Unafiki wa mama yangu na dada zangu

Unafiki wa mama yangu na dada zangu

Hv ww yan huon aibu kumwita mama yako mnafiki?kweli unakili ndan ya jamvi zima hl kabisa?baada ya kukuzaa,kukulea,ukusomesha,kukufunza kuish na watu hayo ndo malipo anayo stahili??haya ww mtakatifu,usie mnafiki,mbona hujamwambia?sikia huyo mama anakufundisha uvumilivu kwa hali zotee.afu kamuombe msamaha.looooh
 
Habarini wadau,kwa takribani wiki mbili sasa nipo nyumbani kwetu(kwa baba na mama) baada ya kuchukua likizo ya mwezi mmoja kazini.hapa nyumbani ninaye dada zangu wawili na dada wa kazi.

Moja kwa moja twende kwenye mada husika,siku mbili baada ya mimi kuwasili hapa home akaja ndugu yetu mmoja hiv wa kiume ambaye rika lake ni sawa na mimi tu.huyu ndugu siyo mara yake ya kwanza kuja hapa home kwa mujibu wa maelezo ya mama lakini kwa upande wangu tumeonana awamu hii.kwa maana hiyo huwa anawatembelea mara kwa mara mm nkiwa zangu mkoa mwingine kikazi.

Kinacho nishangaza kuhusu huyu ndugu anavoishi hapa home,yaani yeye ni mtu ambaye hajishugulishi na chochote,yaani yeye ni kama boss hapa home.Muda wa msos tunajumuika vizur tu,lakini chombo atakacho piga msos atakiacha hapohapo,hawa ndugu zangu ama mama huchukua jukumu la kumuoshea chombo chake.Hii hali imekuwa kero sasa kwa upande wangu,maana binafsi nikirud hapa home,nashiriki kila kitu muhimu cha hapa ikiwemo kuosha chombo changu ambacho nimepigia msosi.kiukweli imekuwa ni kero saana maana utakuta siku katoka,akirudi anakuta sisi tumeshakula na hivo msos ulio bakia ni kwa ajili yake tu..lakini ataishia kula na kuacha kila kitu hapo hapo mpaka glass aliyo nywea maji..dada zangu watakuja kuvitoa na kwenda kuviosha.

Huyu ndugu analala na mimi,hvo mida ya asubuh siku zingine huwa nawah kuamka kwa ajili ya michakato yangu.nikirud ile sa nne nakuta kaamka,kaoga kakaa sebuleni lakn kitanda hata hakijatandikwa.Binafsi sina maneno mengi,ninacho kifanya ni kutandika tu basi na kuendelea na mishe.



Nb..kinacho niuma zaidi mother anafahamu kila kitu lakin haongei lolote.yaani hata kikombe cha kunywea chai anakiacha hapohapo,hata kwenda tu kukisuuza ni kazi wadau.maana karo la kuoshea vyombo liko ndani humuhumu.Ingekuwa ni mara yake ya kwanza kuja hapa home nisingemlaumu kwa kufanya hivo,lkn wanadai ni mara nyingi tu huwa anakuja na anafanya hivohvo.


vp wadau,tatzo huwa ni nini? je,nimchane live ama nimpotezee? maana jamaa anaondoka kesho
Huyo mtu ni nani kwenu..??
 
Kama mna binti wa kazi na dada wawili why bother, especially kwa sbb ni mtoto wa kiume anayekujaga kuwacheki marakwamara its OK!

Mbaya n kuwa akiwa hana msaada hapo lazima umiweke wazi, kama anakuja hata na kachungwa kidogo na shuguli ndogondogo maza anaweza mtuma na akazifanya bila taabu! Achana nae otherwise muweke sawa
 
Kwahiyo katika familia yenu kila mtu akishakula anaenda kuosha chombo chake? Kweli kila familia na vituko vyake asee...mwe!
 
Wewe ndy mnafiki mkubwa,Pumbavu zako. Unamuita Mama mnafiki??? Unalaana wewe,mshenzi sana wewe,umekosa adabu kwa mzazi wako. Mpuuzi sana wewe. Km mama yako wamuita hivyo,Mama wa mwenzio utamuita nani?
 
Usimuite mama yako mnafiki... alafu huyo ndiyo alivyokuzwa... siyo rahisi kumbadilisha...
 
Hahaaa huyo jamaa atakuwa mpelelezi.

Yaani hafanyi chochote kabisaa!!!
 
Mwenye matatizo ni wewe unayemuita mama ako mnafiki kwa kosa LA mtu mwingne nn hasa unaogopa kumwambia huyo ndugu yako..
 
Huyo nduguyo ana element halisi za kiume siyo wewe ulizoea kuchekacheka na kushinda na dada zako na Mama.
Kwa sisi wanaumme wa kanda ya ziwa hatuna hizo time kuosha vyombo wakati dada zangu wapo.
Nimecheka sana Hahahahaha
 
Yaani wewe unakuja hapa kulalamikia kuhusu kuosha vyombo na kutandika kitanda,halafu unamwita mama na dada wanafiki❔➖shame on you ❗❗
 
Mimi binafsi sipatani na mishe za kulala kwa ndugu mana nina character kama za huyo jamaa unaemuongelea ninapo enda likizo home kwa maza angu huwa sigusi chochote si nguo zangu wala kitanda kutandikwa ,Hakuna anaeniona uvivu kama pana ndugu yupo na ananiona niko wrong anipishe nikae na mama.
Kama ni kwenu kweli app kwanza utaoshaje vyombo mkuu dada, maza wapo? pili unakosaje maamuzi hapo kwenu mimi nirudiipo kwetu nasikilizwa kuliko baba
 
Inaonekana wewe pia ni kiburi au una katabia kabovu, kitendo cha kumuita mama ni Mnafiki nina mashaka na malezi yako, japo mama yako anaonekana kuwalewa vizuri dada zako, (kama ikiwa huyo mgeni hamna hata mmoja mwenye mahusiano nao), Wanaopaswa kulalamika ni hao wanaomuoshea kwanini ukerekwe wewe? unakitu kinakusumbua juu ya huyo, mgeni, japo ni kweli anachofanya si sahihi, ulipaswa kuongea nae kama mtoto wa kiume ungemsikiza majibu yake ndo ungepata jibu sahihi kuwa ni tabia yake tu au ni shemeji yako n.k..kumbuka mtu kama ni tabia yake ni ngumu kugundua kama anachofanya si sahih yeye anaona poa tu, kwahiyo wewe unapaswa uongee nae sio kumchana kama ulivyosema.
 
Kuuna watu kama nyie duniani hamtakiwi kuishi n.a. watu kapange msituni unaonekana una roho mbaya ajabu.
 
Kweli kila familia ina taratibu zake..Yaani kila mtu baada ya kula anaenda kuosha chombo chake mwenyewe..Na hadi mgeni akija akishakula na yeye kwenye sink kuosha vyombo..
Hii familia ni kioja. Mimi naona familia nzima imejaa unafiki. Kijana anawaita mama na dada zake wanafiki. Sababu za kuwaita hivyo pengine ni kwa sababu hawamwambii kasoro zake huyo asiyeosha vyombo. Lakini wakati huo huo huyu kijana nae badala ya kumwambia kasoro zake huyo asiyeosha vyombo na kutandika kitanda au kushauriana na ndugu zake juu ya nini cha kufanya kuhusu huyo bwana, nae kwa unafiki anakuja kulalamika JF kiunafiki. Kiufupi familia inampiga majungu mgeni pembeni bila yeye kujua badala ya kuangalia ni yapi kati ya matendo yake yanyamaziwe na ni yapi wamweleze ili abadilike kitabia ukizingatia kuwa watu tunakulia katika mazingira tofauti tofauti na wakati mwingine unaweza kufanya jambo ukidhani uko sahihi kumbe sivyo. Hii ni ajabu sana. Mwisho hili la kila mtu kuosha chombo chake baada ya chakula ni mapinduzi makubwa katika jamii yetu ya kiafrika.
 
Mtoa mada una roho mbaya sana usipoacha utakufa umekundula
 
Back
Top Bottom