Una kitu gani cha kuipa Dunia ikupe utakacho?

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,574
3,481
UNA KITU GANI CHA PEKEE?

Swali hili ni muhimu kujiuliza na kujijibu mwenyewe hata kama likikukera ikiwa tu unahitaji kuitambua thamani yako au kuiweka katika hadhi yake sawasawa na vigezo vyako.

Acha kuendelea kutamani jaribu sasa kujiuliza wewe una kipi cha kukufanya upate uyatakayo. Kwa nini wewe?..

Jiulize tu usiogope utapata majibu yake....ni kitu gani cha pekee ulicho nacho kama sadaka kwa yale uyatakayo?

Dunia ipo katika mfupo wa nipe nikupe. Jiulize wewe unaipa nini na ili ikupe nini? Na ni kwa nini ikupe wewe na siyo wengine?. Unachokihitaji kina thamani gani na je kile unachokitoa kina thamani gani. Usijidanganye kuendelea kutamani badala ya kujitafuta kwanza ili ujue cha kutoa.

Unaweza kukutana na kijana wa kiume anasema waziwazi kabisa kuwa anatamani sana kuwa na mke mzuri waaina na umbile fulani analoona yeye ni zuri au kuwa na familia nzuri lakini hajiulizi yeye ana kipi cha cha pekee kwa hayo anayo yahitaji. Hata mimi najiuliza hapa nina nini cha pekee kitakachokuwa kama chombo cha mbadilishano "medium of exchange".

Usipoteze muda mwingi kutamani, ila tumia muda wa kutosha kujitafuta kwanza. Jiangalie upo katika pembe ipi ya thamani itakayoweza kukusaidia kufikia matamanio yako.

Upekee wako ni sadaka unayoipa Dunia na kuiamisha izidi kuyasogeza karibu zaidi matunda ya matamanio yako. Upekee wako katika chochote kile ukifanyacho ni ulinzi wa thamani yako.

Halipo darasa la kujifunza kujitafuta, kujibaini na kuufanyia kazi upekee wako zaidi yako wewe mwenyewe. Amua kujingalia kwa ndani na kukubali kujikosoa hata kama inaumiza. Kuendelea kutamani hakutakusaidia sana kuona matunda halisi ya matamanio hayo usipojibaini na kuibaini sadaka yako.

Kuendelea kutamani au kutaka bila kuangalia upekee wako ni sawa na kwenda Dukani bila fedha na kutaka kuchukua bidhaa. Kumbuka hata mkopo huwekewa dhamana. Wewe na Mimi tunatoa nini au tunawekeza nini ili kupata tuyatakayo?.

Unajisikiaje juu ya swali hili siyo suala langu kwa sababu hata Mimi niliyeandika haya yote kuna namna ninayojisikia. Jambo la msingi ni hatua utakazochukua kuelekea kwenye kujitafuta.
Bado najitafuta pia.

river basin2.jpg
 
Akili inakataa maandishi haya yaliyobeba mawazo yako....
I always affirm strongly that "there is pure life somewhere elsewhere..(source/essence/form)...immaterial and immortal.
Dhima ya maisha ni kuishi na sio kutafuta sababu au maana ya wewe kuishi. Ishi leo maana hakuna sehemu nyingine tena utakayoishi baada ya "Existence" yako kufutiliwa mbali kwa kifo.

Existing is such a paradox, Kuishi ndio Mision kuu.
 
Ulichosema ni kweli kabisa maana maisha haya nikujipambania wewe kama wewe sio kumuangalia mtu...
 
Back
Top Bottom