Unaangalia taarifa ya habari kutoka kituo gani?

Unaangalia taarifa ya habari kutoka kituo gani?

Meja Jenerali Isamuhyo

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
3,537
Reaction score
10,517
Mimi kwasasa Azam two wameniteka, taarifa yao ya habari huwa imeshiba sana na huwa ni ya kina hasa, huku ikichagizwa na uwepo wa Mkongwe Charles Hillary akiwa kama msomaji.
Changamoto pekee ni kuwa lazma uwe na kisimbusi chao ili uweze kufaidi uhondo wa taarifa yao ya habari.

Je wewe mdau ni taarifa ya habari ya kituo gani huwa inakuvutia?
 
Huwa sina chanell maalum ila kama jana mi pia nilivutika na Azam two kwa sababu kama jana kulikuwa na ile habari inayohusu miili ya watu ambayo inayoopolewa kila kukicha baharini kule Coco beach waliielezea kwa urefu ambapo ilinifanya nijue kuwa Tanzania ya sasa ina watu makatili ambao hawajawahi kutokea.

Yaani miili 17 ndani ya wiki mbili ni hatari sana aisee.
 
mi huwa siangalii habari, naangalia vile vichwa vya habari pale chini halafu nakuja kuitafuta JF
 
Nilishaazimia kutotizama habari za TV isipokuwa kwa sababu maalum. Hii ilikuwa baada ya kuona napata tatizo la KUBISHANA na TV kila mara nikitizama habari.
 
ITV imeniteka sana..labda kutokana na historia..Ila kwa miaka ya hivi karibuni nimeona imekuwa ikipoteza watangazaji wake maarufu na haifanyi usajili wa garama.. ,,ITV imekuwa kama Arsenal inakuza vipaji na kuviuza but hawasajili wakongwe.. Asilimia kubwa ya Watangazaji maarufu wametoka pale.. Azam siwapendi kwa sababu ya ubinafsi wao but they are good also...Channel yao haipatiakani kwenye vingamuzi vingine..
 
Back
Top Bottom