Umuhimu wa suala la umri Serikalini

Umuhimu wa suala la umri Serikalini

M-Manoti

Member
Joined
Nov 10, 2017
Posts
7
Reaction score
6
Kama kichwa cha mada kinavyojieleza. Nafikiri kuna umuhimu mkubwa kwa serikali kuliangalia suala la umri kwa wananchi wake ili kupunguza au kuondoa kabisa sintofahamu na maswali hapo baadae.

Nasema hivyo nikiwa na maana gani, yaani kwa mfano kama sasa walivyotangaza kwamba mwanafunzi kudahili kujiunga na kidato cha Tano mwisho ni mwenye miaka 25.

Kwahiyo hata kwenye matangazo ya ajila au kujitolea yawe yanashabihiana kwa kuweka ukomo wa kiumri kwa kuangalia vigezo vya kiumri kwenye Elimu. Mfano mwingine mwaka jana vigezo kwa mwanafunzi aliemaliza kidato cha sita kujiunga na JKT ilikuwa mwisho miaka ishirini na mitatu (23).

Sasa hapa tayari kunakuwa na ukinzani yaani wa kiumri nikama kunakuwa vile hakuna ushirikiano kati ya idara moja ya serikali na nyingine *ukinzani "umri kujiunga kidato cha tano mwisho miaka 25 na umri wa mwisho kujiunga na JKT kwa aliyehitimu kidato cha sita ni miaka 23".

Nafikiri hili serikali italiangalia na kulirekebisha kwa njia bora zaidi.

NAWASILISHA
 
walipopitiliza ni pale waliposema hata shule za watu binafsi zisichukue wanafunzi wenye umri mkubwa why!!?? kama mimi nina miaka 25 nakwenda kusoma kwa ajili ya kujielimisha binafsi kwani elimu haina mwisho nalipia pesa zangu binafsi wao serikali inawahusu nini!!??? na pia wanavunja haki za binadamu zinakataza Age discrimination.
 
Wanadhani wanapunguza matumizi ya serikali ili waijenge chato, kumbe wanazidi kuongeza wafuasi wa mange.
 
walipopitiliza ni pale waliposema hata shule za watu binafsi zisichukue wanafunzi wenye umri mkubwa why!!?? kama mimi nina miaka 25 nakwenda kusoma kwa ajili ya kujielimisha binafsi kwani elimu haina mwisho nalipia pesa zangu binafsi wao serikali inawahusu nini!!??? na pia wanavunja haki za binadamu zinakataza Age discrimination.
Hili ni jambo lingine linalotakiwa kuangaliwa pia. maana linakinzana na ule usemi kwamba Elimu haina mwisho
 
Inachanganya sana...

Kwa maana hiyo itawalazima watu kufanya QT ingali umri wao bado mdogo...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom