Umuhimu wa server | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umuhimu wa server

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Nov 12, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Nov 12, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  NI SHULE chache zinazoweza kumudu kuwa na kila aina ya vitabu vya kiada na ziada vinavyohitajiwa na wanafunzi wake.

  Ujio wa kompyuta unaweza kutumika vyema kuepuka gharama kubwa ya kununua vitabu kutoka nje.

  Kinachotakiwa ni kwa shule au taasisi nyingine ambayo vitabu na ripoti mbalimbali ni muhimu katika shughuli zake za uendeshaji kuwa na kompyuta inayoitwa seva na mtandao wa kuwezesha watu katika madarasa au maktaba au ofisi mbalimbali kuweza kupata vilivyohifadhika kwa urahisi.

  Seva ni ngamizi (kompyuta) yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi mamia vya vitabu na wakati huo huo kuziunganisha kompyuta mbalimbali ndani na nje ya ofisi kwa mawasiliano ya kila siku.

  Mtandao huandaliwa kwa kuwa na nyaya zenye spidi tofauti kuunganisha kila kompyuta katika shule au ofisi na seva ili watu waweze kuwasiliana ndani kwa ndani na vile na watu au taasisi za nje kiurahisi.

  Katika hili la kuhifadhi mambo mengi, kazi kuu ya seva ni kuhakikisha kila kinachohifadhiwa kinakuwa na nakala kadhaa ndani na nje ya seva yenyewe na kisha kugawa hivi kwa yeyote atakayeomba kuvitumia katika nyakati mbalimbali.

  Tuchukulie, kwa mfano, kuna kitabu cha Uraia na kitabu hiki ni cha Serikali na hakiuzwi.

  Kitabu hiki kinaweza kuwekwa kwenye seva na mwanafunzi yeyote anayetaka kukisoma ataweza kufanya hivyo ilimradi tu apate nafasi katika kompyuta iliyoko kwenye mtandao.

  Kompyuta inaweza ikarahisisha kazi ya kukitafuta kitabu, kurasa au mada husika kwa kiasi ambacho mwanafunzi ataweza kwa saa chache kufanya kazi ambayo ingemchukua saa kadhaa kama angehitajika kwenda maktaba hata ya karibu namna gani.

  Pakiwa na vifaa vya kuchapia mwanafunzi ataweza kuchapa kurasa anazozitaka pengine zile za maswali na majibu na kwenda kuzisoma tena wakati mwingine.

  Mitihani iliyopita

  Katika shule nyingi ni vigumu kupata mitihani iliyopita. Na ninaambiwa si shule tu hata vyuoni bado mitihani iliyopita iko katika makaratasi makuukuu na yaliyochafuka na ni kazi kuomba mpaka upatiwe mitihani hiyo ya zamani.

  Kwa kuwa na seva, mitihani yote ya zamani inaweza kuingizwa kwenye kompyuta na kuwa mtandaoni kwa kila mwanafunzi kuipata pindi atakapo.

  Haitakuwa kitu cha kawaida tena kwa wanafunzi fulani kufanya vizuri kwa kuwa tu wazazi wao waliwahonga walimu na kupata mitihani iliyopita kwani mitihani hiyo sasa itakuwa kwenye seva na yeyote atakaye kuipata bila gharama yoyote.

  Hali kadhalika maswali ya rejea (revisheni) yanaweza kuwepo pia katika mtandao na mwanafunzi kufanya mazoezi kwa muda anaopenda au kushusha maswali na kuyachapa ili kufanya kazi hiyo baadaye bila matatizo.

  Kwa shule za msingi, mwanafunzi anayetarajiwa kufanya mtihani wake wa darasa la saba atakuta masomo yote ya kuanzia darasa la kwanza hadi la sita kwenye mtandao na kujikumbusha kila apatapo nafasi.

  Katika sekondari na vyuo vikuu, kazi hii pia inaweza kufanyika na wanafunzi wakawa na njia mbadala ya kusoma na kufanya marejeo mbali na njia zilizozoeleka.

  Ni rahisi wanafunzi wa vyuo pia kuanza kufanya utafiti kwa kutumia kilichomo kwenye mtandao kwa kiasi fulani.

  Utafiti kwa kutumia mtandao sasa hivi ni somo linalojitegemea katika baadhi ya nchi.

  Kazi kubwa katika utumiaji wa wavuti ni kuwa na mpango na utaratibu mzuri wa kukipata ukitakacho bila kupoteza muda kutokana na shughuli au maelezo mengine yasiyo na maana kwa upande wa mtumiaji kwa wakati huo.

  Uzoefu wa matumizi ya kompyuta bila shaka ni muhimu kabla ya mtu kuanza kufaidika na huduma kama hii.

  Hii ina maana somo la kompyuta litakuwa na umuhimu wa kipekee katika siku zijazo ili kuwawezesha wanafunzi wote waweze kutumia huduma hii bila shida au kubabaika.

  Endapo somo la kompyuta litakuwa kwa Kiswahili basi nusu ya kazi hii itakuwa imekamilishwa na kitakachobaki ni kuongeza ufundi wa wanafunzi katika lugha nyingine ili waweze kufaidika pia na vilivyomo katika lugha nyingine.

  Katika ofisi, mtiririko mzima wa kazi unaweza sasa kufanyika bila mtu kuwa na sababu ya kutoka ofisi moja na kwenda nyingine ili kufuatilia jambo fulani.

  Hata hivyo, hapa sio tu kuna kazi kubwa ya kubadilisha utamaduni wa Mswahili wa kutaka kuonana uso kwa uso kabla jambo halijaeleweka na kufanyika, bali pia ujenzi wa mifumo ya kisasa ya TEKNOHAMA inayowawezesha watu kuona kwamba kazi ni nyepesi na wananchi wanaridhika na huduma zikifanyika kisasa kuliko kwa njia za kizamani kama ilivyokuwa huko nyuma.

  Huu ni utamaduni unaojali muda au wakati kama rasilimali adimu na lolote linalookoa muda kuwa jambo muhimu katika uendeshaji wa taasisi ya kisasa.

  Ni watu wachache wanaojua a-be-chee za seva na mitandao. Ni jambo muhimu pia tukawaelimisha watu juu ya vitu hivi vinavyofanya kazi ili wao wenyewe wawe kichocheo kwa wakuu wao wa kazi kubadilika na kwenda na wakati.
   
 2. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2008
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pamoja mkuu ujumbe tumeupowa na unaingia akilini tu sote
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Yes Shy is ours
   
 4. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kuna yeyote anayeweza kunisaidia KEY ya Windows server 2003?? Nimepoteza boksi la key. I hate kuhamahama!!!!
  Sio lazima iwe ya multiple users, hata single user inatosha, nataka kuchezacheza nayo tu kujifunza mambo.....
   
Loading...