Umuhimu wa serikali kuwapa wananchi taarifa sahihi na kwa wakati

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,102
3,615
Kuna yule binti Mtanzania aliyekuwa mshauri wa rais wa Zambia katika mahusiano ya umma, alisema kwamba, alipofika Zambia alikuta hali ni mbaya sana kuhusu usambazaji wa taarifa kati ya serikali na wananchi kwa sababu serikali ilikuwa haiwapi taarifa wananchi kwa wakati, hali iliyopelekea wananchi kuziamini propaganda chafu dhidi ya serikali.

Binti yule Mtanzania alipofika, akamshauri rais wa wakati huo Edger Lungu kwamba, ni vyema kutoa taarifa za serikali kwa wakati na usahihi ili wananchi wajue kinachoendelea kuhusu nchi yao, na hivyo kuzuia propaganda chafu dhidi ya serikali.

Binti yule akaongeza kwamba, hata kama serikali ilikuwa inataka kufanya jambo fulani zito mfano ubinafshaji, ni lazima serikali iwaeleweshe wananchi wajue dhamira ya serikali na faida za ubinafshaji huo kuliko kukaa kimya.

Binti yule pia alisema, baada ya yeye kutumia mbinu ile, nchi ya Zambia ilitulia na maneno yakapungua kabisa.

Binafsi naweza kumuunga mkono binti yule kwa sababu kabla hajaenda Zambia tulikuwa tunasikia maneno mengi hasi kuhusu Zambia.

Tukija hapa Tanzania, ni lazima serikali itoke mbele na kutuelewesha wananchi tujue faida za kumpa mwekezaji bandari ili tung'amue sisi wenyewe.

Inawezekana kuna faida nyingi kuliko hasara. Kwa upande wangu mpaka sasa sijajua serikali imeingiza, au itaingiza TSH kutokana na makubaliano hayo. Nasikia kipengele cha kukuza ajira tu. Vipi hao DPW hawatoi hela keshi kwa serikali? Kule migodini enzi za Kikwete tulikuwa tunaambiwa serikali inachukua asilimia 4 ya mrahaba na 96 zinaenda kwa mwekezaji. Vipi kuhusu hao DPW jamani?

Kama serikali ikijichimbia kimya, ina maana wananchi lazima waamini ni kweli bandari imeuzwa kama ambavyo ilitokea bandari ya Sri Lanka ilivyochukuliwa na Wachina kwa miaka 100. Tusifikiri Sri Lanka walipenda bandari yao kuchukuliwa, ni kwa sababu ya anguko la kiuchumi ambalo linaweza kuikumba nchi yoyote hata Tanzania.

Mfano mwingine, ukisoma dondoo mbalimbali za mtandaoni unaona kumbe haya makubaliano ya mpito ya miezi 12 kati ya URT na DPW yalifanyika tangu Novemba 2022. Kama hizo dondoo ni kweli, sasa mpaka leo serikali ilikuwa wapi angalau kuanza kuuhabarisha umma na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kubinafsisha bandari kama jambo ni la kheri? Je, kuna nia ovu?

Hawakumbuki bwana yule alipotaka kuhamia Dodoma aliandaa hadi vipindi vya Television ili kuelimisha umma!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
"Whatever is secret is not sincere".

Uzoefu unaonyesha kwamba, mara nyingi waovu au nia ovu huwa inagubikwa na usiri.
 
Back
Top Bottom