Umwamba barabarani wa maafisa wa Serikali mlioko Dodoma, unatumaliza kwa ajali

Usiwe na hasira na Traffic police. Nini uelewa wa dereva? Kuwa na namba za ST isiwe ni umaarufu wa kukiuka sheria. Hiyo inayoonyeshwa ni somo kwa wote! Ukikimbia mkono wa sheria ukakutana na ajali na kifo, nini umwamba wako? Tunakutana nao barabarani na wanalazimisha uwapishe, eti tu kwa sababu kawasha taa kuonyesha ana haraka, mara unawakuta morogoro wnakula supu! wakiondoka upuuzi ule ule!

Binadamu anayependa umaarufu eti hakamatwi, tunapita tu, wanatuogopa, sisi muhimu, sisi waheshimiwa, n.k. haiwasaidii zaidi ya hatari kwao na kwa wengine. Maisha ya umaarufu ni mafupi sana! Barabara ya Dodoma - Dar imekuwa ni ya kuwasha taa tuuuu na overtake za kishenzi tu.
Nani huyo
 
Spidi na vituko hivi vimeanza kipindi hiki baada ya kuhamia Dodoma, maana kuvunja sheria za barabara kwa kisingizio cha uafisa wako, kilikwama kipindi kile mke wa waziri mwenye maringo alipotiwa kibano. Nawaangalia watumishi hawa wa serikali kama kikundi cha watu wanaojiamini wao wako juu kwa ufahamu. Nahisi ni ile syndrome ya kuhama Dar wanaamini bado Dodoma ni mkoani, kumbe wote wamehamia Dodoma. Ujuaji mwingi bila sababu!

Ukiangalia watumishi hao wa wizara ya kilimo walikuwa wengi ktk gari moja na ni watu wazima, wote above 30. ilikuwaje asipatikane hata mmoja mwenye uelewa wa kutoa onyo kwa wenzake na kusikilizwa. Ni kama walikuwa wanamchochea dereva wao asisimame. Wana haraka! Wana kazi muhimu, nk. wako wapi sasa! Nahisi pia ktk hii tumbua tumbua, kuna watu wamepewa madaraka premature. Ukiona mtu anapewa ukurugenzi na anajivuna kwa hilo kama yule aliyewahi kumtolea bastola traffic police pale Morogoro, hiyo ni ishara ya ubora duni wa akili. Ukiwa Mkurugenzi, Mbunge, Waziri, public figure, boss fulani, inatakiwa uwe smart! Ujue risk za kila jambo, hata maneno unayotumia yawe standardized. Leo hii ni bureeeee!
Na mtaamia kaka
 
chakwanza mimi sio polisi,na chapili hizi picha zilitolewa mitandaoni na polisi baada ya hii ajali kusudi madereva wazembe wajifunze kitu,na cha tatu jukumu la kusimamia sheria hasa za barabarani si la polisi pekee bali nilakila mtu hata hao waliopata ajali walitakiwa wajijali wao kwanza kwa kufuata alama za barabarani na kuwa na mwendo ambao hauta hatarisha maisha yao,damu zao zipo juu ya vichwa vyao wenyewe hasa dereva ambaye alikuwa anakimbia bila kufuata alama za barabarani,usitegemee traffiki wakusaidie na namna ya kuendesha gari kama huwezi kufuata sheria za barabarani kwa manufaa yako na yawengine usiendeshe gari
Hahaha
 
Sasa ukutane na hawa wana WA Dora. Au ving'ora juu utashangaa hii miendo ya kifo inawapeleka kuzimu.nilikutana na msafara WA mmoja WA marais wetu mpendwa Mimi na Volkswagen kangu T126AAD tena kwenye kona niliamini kwa mwendo ule lazima tufanye uchaguzi maana speed zao ilikuwa wanazunguka around makaburi yao.nadhani walifika salama.nashauri sheria ikate huku na huku.
Hao hawapati ajari mkuu
 
Ajali za magari madogo ya Serikali ina sura nyingi.
Tukumbuke kwanza, madereva wazoefu walienguliwa kwa kukosa vyeti vya Form IV.

Madereva vijana wengi wana uzoefu tu wa kuendesha mijini, hasa wale waliohamia Dodoma toka Dar.

Wengi wa madereva vijana hawaelewi kuwa huko porini barabarani, mfalme ni malori.

Malori yanaenda mwendo wa kawaida na hayana papara.
Vile vile malori yakishika mwendo na yana mzigo tani 20 hadi 40, hayana breki za karibu.
Kupunguza mwendo ni kwa kupangua gia.
Hivyo lori haliwezi kukukwepa, haliwezi kupiga breki kusimama ghafla.

Kwa mtaji huu madereva vijana wengi watapotea na abiria wao wakicheza na malori yenye mwendo na yaliyosheheni mzigo.
Sawa
 
Ndo madhara ya kulazimisha watu wahamie dodoma bila maandalizi....wewe unategemea nini mtu anaishi Dar lkni kituo cha kazi ni dodoma kwahiyo hamna namna akichelewa atatumbuliwa bure, familia yake na mkopo nani atavimudu akikosa ajira kwa ujinga wa kufuata sheria za barabarani....hamna jinsi mkuu.
Kwa hiyo aendeshe mwendokasi ili asababishe ajali na afe kabisa simply kwa sababu ulizozita hapo juu mkuu au?? Wakati mwingine tumia akili vizuri ulizopewa na Mungu!!
 
Ajali za magari madogo ya Serikali ina sura nyingi.
Tukumbuke kwanza, madereva wazoefu walienguliwa kwa kukosa vyeti vya Form IV.

Madereva vijana wengi wana uzoefu tu wa kuendesha mijini, hasa wale waliohamia Dodoma toka Dar.

Wengi wa madereva vijana hawaelewi kuwa huko porini barabarani, mfalme ni malori.

Malori yanaenda mwendo wa kawaida na hayana papara.
Vile vile malori yakishika mwendo na yana mzigo tani 20 hadi 40, hayana breki za karibu.
Kupunguza mwendo ni kwa kupangua gia.
Hivyo lori haliwezi kukukwepa, haliwezi kupiga breki kusimama ghafla.

Kwa mtaji huu madereva vijana wengi watapotea na abiria wao wakicheza na malori yenye mwendo na yaliyosheheni mzigo.
Nimekuelewa sana mkuu
 
Back
Top Bottom