UN: Kama maambukizi ya COVID-19 ndani ya jamii yamedhibitiwa, fungueni shule

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID- 19 likiendelea kuripotiwa maeneo mbalimbali duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa tamko lake la kisera lenye lengo la kuhakikisha kuwa janga hilo halizidishi pengo lililokuwa la walio na elimu na wasio na elimu.

Tamko hilo alilolitoa kwa njia ya video jijini New York, Marekani hii leo pamoja na kuweka bayana changamoto za elimu zilizokuwepo kabla ya COVID-19 na baada ya COVID-19, linaeleza kuwa hata hatua zilizochukuliwa za kutoa elimu kwa njia ya televisheni na radio wakati huu ambapo shule zimefungwa bado zimeonesha pengo la wenye fursa na wasio na fursa.

1596534748922.png

“Katikati ya mwezi Julai, shule zilikuwa zimefungwa katika nchi zaidi ya 160 na kuathiri zaidi ya wanafunzi bilioni 1. Takribani watoto milioni 40 duniani kote wamekosa elimu yao muhimu ya awali. Na wazazi, hususan wanawake wamelazimika kubeba mzigo mzito wa malezi nyumbani,” amesema Katibu Mkuu.

Akifafanua kuhusu mbinu mpya ya kufikishia masomo wanafunzi majumbani, Bwana Guterres amesema, “licha ya masomo kupelekwa kwa njia ya redio, televisheni na mtandaoni, na juhudi kubwa za walimu na wazazi, wanafunzi wengi bado hawajafikiwa. Wanafunzi wenye ulemavu, wale walio katika jamii ndogo au za pembezoni, wakimbizi wa ndani, wakimbizi na wale walio maeneo ya ndani wako hatarini kuachwa nyuma.”

Amesema hata wale wanaobahatika kupata elimu kwa njia hizo bado mafanikio yanategemea mazingira wanamoishi ikiwemo mgawanyo sawia wa majukumu ya nyumbani.

Janga hili la elimu halijawahi kutokea
“Hivi sasa tunakabiliwa na janga la kizazi ambalo linaweza kupoteza uwezo usiojulikana wa kibinadamu, kusambaratisha maendeleo yaliyopatikana miongo kwa miongo na kuongeza zaidi pengo la ukosefu wa usawa,” amesema Katibu Mkuu.

Amesema ni kwa mantiki hiyo tamko lake la kisera linazindua kampeni mpya ya Umoja wa Mataifa na wadau wa elimu ikipatiwa jina Okoa Mustakabali wetu.

“Tuko katika kipindi cha kuamua hali ya baadaye ya watoto na vijana wetu. Maamuzi ambayo serikali na wadau wake wanachukua sasa yana athari za kudumu kwa mamilioni ya vijana na maendeleo na matumaini ya nchi kwa miongo ijayo,” amesema Katibu Mkuu akitaja maeneo manne ambayo sera yake inaangazia.

Mosi, fungueni shule
Guterres anasema kuwa pindi maambukizi ya COVID-19 yakidhibitiwa ndani ya jamii, suala la kurejesha wanafunzi shuleni na vyuoni kwa kuzingatia kanuni za afya linapaswa kupatiwa kipaumbele.

Amesema kuwa, “tumetoa mwongozo wa kusaidia serikali katika suala hili gumu. Itakuwa muhimu kuweka mizania ya athari za kiafya na elimu na ulinzi wa watoto, na pia kuzingatia athari za ushiriki wa wanawake kwenye nguvukazi. " Hata hivyo amesema mashauriano na wazazi, walezi, walimu na vijana ni muhimu katika kufikia uamuzi huo.

Pili elimu ipatiwe kipaumbele cha kupatiwa fedha
Guterres amesema hata kabla ya janga la Corona, nchi za kipato cha chini na kati zilikuwa zinakabiliwa na pengo la dola trilioni 1.5 katika sekta ya elimu kila mwaka na penog hilo linazidi kuongezeka, “bajeti za elmu lazima zilindwe na ziongezwe. Na ni muhimu kwamba elimu iwe katika kitovu cha juhudi zetu za mshikamano kimataifa, usimamizi wa madeni, mipango ya kuchechemua uchumi, maombi ya misaada ya kibinadamu na misaada rasmi ya maendeleo.”

Tatu, tulenge walio maeneo ya ndani zaidi
Hapa Katibu Mkuu ameangazia makundi ambayo yanaachwa nyuma kwenye mipango ya elimu hususan nyakati za dharura na majanga, makabila mdogo,, wakimbizi na watu wenye ulemavu akisema kuwa, “changamoto zao za kipekee wanazokabiliana nazo lazima ziangaziwe, watoto wa kike, wavulana, wanawake na wanaume na lazima tusake mbinu za kuondoa pengo la kidijitali.

Nne, mustakabali wa elimu uko hapa
Kwenye kipengele hiki, Katibu Mkuu anasema kuwa hivi sasa jamii ina fursa mpya ya kizazi ya kufikiria upya elimu, “tunaweza kusonga kwa kasi kwenye utoaji wa elimu bora kama njia ya kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu. Ili kufanikisha hili lazima tuwekeze kwenye elimu ya kidijitali na miundombinu yake. Mabadiliko katika mbinu za kujifunza kunachochea na kuimarisha muunganiko wa elimu rasmi na isiyo rasmi.”

Ametamatisha tamko lake la kisera akiseam kuwa, “wakati huu ambapo dunia inakabiliwa na ukosefu wa usawa katika viwango tunahitaji elimu- kitu cha kujenga usawa kuliko wakati wowote ule. Lazima tuchukue hatua za kijasiri sasa, kujenga jamii jumuishi, yenye mnepo, mifumo yenye elimu bora kwa itakayoendana na siku za zijazo.”
 
Back
Top Bottom