Unafiki wa clouds fm na serengeti breweries

domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,545
1,719
Serengeti Breweries ni mdhamini wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Clouds fm ni mmoja kati ya waandaji eti wa kitu kinachitwa tamasha la uzalendo. Leo Serengeti Breweries eti ndio wadhamini wa timu za ulaya kama vile Barcelona, AC Milan, Man U, Real madrid, Arsenal na nyinginezo. Wanawachukua vijana wa kitanzania wanawakusanya wakiwa wamevaa jezi za timu hizo na kuwashawishi wawe walevi. Hivi hawa wadhamini wa Taifa Stars wamefikiri mpaka mwisho ndo wakaona bora wafanye hilo wanalolifanya? Hivi na hawa wazalendo Clouds Fm wameona kuzitangaza na kutengeneza timu za man u, barca na nyinginzo eti tena kuwa na uongozi wale hapa Nchini ndio uzalendo? Nisaidieni jamani labda mimi siujui uzalendo maana yake nini. Nafananisha hii na kauli ya Mheshimiwa Ngeleja anayesema madini yameifanyia mengi nchi hii wakati hayachangii hata asilimia tano katika pato la taifa, mimi naona mambo yanafanywa kinyume na vile yanavyostahila na pia kinyume na vile inavyonadiwa
 
Back
Top Bottom