Eiyer, usiangalie flani amesemaje, wengi wanaongozwa na unafiki tu. Cha msingi ni kufuata kanuni ulizojiwekea.
Unaweza kujichelewesha kuoa kisa unatafuta pesa, bahati mbaya usiipate hiyo pesa na hata familia uchelewe kuwa nayo. Huwa haya meneno ya "tafuta pesa ndio uoe" yanatoka kwa singles. Labda tungepata insights za wanandoa tungeweza kuoanisha hili swala la pesa na ndoa kwa urahisi zaidi. Coz naona linaleta sintofahamu kubwa katika kizazi chetu.
watu wengi tumeathirika na hii hali unatafuta pesa ndo uoe. shidaa sana
Nilichosema mimi usiipe pesa kipaumbele kwenye ndoa,dada yangu alianza maisha na chumba kimoja lakini sasa wana nyumba tatu tena zenye hadhi na gari na wanapendana mpaka raha japokuwa ndoa yao ina miaka 15,jambo la msingi ni upendo wa kweli na mkisharidhiana mnaishi vyovyote tu PESA NI IBILISI UKIIPA KIPAUMBELE INAKUVUA UTU WAKO.
Hivi usipokua na mpango wa kununua gari au kujenga nyumba kwa mfano, utatafuta hela ili uifanyie nini?Mi nadhani watu wanaitafuta hela wakiwa tayari wana mipango wa nini matumizi ya hizo fedha.
Ni sawa sikatai kuna cases kama hizo....lakini sio haki kuwahukumu maskini wote kwa staili hiyo. Mimi nna ndugu zangu kibao walioanza kwa staili ya kukaa chumba kimoja sasa hivi wana hali nzuri na ndoa zao ziko vizuri tu....hao matajiri wanaogeuka nimewaona kwenye bongo muvi tu kwenye real life sijawahi kuwaona kiukweli
Aisee pesa ndio kula kitu na hio amanii unayoona katika ndoa za watu na kupata taama ya kujiingizaa ni pesaa ndugu yangu! Tafuta pesa halafu tafuta kisu kikalii dunia itakujuaa tuuuuu ndugu
Hela huwa haitoshi milele atafute mpaka lini?
wanaoongoza kwa michepuko ni wanaume walio na hela au ni wanawake walioolewa na wanaume wasio na hela nyingi? Michepuko inachochewa zaidi na Tamaa au umasikini au utajiri?
Kuna mipango ya kutafuta hela, na mipango ya kutumia hela. ukiwaza upande mmoja tu wa shilingi itakusumbua. lazima uwe na yote kwa wakati mmoja.
Sijui ninaposema mipango unachagua kuamini nini. una point ya msingi ila haina corelation na ninachojaribu kukisema... Unaona, unapanga, unatake over. Hela haiji tu... lazima uwe na mipango ya kuzipata, mipango ya kuzibakisha na kuendelea kuziongeza.... ukiacha kimoja wapo utakuwa unazunguka tu hapo ulipo.
Hii ipo kwa wazungu sana au kwa wabongo wachache sana walioshauriwa vibaya,
Hao unaosema masikini wana jeuri saana kwa taarifa yako. Labda ukute ameoa mtoto wa tajiri au mdada mwenye hela kumshinda yeye kama hatokuwa makini na kucheza karata yake vizuri inamlazimu kuwa hivyo...
''Money talks but has nothing to say'' again ''Money is a good servant but a very bad master''. Whatch out how you treat money, can be either your servant or your master... choose wisely and be the MASTER.
Wewe unavyojua matunzo ni kitu gani?
Kuna watu hawana pesa na kke anatunzwa na hana maradhi,sijui kama unalijua hilo
Kwa akili yako ya ajabu naona unaweza kudhani kutunzwa ni kuwa na iPhone 5,kwenda saloon,kuwa na Gari,kuwa na nyumba kali na mengine ya kufanana na hayo,hayo sio matunzo bali ni matatizo tu
Binadamu ana mahitaji yake ya msingi,akishapata uwezo wa kuyatim iza hayo mengine ni utashi tu,binadamu anahitaji kula bila kujali anakula chakula gani na cha gharama gani, kulala bila kujali analala kwenye kitanda cha gharama gani,kuvaa bila kujali anavaa nguo ya gharama gani na mengine ya kufanana na hayo
Najua unaweza kuniona kama mwendawazimu fulani hivi lakini najua ni kwasababu hujui kitu kuhusiana na ukweli wa maisha,ngoja ukiendelea kuwepo kwenye dunia hii utakuja kukumbuka haya
You know nothing about God,so acha kabisa kuen delea kujionesha vile ambavyo hujui kitu
Mungu unamjua wewe?
Yaani kwa akili yako kama ya panzi unadhani Mungu anategemea kitu ambacho binadamu amekitengeneza ili afanye mambo yake,wewe ni wa kuhurumiwa kabisa
Hebu acha kuchekesha watu we binti,hujaolewa halafu unadai ndoa ni pesa,sijui kama uko sahihi wewe
Acha kuishi kwenye ndoto,tafuta watu ambao wamekua na wamekaa muda mrefu kwenye ndoa halafuy waulize kwa adabu halafu uone watakuambia nini cha kujifunza kama unataka kuishi maisha halisi
Labda cha kukumbuka kuhusu hili ni vile ambavyo nilivyocheka nilivyosoma haya maelezo yako!
this is a typical utopian thinking
Kutokana na coment yako bomba nimeona sina cha kukupa zaidi ya kiss.....MMMWAAAAAAAAAAAAH............Lakini sio shavuni........................
Upeo wako WA mwisho kufikiri ni PESA tuu, pesa zisizo na idadi kamili!! bado hadi sasa hujajua definite amount of money worth for you!!!
Think of ideas first then materials will follow you!!!
Unatoka kwnye necessary demands unakimbilia kwnye luxurious ones!!!!
Hekima & busara hata mfalme Suleiman aliiomba kwa Mungu licha ya Ukwasi wake woooote!!!
tinna CUTE!!!!
Kwa msisitizo hela ni muhimu,Ndio maana inafika miaka 2 ndoani watu wamechokana kisa mipango haiendi,kulumbana tu,kulalamika etc
shikamoo upo?1: status; hata uwe na wake mia bila hela utaishia kuitwa mjinga usie na akili
2: Mipango; bila hela hakuna mipango itakayopangika zaidi utakesha ukiota mipango,,,, na ukioa kilaza ndo kabisaaaaaaaaaa!!!!!!!!! utahisi una mikosi ya kila rangi.
3: Watoto; yes watoto ni furaha na faraja baraka kutoka kwa mungu..... but bila hela utawaona ni mzigo na kuchukia mama yao eti haijui nyota ya kijani anaijua ya bluu tu!!!!!!!!!!!!!
Ushauri; tafuta hela,, pata hela,,, waza kuoa over!!!!!"
Hiyo bahati ya dada yako usiote kuipata kirahisi ndugu,,,,,,!
shikamoo upo?
Mimi naomba niishie hapa dada ila kama unataka mume mwema mshirikishe sana Mungu lakini kama pesa ndio kipaumbele sahau mume mwema.