UN yaingilia kati marufuku ya wanawake kusoma Afghanistan.

Raphael Thedomiri

JF-Expert Member
Sep 1, 2019
442
728
Baraza la usalama la Umoja wa mataifa Jumanne limeomba wanawake na wasichana nchini Afghanistan washirikishwe kikamilifu na kwa usawa,

likilaani marufuku kwa wanawake kusoma kwenye vyuo vikuu au kufanya kazi kwenye mashirika ya misaada ya kibinadamu, iliyowekwa na utawala unaoongozwa na Taliban.

Katika taarifa iliyokubaliwa kwa maafikiano, baraza hilo lenye wanachama 15 limesema marufuku kwa wanawake na wasichana kusoma kwenye shule za sekondari na vyuo vikuu nchini Afghanistan “inawakilisha mmomonyoko unaoongezeka wa kuheshimu haki za binadamu na misingi ya uhuru.”

Marufuku kwa wanawake kusoma kwenye vyuo vikuu ilitangazwa wiki iliyopita, wakati Baraza la usalama likikutana mjini New York kujadili hali ya Afghanistan.

Wasichana walipigwa marufuku kusoma kwenye shule za sekondari tangu mwezi Machi.

VOA
 
Taliban wana Imani ya kulevya. Wanahisi Bado wanaishi enzi za Mtume S. A. W. Hata Mtume kama angekuwepo hai mpaka Leo asingeweza kufanya kama wanavyofanya.
 
Taliban kampa kichapo anaejiita superpower US+NATO nzima,Leo ndio aje apigiwe kelele na hao toothless dog waitwao UN? Impossible
 
Back
Top Bottom