Umuhimu wa kukumbuka siku ya kuzaliwa (birthday)

Blank page

JF-Expert Member
May 28, 2015
4,728
3,173
Happy born day to myself (kijana).
Nafurahi kwamba leo, toka kuwamo duniani ni miaka 22 sasa, namshukuru M/Mungu kunijalia uhai na furaha.
Wakuu napenda tuweze kubadilishana mawazo, juu ya umuhimu wa siku ya kuzaliwa, simaanishi kuiwekea pati ama kuisherekea kwa kula keki. No, nataka kufahamu ni nani mtu muhimu huwa unamkumbuka ikifika tarehe yako ambayo miaka nyuma kadhaa imepita toka uzaliwe? Ama ni mambo gani huwaza ama kuyaanzisha upya ama kuyakumbuka? Kiufupi ni jinsi gani, hii siku unaiadhimisha labda kwa kujiwekea malengo kadhaa ama kuona kuna sehemu mwaka ulopita hukuifanya au kuna kitu unataka kubadilisha katika maisha? Baada ya kufika umri fulani.
Kiukweli mimi huwa naadhimisha kwanza kwa kufurahia familia yangu, kingine kuona kuwa nimeishi miaka mingi duniani lakini mchango wangu ni upi? Nagundua kuwa kuna vitu, natakiwa kuvibadilisha. Karibuni watu wa kutoa mawazo, na kushauri mambo gani makubwa nifanye ama yanapendeza kwa umri wangu, bila kusahau na kutoa uzoefu wenu katika siku ya kuzaliwa.
 
wakati unazaliwa, mama yako alinusurika kufa. So shukrani kwa wazazi, ni very important.
After all, watu wenye tabia ya kukata keki na kulisha washikaji na mashosti, wakasahau kabisa tabu aliyoipata mzazi wakati yuki leba, huwa wana tabia zinazofanana, ..mbaya
 
wakati unazaliwa, mama yako alinusurika kufa. So shukrani kwa wazazi, ni very important.
After all, watu wenye tabia ya kukata keki na kulisha washikaji na mashosti, wakasahau kabisa tabu aliyoipata mzazi wakati yuki leba, huwa wana tabia zinazofanana, ..mbaya
ujumbe,muhimu..sana,mkuu..asante.
kweli,bila..baba,na..mama..tusingekuwa,hapa.
 
Back
Top Bottom