Una habari? Mwisho wa mambo yote umekaribia!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala. Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendo husitiri wingi wa dhambi.
 
Hicho ni kifungu kutoka 1 Pet 4:7-14
Mwisho wa mambo yote... Mambo gani hayo yanayokaribia mwisho?
Tuwe na akili... Kwani hatuna akili?
Tukeshe katika sala... Tusilale? Tukae tukiomba tu?
Upendo husitiri wingi wa dhambi... Nini maana yake?

Tusaidiane kujibu maswali hayo kwa usahihi.
 
Uzwazwa mtupu. Tumesikia uongo huu tangu tukiwa vichanga na sasa tunazeeka na hamna kitu. Kesha mwenyewe kwa vile mwisho wako umefika.
 
CCM imefika mwisho, wanakumbushwa kukesha na kusali
 
Gwajima kafurushwa, rudi kanisa lako la asili, achana na matapeli, umewachangia kununua magari na majumba ya kifahari, umebaki fukara, hujachoka tu?
 
Uzwazwa mtupu. Tumesikia uongo huu tangu tukiwa vichanga na sasa tunazeeka na hamna kitu. Kesha mwenyewe kwa vile mwisho wako umefika.
2 Petro 3:8-9
"Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani anakawia, bali huwavumilia, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba."

Andiko hilo linaonyesha kwamba Mungu yuko juu ya muda, na hachelewi kama wanadamu wanavyofikiri. Subira ya Mungu si uzwazwa, bali ni rehema; anatupa nafasi ya kutubu.

Hebu tufanye hesabu ndogo uone jinsi ambavyo Yesu hajakawia kuitimiza ahadi yake:

Yesu Kristo aliondoka duniani (alipaa mbinguni) takriban mwaka 33 BK. Sasa tuko mwaka 2025.

2025 - 33 = miaka 1992
Sasa tukigeuza miaka hiyo 1992 kuwa “siku” kwa hesabu ya Mungu, unapata siku 1.992 tu(1992/1000 = 1.992)

Hivyo kwa hesabu ya Mungu na kwa kulingana na andiko la 2 Petro 3:8, zimepita takriban siku 2 tu tangu Yesu aondoke duniani. Sasa siku mbili ndio wewe unaona Yesu amekawia? Tubu dhambi zako ndugu yangu Leo X kabla hujachelewa.
 
Hicho ni kifungu kutoka 1 Pet 4:7-14
Mwisho wa mambo yote... Mambo gani hayo yanayokaribia mwisho?
Tuwe na akili... Kwani hatuna akili?
Tukeshe katika sala... Tusilale? Tukae tukiomba tu?
Upendo husitiri wingi wa dhambi... Nini maana yake?

Tusaidiane kujibu maswali hayo kwa usahihi.
Endelea kuota
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom