kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,956
- 17,368
UN imekuwa na kazi ya kushughulikia migogoro inapotokea katika nchi wanachama kwa njia za kufanya usuluhishi, kutuma majeshi, kuwekea vikwazo na kutuma misaada kwa wahanga wa machafuko ya kivita. Njia hizi zipo lakini zinaonekana hazifui dafu katika kupunguza migogoro ndani na kati ya nchi wanachama. Njia nyingine kama vile kuwekea vikwazo na kupeleka majeshi zina madhara makubwa kwasababu zinaumiza hata raia wa kawaida wasiokuwa na hatia. Kupeleka misaada pia ni shida kwakuwa misaada mingi haiwafikii walengwa na wakati mwingine hata watoa misaada wenyewe huwa wanauawa wakati wanapotoa misaada hiyo.
Hivyo, UN haina budi kuja na njia mpya za namna ya kuzuia migogoro isitokee badala ya kushughulikia migogoro. Mimi napendekeza UN ifanye yafuatayo ili kupunguza kama si kuzuia migogoro isitokee:
1. UN iwe na kitengo rasmi cha kukagua, kusimamia utungwaji na utekelezwaji wa katiba zote za nchi wanachama ili kuona kama hazina viashiria vya migogoro kama vile kubinywa kwa haki za binadamu, utawala wa sheria na uvunjwaji wa katiba. Hii itapunguza migogoro inayosababishwa na utungwaji, utekelezwaji na uvunjwaji wa katiba badala ya kusubiri migogoro inayotokana na katiba mbovu au zilizovunjwa na watawala itokee
2. UN iwe na kitengo cha kuangalia uteuzi wa tume zote za uchaguzi za nchi wanachama na namna chaguzi zinavyosimamiwa na kuchukua hatua hapohapo mara moja kabla migororo inayosababishwa na tume mbovu za uchaguzi na usimamizi mbaya wa chaguzi haijajitokeza
3. UN iwe na kitengo kinachoshughulikia kwa haraka na kwa nguvu zote migogoro inayohusu mipaka ya nchi wanachama kabla haijasababisha vita.
Hivyo UN itumie rasilimali zake nyingi katika kuzuia migogoro badala ya kushughulikia migogoro.