Umuhimu wa meneja wa kampuni (company manager) kuwa na uwezo wa kufikiri kwa umakini (thinking critically)

Feb 5, 2022
31
49
Critical Thinking ni kitendo cha kufikiri kwa kuzingatia mazingira au hali tofauti tofauti (different contexts) ili kufikia maamuzi yenye tija.

Meneja wa Kampuni (Company Manager) anapaswa kuwa na uwezo wa kufikiri kwa umakini ili kufikia maamuzi ambayo yataiwezesha kampuni yake kufikia malengo.

Ufikiriaji kwa umakini katika kampuni huzingatia vitu vifuatavyo, ambavyo meneja mzuri, hupaswa kuwa navyo.

1. KUTAMBUA NA KUHOJI NADHARIA (identify and challenge assumptions)
Kimsingi tabia na matendo yetu yamejengwa katika nadharia mbalimbali. Na bahati mbaya tumelelewa katika namna ambayo hatuwezi kuhoji hizi nadharia (tumezaliwa tumezikuta na tunaziishi)

Katika biashara, wewe kama meneja lazima uwe na uwezo wa kutambua na kuhoji nadharia ambazo zinajenga "practices" katika biashara yako. Kwa mfano kuhoji nadharia ambazo zinatumika katika eneo la masoko (marketing), rasilimali watu (human resource) n.k. Pindi hizi nadharia zinapoonekana kuwa hazifai (invalid assumptions) meneja mzuri huziacha na kutafuta nadharia zenye kufaa zaidi.

2. KUTAMBUA UMUHIMU WA MAZINGIRA ( Recognizing the importance of contexts)
Meneja mzuri anafahamu kwamba mazingira yana ushawishi katika fikra na matendo yetu. Na kwamba njia itumikayo kutatua tatizo katika mazingira fulani si lazima ifae kutatua tatizo katika mazingira mengine.
Hivyo lazima kuzingatia utofauti wa mazingira ili ipatikane njia itakayoendana na mazingira husika.

3. KUTAMBUA NJIA MBADALA (Imaging & exploring alternatives)
Meneja lazima atafute njia zingine mbadala katika uendeshaji wa kampuni. Ni vyema kuuliza wengine (colleagues) walikabiliana vipi na changamoto katika uendeshaji wa kampuni, ili uweze kujifunza namna walivyofanya.

4. KUTAMBUA UKOMOWA UFAHAMU (Seeing limitations)
Meneja lazima utambue kwamba kuna ukomo juu ya ujuzi, ufahamu na uzoefu ulionao. Hivyo ujuzi ulionao hauwezi kuwa suluhisho kwa kila tatizo linaloibuka katika kampuni yako. Hivyo kuwa tayari kujifunza vitu vipya kwa wengine kwa ustawi wa kampuni yako.

AHSANTE

OMAR MSONGA (BA. PPM & CD)
Consultant
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call + 255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania

IMG_20220715_175647_561.jpg
 
Back
Top Bottom