Umuhimu wa mapumziko siku ya Sensa

nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
3,609
4,097
Nimefikiri mara mbilimbili kuhusu sensa ya watu na makazi. Nimegundua Ili kupata takwimu sahihi kabisa Kuna umuhimu wa kuruhusu siku hiyo iwe ya mapumziko.

Itasaidia kupata takwimu sahihi lakini pia wahusika wakubwa wa hizo familia watakiwepo nyumbani na hivyo kutoa taarifa sahihi.

Hayo ni maoni yangu.

Pia, soma: Serikali: 23 Agosti ni siku ya mapumziko
 
... hakuna namna Tanzania yote itakuwa off siku hiyo; hakuna. Muhimu ni kuhakikisha taarifa zinazohitajika kwenye sensa zitapatikana.
 
Hapa nnapoishi kuna apartments tunaishi wapangaji tu bila ya mwenye nyumba, ikifika asubuhi wote tunaenda maofisini kiongozi hizo taarifa unamuachia nani ilhali hakuna anayebaki hapo nyumbani mkuu...?
Hili zoezi litachukua zaidi ya Siku moja bwashee, labda wafanye week end na Jumatatu owe mapumziko
 
Hili zoezi litachukua zaidi ya Siku moja bwashee, labda wafanye week end na Jumatatu owe mapumziko

Nafahamu lakini kuna ofisi watu wanaingia kwa muda wa siku zote hizo za hilo zoezi and still boss anakuhitaji mkuu, utawezaje kuacha kwenda kazini...?
 
Nimefikiri mara mbilimbili kuhusu sensa ya watu na makazi. Nimegundua Ili kupata takwimu sahihi kabisa Kuna umuhimu wa kuruhusu siku hiyo iwe ya mapumziko.

Itasaidia kupata takwimu sahihi lakini pia wahusika wakubwa wa hizo familia watakiwepo nyumbani na hivyo kutoa taarifa sahihi.

Hayo ni maoni yangu.
Nyie vitoto vya kidato cha nne mnasumbua sana mkila mkashiba ugali shikamoo,kwani sends ndiyo imeanzishwa sasa?
 
Uzi wako kwa namna fulani una uelekeo wa UVIVU tu,,,ni kama Wanafunzi wanayofurahi siku asipoingia Mwl wa hisabati.

Hii nchi Wafanyabiashara ni wengi sana,,,Private sector ndio inaendesha hii Nchi,,,kuna huduma muhimu sana tunahitaji tuzipate kwenye ofisi za umma...

Muhimu Toa ushirikiano unaotakiwa ikifika hio siku,,,, Na wewe Demi pia hakikisha umeacha mlango wazi alfajiri sana....Usikwamishe Juhudi
 
Uzi wako kwa namna fulani una uelekeo wa UVIVU tu,,,ni kama Wanafunzi siku asipoingia Mwl wa hisabati.

Hii nchi Wafanyabiashara ni wengi sana,,,Private sector ndio inaendesha hii Nchi,,,kuna huduma muhimu sana tunahitaji tuzipate kwenye ofisi za umma...

Vilevile ikiwa mapumziko sio guarantee ya watu kubaki majumbani...

Muhimu Toa ushirikiano unaotakiwa ikifika hio siku,,,, Na wewe Demi pia hakikisha umeacha mlango wazi alfajiri sana....Usikwamishe Juhudi
😅😅😅 sawa kaka, kwakuwa umesema hivyo nitawafungulia mlango
 
Ndugu wana jamvi nmeona Serikali imetoa taarifa kuwa Ile siku inayotangazwa Sana ya Sensa kuwa sio siku ya mapumziko. Kiukweli niseme serikali inakosea Sana na haitapata taarifa sahihi kabisa.

Kuna Baadhi ya nyumba hakuna anaebaki Nyumbani hivyo hata wakienda kesho yake hawatakuta mtu maana wote wanaenda kazini.

Pia wanasema ukiondoka uache taarifa zako Kwa anaebaki. Hilo ni ngumu Kwa vile sio Kila niliepanga nae ninamuamini kiasi cha kueza kumuachia taarifa zangu zote binafsi.

Pia Kwa wale walio na wadada wa kazi haiwezekani kuanza kumuambia mdada wa kazi taarifa zangu na familia Kwa ujumla maana ni kama kuwa wazi sasa kitu ambacho sio wote tupo tayari.

Pia hawajasema ni taarifa zipi ambazo zinatakiwa kuachwa ili wakija waweze jibiwa maana tangazo linasema Tu taarifa ziachwe Nyumbani.

Naishauri serikali hiyo siku waifanye iwe ya mapumziko ili kuondoa hizi dosari lasivyo watapata taarifa potofu kuwa tumefika 67m kumbe tupo pungufu

View attachment 2326622

IMG-20220817-WA0021.jpg
 
Back
Top Bottom