Umuhimu wa michezo kwa watoto

Umuhimu wa michezo kwa watoto

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Michezo inamsaidia mtoto kupanua wigo wa kufikiri, kushirikiana na wenzake, kujenga misuli, kuijua dunia inayomzunguka na mengi mengineyo.

Bahati mbaya ni kuwa katika maendeleo ya binadamu, sehemu ambazo mtoto anaweza kucheza salama bila hofu ya kugongwa na gari, kujikata na chupa au hofu ya kukutana watu wanaoweza kumdhuru ni chache sana.

Mijini hakuna sehemu maalum zilizotengwa kwa watoto kucheza. Ni haki kuwa kila kata ingekuwa na kiwanja kinachotunzwa na halmashauri cha watoto kucheza. Ikiwezekana kuwa na mhudumu pamoja na msafishaji.

1537580842819.jpeg


1537580918861.jpeg

1537581735930.jpeg


Kwa kweli kwa misitu na mbao tulizo nazo hatuwezi kuwapatia watoto wetu utoto uliobora?

Katika tafiti nyingi zilizofanywa zimeonyesha kuwa watoto ambao wanakosa nafasi ya utoto bora ni wale wanaoishi mijini ambao wazazi wao wana kipato cha chini.

Watoto wanaoishi vijijini wana nafasi kubwa ya kucheza bila hofu ya magari kuwagonga na jamii inajuana hivyo uamunifu wa kuwa watoto wako salama ni mkubwa. Lakini si vibaya wakipewa utaalamu wa kujengea watoto vifaa vya kuchezea kama mabembea.

Watoto wa matajiri wengi wanakua na mabembea nyuma ya nyumba zao au katika shule wanazosoma.
 
Michezo inamsaidia mtoto kupanga wigo wa kufikiri, kushirikiana na wenzake, kujenga misuli, kuijua dunia inayomzunguka na mengi mengineyo.

Bahati mbaya ni kuwa katika maendeleo ya binadamu, sehemu ambazo mtoto anaweza kucheza salama bila hofu ya kugongwa na gari, kujikata na chupa au hofu ya kukutana watu wanaoweza kumdhuru ni chache sana.

Mijini hakuna sehemu maalum zilizotengwa kwa watoto kucheza. Ni haki kuwa kila kata ingekuwa na kiwanja kinaschotunzwa na halmashauri cha watoto kucheza. Ikiwezekana kuwa na mhudumu pamoja na msafishaji.
Wazo zuli, ngoja tumalize stadium ya chattel!
 
Hahaha! Nahisi utakuwa mkatoliki was kindakindaki wasiopenda hata kusifiwa. Wanangu nimewanunulia mpira was kuchezea, pia Mara chache nawapeleka kwenye mabembeo!
Mabembea ni ya bure au unalipia?
 
Nalipia! Akiingia mtoto unalipa 2000,kubembea na kuogelea, ila Mimi sipendi biashara ya kuogelea, nachukia sana maji!
Kuogelea ni life skill ambayo watoto ni muhimu ikiwezekana watoto wote wafundishwe. Fikiria ajali ya MV Nyerere kama wote wangejua kuogelea.
 
Kuogelea ni life skill ambayo watoto ni muhimu ikiwezekana wote wafundishwe. Fikiria ajali ya MV Nyerere kama wote wangejua kuogelea.
unachoongea no sahihi, ila naogopa sana maji.
Inadaiwa nilipokuwa mdogo, tulienda na ndugu zangu kuchota maji, wakaanza kuogelea na Mimi wakaniingiza kwenye maji, nikazama, nikaokolewa na mpita njia, Mimi binafsi sikumbuki tukio hili Bali ninasimuliwa tu, pengine ndio maana sipendi maji kabisa!
 
unachoongea no sahihi, ila naogopa sana maji.
Inadaiwa nilipokuwa mdogo, tulienda na ndugu zangu kuchota maji, wakaanza kuogelea na Mimi wakaniingiza kwenye maji, nikazama, nikaokolewa na mpita njia, Mimi binafsi sikumbuki tukio hili Bali ninasimuliwa tu, pengine ndio maana sipendi maji kabisa!
Pole sana. Watoto huogelea wakiwa tumboni. Hata ukiwawaweka kwenye maji ile miezi mitatu ya kwanza bado wanakuwa na skills zao
 
Swali nje ya mada! Nifanyeje mtoto wangu awe active? Yupo tumboni kwa sasa!
 
Mtoto wa miezi 3 unaweza mfanyisha mazoezi gani? ili awe fiti.
 
Michezo muhim sana ila haipewi nafasi wengi hudhani ni kupoteza muda unapofanya michezo
 
Back
Top Bottom