Dimba la Taifa: Yanga Africans yatakata kwa ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Kagera Sugar

Clark boots

JF-Expert Member
Jun 5, 2017
6,393
5,518
mechi.jpg


01': Mechi ya Yanga vs Kagera Sugar imeanza hivi punde

04': Haji Mwinyi anarusha mpira kuelekea lango la Kagera baada ya kutolewa, anauchukua Ajib, Ajib anapasia langoni mwa wapinzani, wanaokoa

05': Kagera sasa, anao Atupele Green, pasia pembeni mwa Uwanja, hatariii, Kagera wanakosa nafasi ya wazi

07': Rostand anaanzisha goli kiki, ni baada ya mpira kutoka nje

08: Buswiiiita, namna gani hapa, krosi yake inakwenda nje, ilikuwa ni pasi nzuri ya auta kutoka kwa Ajib

12': Matokeo ni 0-0 mpaka sasa

13': Hatari katika lango la Kagera hapa, Buswiita, anababatizana na mlinda mlango, anaudaka

14': Mpira umesimama baada ya kipa wa Kagera kuumia, Cannavaro naye anapasha nje

15': tayari mpira umeshaanza, kwake Kamusoko, anapiga shuti lakini linatoka nje

16': Offside, Kagare wanaotea, mpira unapigwa kuelekea kwao

18': Kibaya anapata kadi ya njano, ni ya kwanza kwenye mchezo wa leo

19': Faulo, kadi ya pili ya njano inaenda kwa mchezaji wa Kagera, ni baada ya kucheza faulo eneo la hatari, inapigwa langoni mwao

20': Ajib yuko na mpira, anapigaaa, inapiga nyavu za juu

21': Ngonyani naye anapata kadi ya njano baada ya kucheza mazambi, ni ya tatu sasa katika mchezo huu

21': Matokeo ni 0-0

22': Mpira umesimama, Maxime anatoa maelekezo kwa wachezaji wake

23': Fhaki anapiga hapa, hatari langoni mwa Yanga, namna gani mshambuliaji huyu anashindwa kutumia nafasi

25': Kavila anamchezea rafu Chirwa hapa, inakuwa faulo kwenda Kagera

25': Ally Nasoro sasa anaondoka nao kupandisha mashambulizi, anapiga pasi mkaa, anaokoa Yondani

26': Wanaanza Yanga eneo la nyuma, Kessy anampasia Buswita, kwake Kamusoko, Kamusoko anapiga kwake Pato lakini beki wa Kagera anautoa na mpira unakuwa wa kona

28': Mpira anao Kamusoko, anapasia nyuma kwake Yondani, Yanga wanajaribu kutafuta bao hapa

29': Emmanuel Martin, anacheza faulo, mpira unapigwa kuelekea Yanga

30': matokeo ni 0-0, mpaka sasa hakuna timu iliyofanya shambulizi la kutisha kwa mwenzake

31': Goli Kiki upande wa Yanga, unapigwa kuelekea Kagera

32': Kagera waanzisha goli kiki, tayari ushapigwa, faulo, unapigwa kuelekea Kagera

33': Mabadiliko Yanga wanafanya mapema, anatoka Pato na nafasi yake inachukuliwa na Maka

35'; Kagera wanapata kona ya kwanza baada ya Mwinyi Haji kuutoa mpira, inapigwaaa, inapigwa kichwa na mshambuliaji wa Kagera lakini kipa Rostand anadaka

37': Unarushwa sasa kuelekea lango la Kagera, anao Ajib sasa, kwake Martin, unapigwa kwake Buswita, anautuliza kwa njia ya kifua lakini beki wa Kagera anaokoa

39': Anao sasa Ajib, unapigwa langoni, kipa anajitutumua anaupiga na mkono unakuwa wa kurushwa kuelekea langoni kwake, kidogo iwe kona

41': Faulo, Ajib anapiga, anapiga ya chinichini lakini mabeki wanaokoa kwa kichwa

41': Mpira uko mbele sasa upande wa kulia mwa uwanja wanao Yanga, beki wa Kagera anauokoa hapa, unapigwa mbele lakini Maka anautoa nje

Mpira ni mapumziko sasa, Yanga 0-0 Kagera Sugar

45': Kipindi cha pili kimeanza, matokeo ni 0-0

46': Beki wa Kagera anachezewa faulo, mpira unapigwa kuelekea langoni mwa Yanga

47': Hatarii langoni mwa Yanga, Atupele Green anakosa kupiga shuti nje kidogo mwa eneo la hatari, ni faulo,

48': Inapigwaaa, inatoka nje sentimita kadhaa tu, bahati nyingine wanaikosa Kagera Sugar,

50': Yanga wanaanza nyuma taraatibu, beki wa Kagera anautoa nje

51': Penatiiii, Yanga wanapata tuta hapa

51': Ajib ndiyo anapiga tuta, anapigaaa, gooooooli, Yanga wanapata bao la kwanza, sasa ni 1-0

53': Kagera wanaanza upya kati, wanapasiana kuelekea langoni mwa Yanga, inapigwa moja juu, kipa Rostand anaruka kama nyani anaudaka

55': Kagera wamezidi kuamka licha ya kufungwa bao hilo moja, wanamiliki zaidi mpira eneo la kati

57': Ajib sasa na mpira, piga huku pembeni lakini Kagera wanaokoa, inapigwa mbele hukuu, offside

59': Namna gani Kagera wanakosa tena bao hapa, ni nafasi adhimu kabisa hii ndani ya eneo la hatari mwa Yanga, mpira unakwenda nje

61': Kagera wanaanza mashambulizi tena, wanapasiana eneo la nyuma

63': Faulo inapigwa kuelekea Kagera baada ya beki wake kucheza mazambi

64': Yanga wanao mpira hivi sasa, Ajib anajaribu kuzunguka lakini ananyang'anywa mpira, Kamusoko anauwahi

65': Mpira anao Fhaki sasa, pasia kati ya uwanja huku, unarejeshwa kwake Fakhi tena, Kagera bado wanaumiliki, pigwa huku langoni mwa Yanga, offside

68': Kagera wanashindwa kutumia vema nafasi ya kufunga baada ya kupasiana vizuri na kuingia eneo la hatari la Yanga

69': Kona wanapata Yanga, ni ya nne na tano katika mchezo wa leo, Ajib anapiga lakini inaokolewa

70': Chirwaa, anapiga krosi moja ya hewani lakini inatoka nje

71': Mpira umesimaa kidogo, mchezaji wa Kagera ameumia

72': Omary Daga anaingia kuchuka nafasi ya Atupele Green, matokeo bado ni 1-0

75': Yanga wanapata kona, inapigwa na Ajib, pigwa huku Chirwa anapiga kichwa lakini inaenda pembeni, Kagera wanaokoa

75': Emmanuel Martiiiin, anapigaaaa, kipa wa Kagera anakuwa mahiri anaokoa

76': Goooooooli, Martin anaifungia Yanga bao la pili kufuatia krosi nzuri ya Obrey Chirwa, Yanga wana mabao mawili sasa na Kagera 0

79': Yanga wameamka sasa, wanakwenda mbele na mpira, kona! Ajib yu tayari kupiga, anaanza fupi hukuuu, kona nyingine, ni ya 7 sasa, inapigwaaaa, Kagera wanaokoa

81': Kagera wanapata kona pia, inapigwaaa lakini inaokolewa

82': Kagera wanaumiliki mpira tena, wanajaribu kutafuta bao angalau la kufutia machozi

83': Hatari langoni mwa Kagera, kipa anadaka, anaanza taratibu na wenzake nyuma

85': Kagera wanapata kona hapa, inapigwa lakini inatolewa na kuwa kona ya pili, inapigwa tena hukuu, Rostand anadaka na kutulia vizuuri kabisa

87': Yanga wanao sasa, Buswita, kwake Kessy, anarudisha kwa kipa wake

88': Yusuph Mhilu anakwenda na mpira upande wa kulia wa uwanja, anapigaa, gooooooli, Kagera wanajifunga katika harakati za kuokoa, sasa ni 3-0

90': Zimeongezwa dakika tatu pekee mpira umalizike

Full Time, Mwamuzi anapuliza kipyenga kumaliza mpira, Yanga 3-0 Kagera Sugar.
 
Back
Top Bottom