moodykabwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2015
- 625
- 602
Alikaa golini mechi na Al Ahly klabu bingwa Afrika akishuhudia goli la jioni na lililobaki kama alama ya uchungu kwake , wanayanga na watanzania kwa ujumla . Goli lililoiondoa Yanga katika michuano hiyo .
Leo tena akiwa langoni dakika zile zile refa ana amuru ipigwe pennati langoni mwake .
Alivuta pumzi ndefu na kulitazama benchi la ufundi kisha wachezaji wenzake na kwa haraka fikra zake zikasafiri maelfu ya kilomita hadi nchini kwake ( kwetu) na kuziona nafsi karibu milioni 40 zikijenga tumaini la magharibi juu yake , . Taifa nzima likimtazame yeye aamue furaha yao au wahuzunike tena ...
Aliuma meno na na kujiweka sawa langoni .
.... Penati akaipangua ... Taifa likazizima kwa furaha ... mikono yake ikawa mali kuliko almasi za waangola... Kwa hasira na jiwe wakampiga.. Wakamuona adui na katili mkubwa kuliko nduli wao hayati Jonasi Savimbi aliyewatesa kwa miongo kadhaa... Oooh Dida...
Una neno gani kwake?! !