Unafanyaje kuepusha watoto wasiguse mtungi wa gesi?

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Tuna familia na vilevile tuna watoto l, hivi kwa familia mnafanyaje watoto wasicheze au kugusa mitungi ya gesi?

Maana wakijisahau wakifungua na kuacha isambae hatari nyumba kuwaka moto na watu kwisha.

Watoto mnawadhibitije wasicheze au kugusa mitungi ya ges?

Tupeane maujuzi maana ni changamoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama hao watoto ni wakike, waambie waione gesi kama mwanaume mana watatiwa mimba.

kama hao watoto ni wakiume, waambie waione gesi kama wanawake mana wataambukizwa pangusa.
 
Uwe na chumba maalumu kinachofungwa / kutokuwa na mtungi karibu watoto hawasikiii...

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Namna nyingine ni kuwatafutia video za youtube za kuonesha madhara ya matumizi mabovu ya gas.
Unawaelimisha na kuwapiga mkwara mzito kuhusu madhara ya gas.
Maranyingi watoto umri huo huwa wanaelewa na kuwa walimu kwa wenzao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watoto ni watundu kweli

Kama ni wadogo sana under 4yrs unaweza weka ugali wa motooo kwenye mtungi then unamshikisha hatarudia tena

Kama ni over 4yrs ni tayari ana uelewa unakua unamuonesha videos za maafa ya gas huku ukiwa unamuelezea jinsi gas ilivyokua hatari usichoke kila wakati unamkumbusha na unapomkuta red handed anachezea mtungi basi unamtia hapo hapo fimbo hata mbili tu zinatosha

Kama nyumba haina wasimamizi wa karibu sana kwa watoto mnaweza jengea mtungi nje ya nyumba na ndio inavyotakiwa
Au ndani ukaihifidha mahala salama ambapo hawaezi kufika mf kabatini yale ya kujengewa ambayo yenye funguo
 
Mkuu ujengee nje waite mafundi chuma wanakujengea nje ya nyumba then pipe zinaingia ndani hii husaidia pia ata kwa usalama wa nyumba pia endapo gas inalipuka

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna watoto ni watundu kweli

Kama ni wadogo sana under 4yrs unaweza weka ugali wa motooo kwenye mtungi then unamshikisha hatarudia tena

Kama ni over 4yrs ni tayari ana uelewa unakua unamuonesha videos za maafa ya gas huku ukiwa unamuelezea jinsi gas ilivyokua hatari usichoke kila wakati unamkumbusha na unapomkuta red handed anachezea mtungi basi unamtia hapo hapo fimbo hata mbili tu zinatosha

Kama nyumba haina wasimamizi wa karibu sana kwa watoto mnaweza jengea mtungi nje ya nyumba na ndio inavyotakiwa
Au ndani ukaihifidha mahala salama ambapo hawaezi kufika mf kabatini yale ya kujengewa ambayo yenye funguo
Asante sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom