Unafanyeje kurejesha mapenzi katika ndoa yako?

Azial

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
440
500
Habari wana JF!

Mwenzenu moyo wangu umekufa ganzi kabisa kwasasa, nifanyeje kurejesha hisia kwa wangu wa maisha? Mume wangu alini-cheat nikamsamehe ame-cheat tena na sasa moyo wangu umechukia kiasi cha kutokuwa na hisia naye tena
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,822
2,000
Fanya mambo yaleyale na vitu vilevile kama ulivyofanya mwanzoni wakati unambembeleza mwenzio kule kwenye viunga vya kanisani sijui, mpaka akakukubalia na kukupenda kuwa pamoja nawe kwa huzuni na furaha, hadi mauti itakapowatenganisha :)
 

kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
3,055
2,000
Habari wana jf! Mwenzenu moyo wangu umekufa ganzi kabisa kwasasa, nifanyeje kurejesha hisia kwa wangu wa maisha??
Hayo ni matokeo. Mara nyingi wanawake huwa mnaanza maudhi na kunyima unyumba. Mwanaume anavumilia hadi anachoka. Akichoka anatafuta mchepuko, ukija kusituka mwanaume hana hamu na K yako. Hapo ndipo unaanza kulaumu kwanini anachepuka.

Jinsi ya kufanya, jitathimini ulipoteleza, jaribu kujirekebisha. Anza upya naye atabadilika bila ya ukali maana dawa ya moto ni maji si moto. Kila la kheri
 

zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,040
2,000
Nimeongezea mkuu soma tena unishauri please!
Nafikiri jipe muda tu uone hali itakuwaje. Itategemeana na jinsi huyo mwenzako anavyo- au atakavyo-jibehave. Kama ataonyesha kujutia kitendo hicho cha kukucheat basi msamehe tu. Ieleweke wanaume sisi hata pale tunapocheat si kwamba hatuwapendi wake zetu. Huwa mara nyingi ni utoto tukikua huwa tunaacha!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom