hatuogopi mtu. Hata Mwenyekiti wako akichemsha huwa anapewa LIVE hapa hapa.

  Kama chama kinamfahamu, kwanini hakimwiti na kumuonya kwamba hoja yake inazidi kukichafua chama kama jinsi ilivyo hoja ya ufisadi ambayo inaendelea kukimaliza chama.
   
 17. H

  Honey K JF-Expert Member

  #17
  Dec 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kelli,
  HOJA YEYOTE YA NAMNA HII HUANZIA KWENYE KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE, AMBAPO WENYEVITI WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE NA KIONGOZI WA KAMBI RASIMI YA UPINZANI BUNGENI NI MJUMBE. HOJA KABLA HAMJAKUBALIANA KUPELEKA KWA WABUNGE INAJADILIWA HAPA THEN NDIO INAENDELEA MBELE....NINI ROLE YA WABUNGE WA UPINZANI HAPA?? ( ndo maana nikasisitiza HII SI HOJA YA CHAMA HII NI HOJA YA BUNGE).... lakini ILIPOPELEKWA KWA WABUNGE WOTE NA SPIKA WABUNGE WANNE WA UPINZANI NA KADHAA WA CCM WALIUNGA MKONO KWA KUSEMA NA WENGINE WALIOBAKI KWA KUPIGA MAKOFI..... Sasa hoja hii ya Chama au ya wabunge bila kujali Itikadi zao?? TOKA HOJA HII IMEANZA KUNA WABUNGE WA CCM NA WA UPINZANI WANAOPINGA HOJA HII WENGINE HADHARANI NA WENGINE KIMYAKIMYA, NDO MAANA NIKAMUUNGA MKONO ZITTO HII SI HOJA YA CHAMA FLANI NI HOJA YA WABUNGE NA PUBLIC IKO AGAINST HILI...
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Binafsi nimekuelewa vyema ulivyojipambanuwa kwenye hili tupo pamoja, lakini wasi wasi wangu ni mwenyekiti wako yule ni kama popo si ndege na wala si mnyima usije kusikia siku ameshasaini hayo mapendekezo ya Bunge kwa gia ile ile kwamba nisiposaini wabunge wa chama changu hawatanielewa!!
  To be honest mimi simwamini kabisa Mwenyekiti wako, za mbayuwayu changanya na zako, atakustaajabisha siku utakayosikia JK ameshasaini hizi posho.
   
 19. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #19
  Dec 17, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Duh Mkuu Nape, inatosha maana hamna majibu now you can see my point mara kwa mara Kwa Mwenyekiti wa CCM taifa kwamba awe anawalazimisha Viongozi wa CCM kuja kujibu hoja hapa JF itapunguza sana majungu. SALUTE!
   
 20. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #20
  Dec 17, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Duuuuhhh !!!! Nilikuwa sijui kumbe huwa unapiga majungu JF. Wacha wananchi wadadavue mambo. Napita tu.
   
Loading...