Drone Camera
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 14,121
- 14,032
Kwa kipindi sasa nimekuwa nafuatilia computer nzuri kwa upande wa programming na video editing. Sio mtaalamu wa video editing ila napenda kufanya tu for fun. Kwa kuwa nimebobea kidogo kwenye Windows na Linux toka chuo, nikaona best option kwa sasa ni kutafuta computer yenye gpu nzuri au ninunue gpu kisha ni assemble computer yangu mwenyewe. Kuna kitu kikanijia kichwani kwamba nijaribu Mac. Kipindi cha nyuma nilipokuwa nafuatilia tutorials, instructors wengi(80%) walikuwa wanatumia tunda. So nikazama mfukoni kdg nikaenda kwa wauzaji maarufu wa Mac. Nilihitaji hizi model mpya zenye chip ya Apple Silicon, at least M2 ya 2023.
Apple bei zao zimesimama bhana. Macbook Air M2 bei ni 2.5M kama ukibahatisha hadi 3M(Hapo bei inategemea pia Memory na Storage). Hapo bado hujaenda kwenye models za pro. Nakushauri kama wewe ni wale watu wa "Hiyo hela si unapata kiwanja kikubwa mlandege" usikanyage maduka yao.
Kwa kuwa nilikuwa na modern monitor na keyboard maghetoni, pia kazi nyingi nafanyia nyumbani, nikafanya maamuzi ya kuchukua Mac Mini(ni kama desktop version ya Mac). Hii ni cheap ukienda duka zuri ila utajitegemea monitor, keyboard na mouse. Nikatoa kama 1.5M na vichenchi hiv, nikapewa Mac Mini M2 base model Ram 8GB na storage 256GB.
Okay poa, nipo hapa namalizia huu uzi wa JF saa nane kuelekea na nusu usiku. Nimefungua tabs za kufa mtu Safari. Chrome nayo inaomba nizidi kuiongezea tabs. Nina docker, Xcode, Android Studio, pamoja na emulator zote za iOS na Android na naweza tumia zote kwa pamoja. Nina DaVinci Resolve, advanced video editor software inayotumika hadi Hollywood na inakuja na additional apps kibao. Inawaka chap hadi clients wanashangaa. Imebaki na storage ya gb 30 ila bado inapiga job kama haina kitu. Kesho nachukua external ya 1TB. Pia nimejipanga kuhamia M4 muda si mrefu.
Kubalance equation vizuri, nilikuwa na Dell pia yenye ram 8GB na storage ya 500 ila HDD. Kuinstall tu Android Studio na emulator yake feni inapuliza kama upo gesti za dar. Hii ya sasa japo ina feni, ila sijawahi sikia upepo wake wala joto lake.
Apple wapewe maua yao.
Picha kwa hisani ya mtandao.