Umuhimu wa upinzani bungeni

Anfaal

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
1,154
112
Mara baada ya uchaguzi mkuu, Chama cha Demokrasia na maendeleo kimeibuka kuwa ndio chama kikuu cha upinzani nchini. Juhudi za viongozi wa CHAMA hicho si za kubezwa. Kiuhalisia viongozi hawa wamewekeza muda na rasimili zao, za wanachama na hata wananchi wa kawaida na kukifanya CHAMA hicho kifike hapo kilipofika leo hii. Lakini pia kwa namna ya pekee, nguvu ya mtandao imekifanya CHAMA hicho kuimarika zaidi.
CHANGAMOTO kuu iliyopo mbele yake ni kukisuma chama hiki kwenda mbele. Ukweli ni kwamba organizeshen zozote zikikuwa mara nyingi ndio matatizo huongezeka. Na mikikimikiki ya ukuaji mara nyingi hupunguzwa na uwepo wa uwazi, uwajibikaji, haki na usawa. Kama haya yatakosekana basi ni rahisi kwa taasisi husika kuyumba. Mfano, sasa hivi CHADEMA imepata wabunge wapya wengi tu na ushawishi wao kabla ya chaguzi ulikuwa haufahamiki lakini huenda uchaguzi utawafanya wengi wawe maarufu kuliko hata wale waliopo CHADEMA. Uchaguzi huu huenda umewaleta watu waadilifu, wachapakazi na wanaosimamia haki kuliko hata wale waliokuwepo. Watu hawa ni muhimu kwa Taifa letu, tusiwabeze, tuwape uzoefu na nafasi ya kukitumia CHAMA.
Tukiachana na hayo, CHADEMA wamechagua viongozi viongozi wa upinzani bungeni. Safu yao ni nzuri na imeweza kuondoa hisia za makundi ambazo wengi huamini yapo. Lakini sasa; ipo haja kuu ya kushirikiana na wapinzani wenzao. Wapo viongozi wengi wa vyama vya upinzani ni wazuri saana na hawa wakitumika ipasavyo lengo kuu la upinzani, huenda likafikiwa; Maendeleo ya Taifa.
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,547
Sidhani kama kazi kubwa ya upinzani bungeni ni kupinga kila kitu, isipokuwa baadhi ya mambo ambayo hayaendi sawa.
Vilevile wabunge wote ni sawa, kwa maana ya wabunge wa upinzani pamoja na wale wa chama tawala.

Isipokuwa kwa nchi yetu mambo huwa tofauti, ambapo wabunge wengi wa chama tawala ni wale waliopitishwa kwa maslahi ya watu fulani ( Lowassa, Kikwete, Chenge, Rostam nk,).

Ndiyo maana inasemekana kwamba uwezo wa Tundu Lissu wa chadema ni sawa na wabunge 80 wa ccm.
 

Anfaal

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
1,154
112
Sidhani kama kazi kubwa ya upinzani bungeni ni kupinga kila kitu, isipokuwa baadhi ya mambo ambayo hayaendi sawa.
Vilevile wabunge wote ni sawa, kwa maana ya wabunge wa upinzani pamoja na wale wa chama tawala.

Isipokuwa kwa nchi yetu mambo huwa tofauti, ambapo wabunge wengi wa chama tawala ni wale waliopitishwa kwa maslahi ya watu fulani ( Lowassa, Kikwete, Chenge, Rostam nk,).

Ndiyo maana inasemekana kwamba uwezo wa Tundu Lissu wa chadema ni sawa na wabunge 80 wa ccm.
Kazi kubwa ya upinzani si kila kupinga kitu. Lakini uhai wa upinzani unaanzia bungeni. Mf Hamad Rashid na Dr Slaa, hawa watu wamekuwa maarufu kwa kiasi kikubwa kutokana na nyadhifa zao walizokuwanazo. Kwa hiyo kama wapinzani watakuwa live na hata wasipotimiza yale waliyoahidi wananchi bado wataendelea kuaminika tu.
Hivi hiyo ya wabunge 80 wa CCM kulinganisha na Tundu Lissu mnaipimaje? Hii ni dharau na haipaswi kuendekezwa. Basi kwa hali hiyo huyo Lissu angekwenda akapiga kampeni majimbo hata 79 ili yachukuliwe na CHADEMA maana anauwezo mkubwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom