Unabii juu ya anga la Tanzania

Unabii juu ya anga la Tanzania

Hakika, dawa ni kutubu...lakini kutubu kuwe kwa Taifa zima siyo kwa mtu mmoja tu.....kama ni kutubu basi wote tutubu maana wote tumekosea, mpaka viongozi wa dini wamekosea pia.
Kabisa maana kuna watu wanawanyoshea vidole wengine kuwa ni wenye dhambi ikiwa hata wao pia wana dhambi na hawajatubu.
 
Amen Tanzania kwanza kila Mzalendo aiwazie mema Tanzania ni Nchi yetu hatuna nyingine zaidi ya Tanzania ,Hata kama humpendi fulani jilinde usifikie mbali Mwisho ukajaa hasira kifuani hatimaye ukawazia na Visasi hata kama iweje jizuie Kisasi cha Mungu pekee
Shukrani ujumbe uwafikie wa Tz wote tuondoe tofauti zetu.
 
Mheshimiwa Msukuma (mbunge) aliwahi kusema bungeni siku si nyingi zilizopita kwamba zaidi ya asilimia 95 za wabunge wanaenda kwa waganga wa kienyeji. Hakuna mbunge yeyote aliyempinga. Mawaziri wanatokana na wabunge.

Watanzania wote tunatakiwa sasa tuombe kwa bidii zote ili viongozi wanaotumainia ushirikina waache, wamtegemee Mungu. Viongozi wakishamtegemea Mungu, ndipo tukimwomba Mungu atupe amani atatusikia.
 
Nchi iliyojaa Wazinzi na Waasherati inaomba baraka za MUNGU, nchi iliyojaa Uchawi na Ushirikina eti inaomba baraka za MUNGU. Nchi hii imejaa kila aina ya maovu na uchafu. Hivi hao manabii wenu hawawaambii kuwa kwenye Biblia imeandikwa kuwa MUNGU hawasikilizi wenye dhambi?

Msijidanganye wala msidanganywe, baraka za MUNGU haziji kwa kusali na kuomba. Baraka za MUNGU huwa zinawafuata wale watu wanaozishika Amri za MUNGU na kuzitenda kwa vitendo. Baraka za MUNGU haziendi kwa watenda dhambi hata siku moja.

Nabii wa kweli wa MUNGU atawakemea watu waache dhambi na maovu, tena atawafundisha watu kuwa, ili wapokee baraka kutoka kwa MUNGU, basi ni lazima wazishike Amri za MUNGU na kulitii NENO la MUNGU na kuacha kabisa dhambi.

Mimi nasema hivi, Nabii yeyote yule anayesema eti MUNGU kamwambia kuwa atashusha neema zake kwa nchi hii, huyo nabii ni mwongo kabisa. Kutokana na dhambi na uchafu uliotamalaki katika taifa hili, kamwe taifa hili halistahili kupokea baraka za MUNGU, bali "kibiriti" cha moto na laana. Nchi hii imekuwa zaidi ya Sodoma na Gomora, zaidi ya Babiloni; kila siku tunasikia watoto wadogo wanalawitiwa; wanawake wanatoa mimba hovyo, maelfu ya watoto wanazaliwa na kutelekezwa na baba zao, mauaji ya watu wasiokuwa na hatia, wizi na ujambazi, ubinafsi na chuki, ushoga na usagaji na umalaya vimetamalaki kila sehemu hapa Tanzania, ndoa zinavunjika kila kukicha, matusi kwenye mitandao n.k.

Ndugu yangu Abayesu bayesu huyo Nabii wako na huo utabiri wake ni wa uwongo kabisa. Kwa maovu yanayofanyika ndani ya Taifa hili kamwe haliwezi kubarikiwa na MUNGU, hiyo haiwezekani.
Hayo uyaitayo maovu na uyaonayo yakitendeka nchini yanayazidi yale yatendekayo ktk mataifa mengine Mfano Israel na Marekani? Kunaongeza maarifa ktk kumjua Mungu na kinyume chake yaweza kuwa sahihi. Kuna kweli kuu juu ya Mungu, tuzitafute kweli na kuyaongeza maarifa ili tuwe huru.
 
Hujui maana ya NEEMA (grace) ndugu!
Eti mimi nahisi wewe ndiye usiyejua maana ya "neema" , imeandikwa kwamba Mungu alimbariki na kumneemesha Ayubu kwa kumpa watoto na utajiri mwingi zaidi, ila haikuandikwa kwamba wale watoto walitokea kwa njia ya "mnunurisho" toka mbinguni, bali alitafuta mke, akapanda mbegu, akazaa na kulea watoto.
 
Kwa andiko hili, nini maana ya NEEMA?
Pia yapo maandiko mengi (refer the books of Romans and Galatians) yanayozungumzia habari ya NEEMA halafu useme kama yanatoa maana tofauti na andiko la kwenye kitabu cha Ayubu ulicho refer.
 
Umenena kweli tupu mkuu, baraka haiji ila kwa matendo mema tu hata ufunge mwaka mzima km bado ni mnywaji Pombe,Mzinifu,mwezi,mwongo nk hakuna baraka ila Utapata mafanikio ya kishetani km ya kupata utajiri kupitia kwa waganga yasiyo na amani
Nchi iliyojaa Wazinzi na Waasherati inaomba baraka za MUNGU, nchi iliyojaa Uchawi na Ushirikina eti inaomba baraka za MUNGU. Nchi hii imejaa kila aina ya maovu na uchafu. Hivi hao manabii wenu hawawaambii kuwa kwenye Biblia imeandikwa kuwa MUNGU hawasikilizi wenye dhambi?

Msijidanganye wala msidanganywe, baraka za MUNGU haziji kwa kusali na kuomba. Baraka za MUNGU huwa zinawafuata wale watu wanaozishika Amri za MUNGU na kuzitenda kwa vitendo. Baraka za MUNGU haziendi kwa watenda dhambi hata siku moja.

Nabii wa kweli wa MUNGU atawakemea watu waache dhambi na maovu, tena atawafundisha watu kuwa, ili wapokee baraka kutoka kwa MUNGU, basi ni lazima wazishike Amri za MUNGU na kulitii NENO la MUNGU na kuacha kabisa dhambi.

Mimi nasema hivi, Nabii yeyote yule anayesema eti MUNGU kamwambia kuwa atashusha neema zake kwa nchi hii, huyo nabii ni mwongo kabisa. Kutokana na dhambi na uchafu uliotamalaki katika taifa hili, kamwe taifa hili halistahili kupokea baraka za MUNGU, bali "kibiriti" cha moto na laana. Nchi hii imekuwa zaidi ya Sodoma na Gomora, zaidi ya Babiloni; kila siku tunasikia watoto wadogo wanalawitiwa; wanawake wanatoa mimba hovyo, maelfu ya watoto wanazaliwa na kutelekezwa na baba zao, mauaji ya watu wasiokuwa na hatia, wizi na ujambazi, ubinafsi na chuki, ushoga na usagaji na umalaya vimetamalaki kila sehemu hapa Tanzania, ndoa zinavunjika kila kukicha, matusi kwenye mitandao n.k.

Ndugu yangu Abayesu bayesu huyo Nabii wako na huo utabiri wake ni wa uwongo kabisa. Kwa maovu yanayofanyika ndani ya Taifa hili kamwe haliwezi kubarikiwa na MUNGU, hiyo haiwezekani.
 
Ntauleta tena Mungu akimwonyesha
Anaonyeshwa na shetani sio Mungu..
Na wewe unamtumikia shetani bila kujijua, nakushauri soma Biblia kwa kuitafakari wewe mwenyewe usimtegemee uyo kichaa anaekupa unabii wa UONGO akusomee Biblia.. Read it yourself to serve ur own SELF from sins first,then later you'll be able to serve others
 
Huyu bwana ataingiza watu wengi sana kwenye dhambi ya manunguniko, hasira na visasi. Time will tell.
 
Mimi unabii wenu wala siuzingatii, bila kunipa unabii wa lini malaika.jiwe linadondoka siwezi kuwaelewa!!
 
Anaonyeshwa na shetani sio Mungu..
Na wewe unamtumikia shetani bila kujijua, nakushauri soma Biblia kwa kuitafakari wewe mwenyewe usimtegemee uyo kichaa anaekupa unabii wa UONGO akusomee Biblia.. Read it yourself to serve ur own SELF from sins first,then later you'll be able to serve others
Mungu siku zote hujidhihirisha mwenyewe,Mungu huleta mambo kwa sababu nyingi saa nyingine watu wamemsahau wapate shida wamkumbuke Mungu ndiye anayejua hata kesho ya mtu
 
Umenena kweli tupu mkuu, baraka haiji ila kwa matendo mema tu hata ufunge mwaka mzima km bado ni mnywaji Pombe,Mzinifu,mwezi,mwongo nk hakuna baraka ila Utapata mafanikio ya kishetani km ya kupata utajiri kupitia kwa waganga yasiyo na amani
Wewe ndugu yangu Freddienda unayo NURU iwakayo ndani yako. Ni wale tu wenye nuru ndani yao ndiyo wanaoweza kuijua KWELI. Basi sasa itumie nuru hiyo kuwaangazia na wengine pia ili waijue KWELI, ili hiyo KWELI, iwaweke huru kweli kweli.

BABA MUNGU, akubariki sana ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom