Unafiki unaliangamiza Taifa

Unafiki unaliangamiza Taifa

Juzi juzi rais Trunp wa Marekani aligubikwa na lawama kila kona ya nchi ya Marekani, kisa alishindwa kuonyesha heshima alipopiga simu kumpa pole mke wa mwanajeshi wa marekani aliefia afrika kwenye kikosi cha kurinda amani cha UN.

Tunajifunza nini sisi watanzania kutokana na mkasa huo:-
  1. Wamarekani hawamkopeshi Rais wala hawamuonei haya kumwambia ukweli anapomkosea hata raia mmoja tu wa marekani.
  2. Vyombo vyote vya habari duniani vililipoti taarifa hii vikiwemo vya serikari kama VOA bila kujificha nyuma ya unafki ili kulinda hadhi na heshima ya taifa la Marekani.
  3. Dhamana ya urais wa USA haiko juu ya haki za raia wa marekani.
  4. Heshima, haki na utu wa raia wa marekani hauwezi kuingiliwa na taasisi au mtu yeyote yule.
  5. Hakuna mtu ama taasisi iliyomtetea rais katika hili ilimbidi ajitetee binafsi kama Trump.
  6. Wanajua kutenganisha baina ya taasisi ya urais na mtu binafsi kama Trump tofauti na Tanzania ambapo hakuna tofauti kati ya taasisi ya urais na Magufuli kama mtu binafsi.
Kitendo cha rais kuteua mtu ambae yuko chini ya uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa,hii inaweza kutafsiliwa kama:-

  • kitendo cha kuizuia taasisi ya kupambana rushwa kuendelea na uchunguzi dhidi ya mtuhumiwa.
  • Kumwepusha mtuhumiwa na adhabu inayoweza kumkabili endapo tuhuma dhidi yake zitathibitishwa.
  • Kujaribu kufifisha uzito wa makosa ya mtuhumiwa.
  • Kukili kwa mtuhumiwa kujihusisha na alichokiita kununua wapinza na kuwa bado ataendelea kufanya hivyo ni kujaribu kufifisha kosa la rushwa lakini pia ni ujumbe wa dharau dhidi ya raia wa Tanzania.
  • Dalili ya wazi kutangazwa kwa tabaka la raia wasioguswa na sheria.
Hili ni tatizo kubwa na la wazi linalotukabili kama taifa kwa sasa,cha kushangaza ni kuwa hakuna taasisi ya kiraia,dini,watu mashuhuri,Maaskofu,Mashehe ukiachilia mbali wananchi wa kawaida mitandaoni waliojitokeza walau kukemea kitendo hiki.
Hakika watanzania hatutaiepuka dhambi ya unafki uliotukuka.
Tumeiacha hadhi na heshima ya nchi kutwezwa huku tukijificha nyuma ya kichaka cha unafiki wa kuiheshimu taasisi ya rais,vyama vya siasa na chuki binafsi,na sio ajabu tukaona watu wanatetea tendo hili.
Maaskofu na mashehe ni sehemu ya ushetani wa utawala huu
 
Ukitoa kundi la raia, LHRC, vikundi kadhaa na vyama kadhaa vya upinzani, makundi mengine yote yaliyobaki ni matawi ya sisiyemu
 
Kwa bahati, hatua yake hii imenifanya niendelee kumdharau zaidi linapokuja lile la the so called "anapambana na ufisadi".

Na kwa bahati mzuri, mwanzoni kabisa mwa utawala wake nilishasema wazi kwamba Magu hapambani na ufisadi manake, endapo kweli angekuwa anapambana na ufisadi basi angeanza na viongozi kadhaa wa kisiasa wanaotoka CCM ambao wapo kwenye nyadhifa mbalimbali!!!

Niliamini hayo baada ya kuona anapambana zaidi na watendaji na maofisa wengine wadogo serikalini huku akiogopa kugusa yeyote at ministerial level kwenda juu!!!

Kila mmoja anafahamu kwamba CCM ndio tanuru la kuivisha mafisadi wa nchi hii! Lakini tangu achukue hatamu za uongozi wa CCM, wana-CCM walionja joto lake ni wale tu wenye tuhuma za usaliti kwa chama na sio ufisadi!!!
 
Back
Top Bottom