Una habari? Watu 7,000 wanakufa kila saa!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,759
Reaction score
7,573
Takribani watu 7,000 wanapoteza maisha yao kila saa, duniani. Takwimu hizi zinashtua, ila zinapaswa kutufanya tufikirie kwa kina kuhusu maisha yetu yajayo.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na Idara ya Idadi ya Watu ya Umoja wa Mataifa (UN DESA). Sababu za vifo ni nyingi.

Lakini swali kuu ni hili: Je, wewe ukifa leo, utaenda wapi?

Kifo hakigongi hodi. Kinaweza kuja bila taarifa, asubuhi au jioni, ukiwa barabarani au umelala.

Biblia inatuambia:
"Watu wamewekewa kufa mara moja, na baada ya hapo hukumu." (Ebr 9:27)

Fanya haraka, "ukate tiketi" ya kuingia mbinguni na kuikwepa hukumu ya moto wa milele. Tubu dhambi zako zote, umpokee Yesu Kristo moyoni mwako kwa imani, awe Bwana na Mwokozi wako. Yesu ndiye njia pekee ya kutufikisha mbinguni(Yn 14:6).
 
Maadam tupo zaidi ya billion 8 ni sawa pia kuwa na idadi ya vifokama hivyo maan pia wanaozaliwa ni wengi zaidi
 
mpaka sasa wamekufa watu 92.5 billion so kusingekuwa na vifo tungekuwa watu 100.8B
 
Hiyo idadi ni Sawa Sawa na wanaozaliwa kwa kila sekunde
 
Tunaishi mara moja tu.... Maisha yajayo hayatuhusu bali yatawahusu watakaokuwepo
Ndugu yangu, Shing Yui
kusema kuwa maisha yajayo hayatuhusu ni kupuuza ukweli ulio wazi katika Neno la Mungu. Biblia inatufundisha kwamba kuna maisha baada ya kifo: adhabu ya milele motoni au uzima wa milele mbinguni.

Wapi tutaishi baada ya kifo, inategemea uamuzi wetu wa kumkubali au kumkataa Yesu Kristo sasa.
 
Ikiwa siamini katika vitabu vya dini hatma yangu itakua ipi?
 
Kama huamini katika vitabu vya dini, haimaanishi kwamba ukweli wa maisha ya baadaye hautakuathiri. Ukweli unabaki kuwa ukweli, hata kama mtu haamini. Mungu yupo, na Neno lake ndilo linalotufunulia hatima ya maisha yetu baada ya kifo. Hatima ya mtu ni katika maeneo mawili tu: anayeamini anaingia mbinguni. Asiyeamini anatupwa motoni milele.

Mungu anakupenda na hataki upotee. Ndio sababu umesikia habari hizi. Amini.
 
Unamaanisha mababu na mabibi zangu waliofariki kabla hatujaletewa dini wataenda kuchomwa motoni kwa kutoamini kitu ambacho hawakukijua?
 
Andiko hili linawahusu mababu na mabibi waliofariki kabla ya kusikia Injili:
Warumi 2:12-16
"Wale wanaotenda dhambi bila kuijua sheria wataangamia ingawaje hawaijui sheria. Na wale wanaotenda dhambi wakiwa wanaijua sheria watahukumiwa kisheria. Maana sio wanaosikia sheria ndio walio waadilifu mbele ya Mungu, ila wenye kuitii sheria ndio watakaokubaliwa kuwa waadilifu. Mathalani: Watu wa mataifa mengine hawana sheria; lakini kila wanapotimiza matakwa ya sheria wakiongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa kipimo cha sheria ingawa hawaijui sheria. Mwenendo wao unaonesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea. Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo."
 
Ndugu yangu, Shing Yui
kusema kuwa maisha yajayo hayatuhusu ni kupuuza ukweli ulio wazi katika Neno la Mungu. Biblia inatufundisha kwamba kuna maisha baada ya kifo: adhabu ya milele motoni au uzima wa milele mbinguni.

Wapi tutaishi baada ya kifo, inategemea uamuzi wetu wa kumkubali au kumkataa Yesu Kristo sasa.
Maisha baada ya kifo yapo kwa wanaoamini,,kama kuna wa2 hawaamini ipo siku yao!!
 
Ndugu yangu, Shing Yui
kusema kuwa maisha yajayo hayatuhusu ni kupuuza ukweli ulio wazi katika Neno la Mungu. Biblia inatufundisha kwamba kuna maisha baada ya kifo: adhabu ya milele motoni au uzima wa milele mbinguni.

Wapi tutaishi baada ya kifo, inategemea uamuzi wetu wa kumkubali au kumkataa Yesu Kristo sasa.
Walioandika biblia na quran ni matapeli tu
 
Back
Top Bottom