UN General Assembly: Mahudhurio ya JK


JK amekalia misumari sasa hivi
 

Mkuu, Bwana Kikwete anawakilishwa na Waziri Mkuu Pinda,Katika Mkutano huu wa 66 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.Kuna tetesi ktk duru za ndani za siasa za Tanzania kuwa hata kama Rais Kikwete ataweza kuukwaa tena Urais ktk Uchaguzi Mkuu wa Oktoba,Bwana Pinda hatorudishwa tena ktk nafasi yake ya Uwaziri Mkuu.Kuna mambo makubwa kati ya Waziri Mkuu na Mheshimiwa Rais,kuna taarifa kuwa ni karibu miezi miwili sasa watu hao hawajakuwa pamoja katika mazungumzo ya kiserikali kama ilivyokuwa awali,kuna watu wa karibu na Waziri Mkuu wanasema Bwana Pinda hakupenda wala kuafiki mambo ya Zanzibar ambayo kwa kiwango kikubwa yalikuwa na baraka zote za Mheshimiwa Rais.

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa kupitia CUF alishawahi kusema hadharani kwamba Pinda hafai kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.Mheshimiwa Maalim Seif ni fundi wa siasa za Uvunguni,kwa wale wanamuolewa watajua/kumbuka jinsi alivyommaliza Mzee Jumbe kwa Mwalimu Nyerere na kusababisha Jumbe kuvuliwa Uongozi (kulazimishwa kujiuzulu) na kutangazwa kwa kuchafuka kwa hali ya hewa Zanzibar.

Pamoja na Waziri Mkuu Pinda,pia Rais Mstaafu Benjamin Mkapa yupo mjini New York na wote wawili kwa pamoja ni waalikwa katika Mkutano wa Rais Mstaafu wa Marekani .Bill Clinton utakaofanyika New York Jumanne ya tarehe 21/Sept na unatarajiwa kuhudhuriwa na Wakuu wa Nchi 20,Asasi binafsi ya Rais Clinton inajulikana kama Clinton Global Initiative.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…