Habarini wadau,
Kwa takribani wiki mbili sasa nipo nyumbani kwetu (kwa baba na mama) baada ya kuchukua likizo ya mwezi mmoja kazini, hapa nyumbani ninaye dada zangu wawili na dada wa kazi.
Moja kwa moja twende kwenye mada husika, siku mbili baada ya mimi kuwasili hapa nyumbani akaja ndugu yetu mmoja wa kiume ambaye rika lake ni sawa na mimi huyu ndugu siyo mara yake ya kwanza kuja hapa nyumbani, kwa mujibu wa maelezo ya mama lakini kwa upande wangu tumeonana awamu hii kwa maana hiyo huwa anawatembelea mara kwa mara mimi nikiwa zangu mkoa mwingine kikazi.
Kinachonishangaza kuhusu huyu ndugu anavoishi hapa home, yaani yeye ni mtu ambaye hajishugulishi na chochote,yaani yeye ni kama boss hapa home.Muda wa msosi tunajumuika vizuri tu, lakini chombo atakacho piga msosi atakiacha hapohapo,hawa ndugu zangu ama mama huchukua jukumu la kumuoshea chombo chake.Hii hali imekuwa kero sasa kwa upande wangu maana binafsi nikirudi hapa home,nashiriki kila kitu muhimu cha hapa ikiwemo kuosha chombo changu ambacho nimepigia msosi.
Kiukweli imekuwa ni kero sana maana utakuta siku katoka,akirudi anakuta sisi tumeshakula na hivo msosi ulio bakia ni kwa ajili yake tu lakini ataishia kula na kuacha kila kitu hapo hapo mpaka glass aliyo nywea maji dada zangu watakuja kuvitoa na kwenda kuviosha.
Huyu ndugu analala na mimi,hivo mida ya asubuhi siku zingine huwa nawahi kuamka kwa ajili ya michakato yangu. Nikirudi ile sa nne nakuta kaamka,kaoga kakaa sebuleni lakini kitanda hata hakijatandikwa.Binafsi sina maneno mengi,ninachokifanya ni kutandika tu basi na kuendelea na mishe.
Nb; kinacho niuma zaidi mother anafahamu kila kitu lakini haongei lolote yaani hata kikombe cha kunywea chai anakiacha hapohapo, hata kwenda tu kukisuuza ni kazi wadau, maana karo la kuoshea vyombo liko ndani humuhumu.Ingekuwa ni mara yake ya kwanza kuja hapa home nisingemlaumu kwa kufanya hivo, lakini wanadai ni mara nyingi tu huwa anakuja na anafanya hivyohivyo.
Vipi wadau, tatizo huwa ni nini? Je, nimchane live ama nimpotezee? Maana jamaa anaondoka kesho.