UN Employment Scam - Kuweni Macho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UN Employment Scam - Kuweni Macho

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Tiba, Mar 26, 2012.

 1. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Sometimes in January 2012, kuna tangazo la kazi kutoka shirika moja la UN - Commission for International Development (UNCFID). Kwenye tangazo hilo kulikuwa na kazi nyingi na duty station ilikuwa ni Geneva. Mimi nilivutiwa kuomba kazi mojawapo ambayo niliiona inaenda na proffile yangu. Nilipeleka maombi na baada ya wiki tatu nililetewa maswali ya interview na nilipewa siku nne niwe nimerudisha majibu. Nilifanya hivyo.

  Baada ya wiki mbili tena, nilipokea simu ikinitaarifu kwamba nimefaulu written interview na kwamba sasa natakiwa kuhudhuria oral interview through telephone. Tulikubaliana wakati wa hiyo interview na wakati ulipofika walinipigia simu. Nilijibu maswali yao kama nilivyoweza, walikuwa watu watatu kwenye hiyo interviewing panel.

  Tarehe 1 March 2012, nilipokea email kutoka kwao ikinitaarifu kwamba nimefaulu interview na hivyo wakanipa offer ya hiyo kazi. Waliniletea mkataba wa kazi ambao walinitaka ni-usign na kuwarudishia. Walinitaarifu kwamba ingawaje duty station yangu itakuwa ni Geneva, itabidi niende New York kwa muda wa mwezi mmoja kwa ajili ya in-deep training. Walinitaarifu kwamba agent wao angewasiliana na mimi ili kunipa taratibu za kuomba visa na mambo mengineyo. Walinitumia fomu za kujaza na kupeleka kwa huyo agent.

  Baada ya kupeleka form hizo kwa agent (Miyake Corporation) walinijibu na kunipa taratibu za kupata visa ya kuingia Marekani huku wakisisitiza kwamba sipashwi kutafuta hiyo visa bila kupitia kwao. Gharama za hiyo visa ndizo ziliniacha mdomo wazi, ukitaka ya haraka ni USD 3,940 n a ile ya kawaida ni USD 2,750. Kwa gharama hizo machale yalinicheza na kuamua kuwaandikia kwamba hizo gharama ni kubwa na kwamba nitawalipa hizo hela baada ya kuwa nimeanza hiyo kazi au waniletee barua ya Mwaliko ili mimi niitumie kuomba visa mwenyewe. Walipopata hiyo email yangu, wakanitumia form wakisistiza nilipe kupitia account namba waliyonipa na kwamba nikifika New York nitarudishiwa gharama zangu zote na ofisi. Wakanitumia Reimbursement Claim Form.

  Kabla ya kuwajibu, nililazimika kuzama kwenye internet kutafuta hilo shirika la UN linaloitwa UNCFID. Ajabu sikupata jibu lolote kuonyesha kwamba hilo shirika lina website. Nitakajaribu kuitafuta hiyo Miyake Corporation na kugundua kwamba kampuni hiyo ipo huko Marekani lakini haihusiki na travel agent hata kidogo. Lakini through searching (google) nikaja kugundua kwamba lile tangazo la kazi ilikuwa ni employment scam.

  Nimelazimika kuileta hii habari hapa kwa kujua kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba kuna wana JF wengine waliomba hizi kazi na kwa sasa wako kwenye mchakato wa kuibiwa pesa zao na hawa matapeli. Kama sio wewe basi ni ndugu yako, be aware hawa ni wezi na hakuna shirika la UN linaitwa United Nations Commission For International Development.

  Nawasilisha.

  Tiba
   
 2. M

  Muhyi el dein New Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana, na pia ahsante kwa kutuzindua wana jf.
   
 3. m

  moshingi JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole Mkuu umenusurika katika mdomo wa mamba...
  Mara nyingi matapeli hawa wapo makini sana katika kugundua tamaa
  za watu kisha huitumia tamaa yako mwenyewe kukuliza...
  Ushauri kwa yeyote anayeona tangazo la kazi au jambo lolote
  la kuvutia ni muhimu ukawasiliana na mamlaka husika kwa kufika
  mwenyewe katika ofisi zao...ikatokea umekutana na mtu katika mamlaka hiyo
  labda akawa kwenye njama moja ni vema ukatumia vema kamera ya simu yako
  kuwapiga picha. rafiki yangu alitapeliwa T.sh 20ml kwa deal ya kuuziwa mini bus
  aliwapiga picha wahusika ambao walimpeleka show room wakaingia makataba lakini
  alipowapa hela walitoweka... picha alizowapiga kutumia simu yake zilisaidia walikamatwa
  na akarejeshewa fedha zake.
   
 4. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Huu utapeli sasa umevuka mipaka, wanaihusisha na kutumia jina la UN? Hii ni hatari.

  Tiba
   
 5. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Ni kweli mkuu nilishafikiria pa kuipata hiyo USD 2,750 lakini baadae nikashtuka. Nafikiri watu wanaopost nafasi za kazi hapa inabidi nao wawe wanakuwa na uhakika na hizo kazi sio kutuletea kanyabwoya hapa. Ningelizwa!!!

  Tiba
   
 6. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Asante kwa taarifa,
  Wizi sasa umeshika kasi sana
   
 7. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Si mchezo!!!!!

  Tiba
   
 8. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  aksante kwa taarifa mkuu, hawa jamaa ni mtapeli wa kimataifa, tuwe macho.
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Haaaaaaaa Pole sana wanigeria walitaka kukuingiza choo cha kike.
   
 10. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kwamba hawa ni matapeli wa kimataifa, lakini UN infanya nini kuhakikisha jina lake halitumiki kwenye utapeli kama hivi? Kuna ukweli kwamba UN haikuliona hili tangazo la kitapeli na kuwaonya watu kwamba hiyo ni employment scam? Hawa watachafua credibility ya UN.

  Tiba
   
 11. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu nimeponea chupuchupu, halafu wako very systematic!!! Utafikiri wanafanya vitu halali!!!

  Tiba
   
 12. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu pia aliponea chupuchupu baada ya kupitia hatua zote ulizotaja. Akaanza kukopa pesa ili kufanikisha hiyo ajira lakini akashauriwa na mkopwaji aende kwanza shirika lolote la UN akacheki uhalali wa hiyo kitu. Ndiko aliambiwa ni scam na amenusurika kuibiwa!
   
 13. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Pole kwanza!!
  =Kwanza hakuna UNCFID kuna UNCDF!
  =Pili nikwamba wakitangaza kazi UN kokote duniani ikiwa nje yamahali ulipo Uelekezwa kwenda kwenye Office za UNDP zilizopo nchi husika!
  Pili ukiisha fanyia interview kwa simu uenda kufanyiwa aral makao makuu ya UN nchi husika!
  =Maswala ya visa ukiwa umemaliza interview zao UN makao makuu nchi husika ushughulikia malipo yote!!gharama zote visa kila kitu wao uwasiliana na watoa kazi na huwatumia account charge na wao un makaomakuu ya nchi husika ukugharamia kila kitu
  =UN hatumiagi hata siku moja agent
  Hizo ni tip chache kuhusiana na mrorongo wakazi za UN katika recruitment.
   
 14. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Inaelekea tuko wengi kwenye hii trap!!! Inabidi tuwe macho sana na hawa matapeli. Sasa sijui ukikpoa USD 2,750 unakuja kuzilipa vipi ukigundua umeingizwa mjini?

  Tiba
   
 15. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Asante mkuu kwa kutufumbua macho. Mimi nilidhani nimeuchinja maana mshahara kwenye calculation sheet walionyesha ningekuwa napata USD 10,760 kwa mwezi baada ya makato na mkataba ulikuwa wa miaka 5. You can imagine!!!

  Tiba
   
 16. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  shabbash.
   
 17. n

  nemmi New Member

  #17
  Mar 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani,hiyo ni kweli,hata mm ilinikuta ila nilishtuka mapema walipoanza kusema kuwa stakiwi kwenda ubalozini ,nitume copy ya pport na details nyingine. So nilichofanya nilienda pale UNDP information desk kuuliza kama wanalitambua hilo shirika la UN wakadai halipo, na hata last yr pia limesumbua sana watu.

  Pia nilienda hata ubalozi wa Swiss,tho wao hawakuwa na masaada,ila walisema UN office hapa ndo watajua.

  So nilipojua ukweli niliwaandikia mail kuwaambia naomba watume infomation kwa UN hapa Tanzania ,kuthibitisha wao ni genuine,basi hadi leo hawajatuma tena email kwangu. Na hizi kazi hizi hizi,za January,ila mm skufanya oral interview bali written tu.

  So wadau kwanza muwe maco kwani unaambiwa kazi zote za UN lazima zitangazwe kwenye website ila ya UN,na si kwa mitandao mingine(zaidi ya ile organisation husika). So tupende kufanya confirmation na ofic za UN hapa km wana taarifa na hizo kazi.
  Tuwe macho jamani.
   
Loading...