Kwanini tunashindwa kufikiri kwa makini ?"Critical thinking"

Nov 2, 2023
60
50
Kwanini kila mtu anaongelea kufikiri kwa makini kama ni tatizo kwetu. Kama ni kitu cha muhimu kwenye maisha yetu kwanini mpaka tuhamasishwe kukifanya. Kuna faida nyingi sana ukiweza kutulia na kifikiri kwa makini kwenye matendo yako ya kila siku.

Kitu gani kinachotuwekea kivuli kwenye akili yetu tushindwe kufikiri vizuri. Au mifumo yetu ya kuishi imetujenga kupokea zaidi maarifa na kuyatendea kazi tu ndio akili imefugwa hapo. Huoni umehimu wa kufikiri zaidi kwakuwa umeaminishwa ukipata maarifa yenye kukuingizia fedha maisha ni yameishia hapo. Toka tunakuwa akili yetu imeshabanwa kufwata mifumo haiwezi kuwa huru kwa njia hiyo kutupa ubora wake wote.

Kufikiri kwa makini ni jambo la kujitambua zaidi na si la kutatua matatizo na kufanikiwa kimaendeleo. Tukielekeza akili kwenye mwelekeo wa kishule na kutafuta fedha tu hatutoweza kuona uhalisia wote wa maisha jinsi ulivyo. Tukisema kufikiri kwa makini ni akili iliyokuwa huru kuona kila kitu bila kuwa na mwelekeo wa kibinafsi kutaka kuangalia kwa kufaidika navyo.

Je, kwanini huweza kufundishwa au kuhamasishwa kufikiri?

Jambo lakushangaza kuhusu akili ni hili, kama wewe binafsi huna nia na kitu huwezi ukabadilika kwa kusikia tu. Huwezi kufikiri kama huna swali au tamaa yakutaka kujua au kudadisi kitu "curiosity". Swali kubwa lakujiuliza ni hili, kitu gani kina ondoa uwezo wetu wakudadisi mambo?. Au maarifa tunayofundishwa yamesha kidhi mahitaji yetu yote hatuhitaji kufikiri tena.

Kitu gani kinacholeta mabadiliko kukufanya uweze kufufua udadisi wako, akili kuwa na tamaa ya kutaka kujua zaidi. Unahitaji kuwa na akili isiyo na mipaka yenye uhuru wa kutazama, kusikia na kuhisi kwa umakini pia ili kuweza kuona uhalisia wa mambo yalivyo bila kuwa na vizuizi vya kimawazo (akili iliyokuwa tulivu na kimya kwenye mawazo yake). Ukiwa mtumwa kwenye mawazo yasiyokwisha hutoweza kuona kitu kwa makini na kupata swali ndani yake.

Kufikiri kwa makini kunahitaji akili tulivu yenye nguvu (nishati isitumike kwenye vitu visivyo na maana). Akili iliyochoka na mkanganyiko na kuchanganyikiwa haiwezi kufikiri kwa makini kwenye chochote kile. Muda wote ukiwa na akili inayo tapa tapa utakuwa unapoteza nguvu zako nyingi bila kujua. Mwili unahitaji matumizi sahihi ya nishati kwakuwa si muda wote utakuwa nayo.

Tunahitahi kujitambua thamani yetu mwenyewe kwanza ili tusitetereshwe na ujinga. Ujinga unatutesa na kutuchanganya akili yetu imeshindwa kuwa kitu kimoja na kuleta vurugu za kifikra ndani yetu. Sababu kubwa ya kudhofika kwa akili zetu ni huzuni, mfadhaiko, imani potofu kwa kuhangaikia vitu visivyo halisi kwetu. Muda mwingi mawazo na kuwazia kutafuta dhamani ya maisha kwakutojimbua thamani yako ni ipi hutupotezea ufanisi wetu.

Nb: Tunaishi kumbukumbu zetu za kufiti kwenye mifumo yetu na maisha halisi yanatupita. Akili haihitaji kubanwa kwenye mwelekeo inahitaji ufahamu utaoleta kuelewa kinachotakiwa kitatendeka. Kufikiri kwa makini kunakuja baada ya kuelewa na si kuelekezwa.
 
Hata mimi .
Unahitaji umakini kwanza kuweza kulielewa hili kwa kujiuliza mwenyewe. Kabla hujafikiri lazima umepata swali, swali linatokana na ulivyo ona na kusikia. Je, kuona kwako na kusikia kupo huru kukupa kujiuliza au kumejawa na mawazo ya kibinafsi tu. Kila kitu unaona na kusikia kwa kivuli cha kujipendelea wewetu ufaidike. KUWEZA KUFIKIRI KWA MAKINI KUNAHITAJI AKILI ILIYO HURU KWENYE UBINAFSI WAKE NA KUONA UHALISIA KAMA ULIVYO BILA WEWE KUWEPO KATI.
 
Hata mimi .
Unahitaji umakini kwanza kuweza kulielewa hili kwa kujiuliza mwenyewe. Kabla hujafikiri lazima umepata swali, swali linatokana na ulivyo ona na kusikia. Je, kuona kwako na kusikia kupo huru kukupa kujiuliza au kumejawa na mawazo ya kibinafsi tu. Kila kitu unaona na kusikia kwa kivuli cha kujipendelea wewetu ufaidike. KUWEZA KUFIKIRI KWA MAKINI KUNAHITAJI AKILI ILIYO HURU KWENYE UBINAFSI WAKE NA KUONA UHALISIA KAMA ULIVYO BILA WEWE KUWEPO KATI.
 
Huwezi critical thinker kama umelelewa kuwa submissive.
  • ukihoji mambo nyumbani, unaambiwa huna adabu, unasumbua wakubwa n.k
  • Ukihoji mambo shuleni, unadhihakiwa kujifanya mjuaji.
Jamii nzima inataka tuwaze kama kondoo.
Ni changamoto sana.
 
Huwezi critical thinker kama umelelewa kuwa submissive.
  • ukihoji mambo nyumbani, unaambiwa huna adabu, unasumbua wakubwa n.k
  • Ukihoji mambo shuleni, unadhihakiwa kujifanya mjuaji.
Jamii nzima inataka tuwaze kama kondoo.
Ni changamoto sana.
Ndio maana unatakiwa ubebe msalaba wako mwenyewe. Maisha ni yako na nijukumu lako kufuata ukweli na si usalama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom