Unafiki dhidi ya Hayati Magufuli na Rais Samia

brton

Senior Member
May 7, 2019
174
151
Wasaalam wanabodi, Mimi Ni mdau wa maendeleo, linapokuja suala la maendeleo huwa nafurahi na kumpongeza hadharani kiongozi mleta maendeleo bila kuangalia katoka chama tawala au upinzani

Naomba niende mojakwamoja kwenye mada

Kuna tabia ya ajabu ipo hapa nchini huwa inanikera Sana na naweza kusema kuwa watanzania wengi Ni wanafiki na vigeugeu kwenye maneno yao wenyewe

Hayati magufuli alipambwa kwa mapambio mengi na kuonekana Ni Rais Bora kuwahi kutokea Tanzania na kuwa eti nchi yetu inahitaji Sana rais wa Sina yake ili tuwe na maendeleo

Magufuli alipofariki wengi walilia na kugaragara kuonesha wamempoteza kiongozi muhimu km nchi, wengi walishindwa kuficha hisia zao kwa kuigiza push-ups km alivofanya magu kipindi Cha kampeni kuonesha ushujaa wake

Leo tunapozungumza Mambo yamebadilika mno, wengi wamekuwa wanakosoa Kila alichofanya magufuli na mapambio na sifa km zilezile zimehamia kwa samia

Binafsi nakubali mama anaupiga mwingi maana anaendelea kujipambanua kuwa mwanademokrasia na mpenda amani ndomana anafanya maridhiano na upinzani

Swali: magufuli alikuwa mmbaya kiasi Cha kusemwa vibaya Leo hii au Kuna watu ndani ya Ccm kazi yao kubwa Ni kumpamba kiongozi aliyeko madarakani kwa manufaa binafsi?
Screenshot_20220516-012010.jpg
 
Kwani waliomlilia Magufuli na kuuona uongozi wake kuwa ulikuwa na ubora na upekee wa aina yake ni lazima wawe wale wale wanaomponda sasa?

Mimi uelewa wangu ni huu, kuwa kuna watu waliomchukia Magufuli ki kweli kweli na hao ndio wanaomponda sasa. Wengi wao ni hawa aliowatumbua kwa ujinga ujinga wao na upuuzi upuuzi wao. Papo hapo kuna watu waliompenda Magufuli, wengi wao hawakuwa na maslahi binafsi na utawala wa Magufuli sema tu walipenda tu kuona jinsi nchi inavyoanza kutengeneza misingi ya mafanikio na kunyooka.

As for mama Samia, naye atajitengenezea watakaompenda na watakaomchukia. Mwisho wa siku cha maana hakitakuwa nani ni nani kati ya Magufuli na Samia bali kitakuwa jinsi kiongozi binafsi atakavyoweka kumbukumbu isiyofutika kupitia uongozi uliotukuka kwa nchi yake. Magufuli alifanya kazi yake na hatasahaulika, ni juu ya Samia nae kujiwekea alama yake.
 
Back
Top Bottom