Full Time | Senegal 1-1 Tanzania | TotalEnergies AFCON U-17 | Senegal Mabigwa baada ya mikwaju ya penati 4-2

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,690
Reaction score
15,639
Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17), maarufu kama Serengeti Boys, leo inashuka dimbani kuivaa Senegal U-17 katika mchezo wa mwisho wa michuano ya TotalEnergies AFCON U-17.

Mchezo huo utaanza saa 4:00 usiku katika Uwanja wa Stade Moulay Hassan, Rabat, Morocco, ambapo Tanzania U-17 (Serengeti Boys) itakuwa ikimenyana na Senegal U-17 katika fainali ya michuano ya CAF U-17 Africa Cup of Nations Morocco 2026.

Senegal wanakuja wakiwa na uzoefu mkubwa, nguvu, na kasi, lakini soka la kisasa limeonyesha kuwa dakika 90 ndizo zinazoamua na hakuna timu ndogo tena Afrika.

Swali linarudi kwako shabiki wa soka:
  • Je, mbinu na uzalendo wa Taifa Stars utatosha kuwazuia Simba wa Teranga?
  • Au uzoefu na ukongwe wa Senegal utatawala mchezo wa leo?
Kete yako unaitupa wapi leo? Weka utabiri wako hapa chini!

Game ipo on fire dakika 5 ya mchezo

Dakika 7 Serengeti Boys wanafunga goliiiiii zuri sana

Dakika 11, Serengeti boys wanapeleka moto

Dakika 22, Bado vijana wa Tanzania wanaongoza

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimekamilika kibabe kabisa Serengeti Boys wakitoka na uongozi wa goli moja kwa sifuri

Dakika 45 za kipindi cha pili zimeanza
 
Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17), maarufu kama Serengeti Boys, leo inashuka dimbani kuivaa Senegal U-17 katika mchezo wa mwisho wa michuano ya TotalEnergies AFCON U-17.

Mchezo huo utaanza saa 4:00 usiku katika Uwanja wa Stade Moulay Hassan, Rabat, Morocco, ambapo Tanzania U-17 (Serengeti Boys) itakuwa ikimenyana na Senegal U-17 katika fainali ya michuano ya CAF U-17 Africa Cup of Nations Morocco 2026.

Hapo kwanza tuna advantage ya mashabiki, kwa kuwa wamoroko walizinguana na wasenegali kwenye fainali ya AFCON (ya wakubwa) hivyo hapo kuna ile kauli ya kuwa "adui wa adui yangu ni rafiki yangu", na vijana itabidi wajitoe kwa asilimia zote kwani hawana cha kupoteza ila hapo ndipo wanajitengenezea masoko kwenye career zao za mpira.
Tunawaombea kila la heri, hata kucheza tu fainali ni hatua moja kubwa tuliyoipiga kama nchi.
Tuwekeze kwenye mchezo na si ushirikina.
 
Wakishinda tu, it'll be the main topic na wakushukuliwa hapo atakuwa Mama, which again itakuwa the main for a while. Naskia madogo Tyr wameshapewa viwanja. Kwanini wasingeshinda kwanza?
Ikiwa kucheza fainali wamepata viwanja basi wakishinda watajengewa na nyumba kabisa na huenda wakapata na hata na usafiri ila umri wa kundesha utakuwa bado.
 
Hapo kwanza tuna advantage ya mashabiki, kwa kuwa wamoroko walizinguana na wasenegali kwenye fainali ya AFCON (ya wakubwa) hivyo hapo kuna ile kauli ya kuwa "adui wa adui yangu ni rafiki yangu", na vijana itabidi wajitoe kwa asilimia zote kwani hawana cha kupoteza ila hapo ndipo wanajitengenezea masoko kwenye career zao za mpira.
Tunawaombea kila la heri, hata kucheza tu fainali ni hatua moja kubwa tuliyoipiga kama nchi.
Tuwekeze kwenye mchezo na si ushirikina.
Sahau hilo,
Hiyo michezo toka awali ni kama imesusiwa, haina washabiki.
Braza ee, leo uwanja ukifikisha washabiki elfu 3, njoo kesho unitukane humu.
 
Ni siku nyingine kubwa na ya kihistoria kwa soka la Afrika ambapo miamba miwili inakutana uwanjani. Serengeti Boys ya Tanzania inashuka dimbani kumenyana na mmoja wa majitu ya soka barani Afrika, Simba wa Teranga (Senegal). Hawa ni mabingwa wa zamani na timu yenye mseto wa nyota wanaocheza soka la kulipwa Ulaya na kote duniani.

Kwa upande wa Tanzania, timu inaingia uwanjani ikiwa na ari ya "Uzalendo" na kiu ya kuthibitisha kuwa soka la Afrika Mashariki limekua na halitishiwi nyau tena na majina makubwa kuanzia kwenye timu za Taifa mpaka vilabu.

Hii ii mechi inayohitaji mbinu za hali ya juu, nidhamu ya ukabaji, na utulivu wa kufanya maamuzi ya haraka langoni.

Back
Top Bottom