Umuhimu wa kufunga kula | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umuhimu wa kufunga kula

Discussion in 'JF Doctor' started by akohi, Jul 29, 2012.

 1. akohi

  akohi JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 761
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 60
  Zipo faida nyingi za kidimi na pia kisayansi.
  Mi naongelea zaidi ki sayansi japo nakaribisha wadau kuendeleza au kukosoa ntakapoishia.
  1.Inapunguza unene
  2.Inapunguza/kuondoa sumu mwilini
  3.Inaongeza uwezo wa mwili kufanya kazi vizuri
  4....Etc

  Sio lazima ufunge kula kabisa au kunywa, waweza kupunguza baadhi ya milo tu au namna na aina ya misosi, unaweza kufunga kula chips, soda, burger, nyama choma/kaangwa etc. Pendelea matunda na mboga mboga tofauti pia zisi I've sana.
   
 2. F

  Firigisi Member

  #2
  Jul 29, 2012
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  unongea kitaalam au kwa hisia zako tu??
  sumu gani mwilini?
  kuna kitu kinaitwa rebound effect baada ya fasting ,unajua??
  mwili kufanya kazi in what sense,kidney fxn ,liver ? ungesema mazoezi ningekuelewa

  Ushauri:Fanya mazoezi na kula balanced diet ,kufunga kuna madhara makubwa kuliko faida
   
 3. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  huna pesa ya chakula? duh utawala wa JK shilingi imepanda na mfumuko hata viazi havifiki town.
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Faida Za Kufunga Za Kiroho (Nafsi) Na Kimaumbile (Siha Ya Mwili)


  Una wajibu wa kutekeleza majukumu hata kwa nafsi yako mwenyewe. Nafsi zetu sio mali yetu bali ni za Muumba, Bwana wetu; na nafsi hizi si lolote ila zinahitaji uangalizi wa kweli kutokana na sisi wenyewe, na vile vile tuna wajibu wa kuzitunza vyema.

  Maana Ya Funga (Kiroho/Nafsi)


  Mazowea yanaonyesha kwamba Kipofu kwa ujumla ana nguvu ya kukumbuka, na baadhi ya hisia zake huwa zaidi kuliko za mtu wa kawaida ambaye anaona. Kwa maneno mengine (tunaweza kusema), ikiwa kitengo cha fani fulani hakikutumika, basi

  kitengo cha fani nyengine huwa na nguvu zaidi. Ni sawa sawa na uhusiano wa kiwiliwili na nafsi (roho). Kudhaifisha kiwiliwili kunapelekea kuipa nguvu nafsi, mfano wake ni sawa na kukatakata matawi ya mti ili yapatikane maua mengi na matunda kumea (kuota) zaidi.

  Wakati mtu anapofunga, hukingika na vitendo viovu, na huwa na uwezo zaidi wa kujizuia nafsi yake kuelekea kwenye matamanio ya matendo maovu. Zaidi, funga inamfanya mtu amfikirie Muumba wake zaidi, humkuzia mapenzi ya kutoa misaada na humfanya ahisi uzuri wa kumtii Bwana wetu.

  Maana Ya Funga (Kimaumbile)


  Wanafunzi husoma kwa miezi kadhaa mfululizo, baadae hupewa mapumziko. Waajiriwa hufanya kazisiku sita kwa wiki, siku ya saba hupata wasaa wa kupumzika. Binaadamu hutumia nguvu ya akili na mwili siku yote, baada ya hapo usingizi

  unajitengeneza katika kitengo chake ili apumzike kwa ajili ya uwezo wa siku nyingine.
  Hata mashine na zana mbali mbali zinahitaji mapumziko, na tunayaona haya kwenye magari, ndege, matreni na kadhalika.

  Kwa hivyo, sio sawa kufikiri kwamba tumbo na njia ya kusaga chakula haihitajii kupumzika.
  Kwa kweli matibabu ya kileo yamefikia kwenye hitimisho hili hili. Idadi kubwa ya Matabibu wa Switzerland, Ujerumani, na

  kwengineko, wameagiza watu kufunga kwa kupambana na maradhi tofauti yaliyo sugu, kufunga kwa muda mrefu au mfupi kutegemeana na hali ya ugonjwa wenyewe na uwezo wa kimwili wa mgonjwa.

  Vile vile wamegundua kwamba sehemu ya mwili kama kifuko mfanyizwamo maji yenye dawa yaingiayo damuni na kufanya kazi nyengine mwilini (glands), hufanya kiasi fulani cha tindikali (acids) katika tumbo ili kusababisha njaa na kiu. Tindikali hizi

  huua vijidudu (germs) vingi mwilini ambavyo husababisha maradhi mengi. Takwimu vile vile zimeonyesha kwamba usagaji wa chakula mwilini na magonjwa mbali mbali hupungua miongoni mwa watu wenye tabia ya kufunga.

  Tunajua kwamba binaadamu anahitaji mabadiliko ya miongo, hewa na maji kila baada ya wakati fulani. Wagonjwa wanaopata nafuu kutoka kwenye ugonjwa, hupelekwa sehemu nyingine baada ya kupona ambayo sio ile waliyoizoea kuishi kabla.

  Miongoni mwa bahati kubwa waliyonayo watu wa nchi za Magharibi, ni kuutumia wakati wa msimu wa joto katika nchi za nje ya nchi zao. Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuwa, ni muhimu kubadilisha tabia za kawaida wakati hadi wakati. Hii vile vile ni aina ya mapumziko.

  Tunaona kwa mfano, wakulima hutumia maeneo yao ya kilimo kwa aina tofauti ya kilimo ili kuupa udongo mapumziko. Mfululizo huleta madhara, inakatazwa kufunga mwaka mzima mfululizo, hata ikiwa kwa wale wote wanaofunga kwa kutaraji faida ya kiroho.

  Mazoea vilevile yanatuonyesha kwamba ikiwa mtu atafunga milele, itakuwa ni tabia na umbile la pili, na hatofaidika kwayo kama yule ambaye anafunga kwa kipindi maalumu. Kwa kweli, ikiwa mtu atafunga kwa zaidi ya mwezi mmoja, funga yake haileti athari (madhumuni) sana.

  Kwa kumalizia maelezo haya, kwa wale wanaofunga kwa ajili ya maelekezo ya matibabu au hata kwa kulazimishwa kwa ajili ya nidhamu, hupata faida ya kimwili itokanayo na funga, lakini hawafaidiki wala hawaathiriki kiroho. Waumini hufunga kwa mazingatio ya kutii amri ya Muumba (Allaah). Kwa hivyo wanapata malipo yake ya Kumcha Mwenyezi Mungu, na hawapotezi faida ya funga kimwili wala kimaumbile.

  Funga Kwa Kulitunza Umbile La Mwili Vyema

  Kujiweka Vyema:

  Tukiiweka mbali thamani ya funga inayopatikana kiroho, kuna Manufaa ya kiwiliwili yanayopatikana kwa kutokula kwa muda mfupi. Manufaa haya huvunwa sio tu na mtu aliyenenepa sana bali na kila aliyefunga.

  Kujiweka vyema kwa ujumla kwa mtu anayefunga kunabainika na madaktari. Madaktari wengi hutoa ushauri wa kufunga kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi ya maumivu ya kuvimba viungo (Gout), magonjwa ya moyo, ugonjwa ya ngozi,
  ukosefu wa kujizuia kwa chakula na kinywaji, au uvutaji sana wa sigara.

  Faida ya Ubongo:


  Funga ni nzuri kwa nidhamu ya ubongo, kwani huchangamsha taathira ya kiroho. Ubongo unafaidikasana. Ikiwa unasomea masomo magumu, unatayarisha hotuba, au umejiingiza kwenye mazingatio ya mawazo mazito; utayatekeleza vizuri mambo

  hayo ikiwa utafunga. Funga inaipa werevu akili yako, inakufanya utanabahi haraka na kuwa na nguvu za hisia ya akili. Unazingatia zaidi ikiwa tumbo lako ni tupu na halipokei damu kutoka kwenye ubongo kwa ajili ya kusaga chakula.

  Wazungumzaji wa hadhara wengi wanatambua vyema kwamba kula kabla ya kuzungumza kunapunguza werevu wa akili na kushusha nguvu ya kuhutubia. Huwa wanafunga kabla ya hotuba muhimu na hula baadaye. Wanaelewa ubongo unafaidika kwa funga.

  Kupumzisha Usumbufu wa Kusaga Chakula:


  Sehemu nyingine za mwili ambazo hupumzika kwa kufunga ni tumbo, ini, pancreas, na chango. Hivi mara nyingi huwa vinafanya kazi kupita kiasi. Endapo mfumo mzima wa kusaga chakula utapewa mapumziko, kula huwa ni jambo la kupendeza sana.

  Kurudisha Ujana na Kunawirisha Ngozi:


  Funga imetajwa na wautunzao sana ujana na wale wanaopenda kuzidisha/ongeza maisha. Wazo hili linamea kutokana na ukweli kwamba, watu wanaofunga wanajipatia ngozi safi, rangi ya waridi kwenye mashavu yao, na huonekana vijana zaidi kuliko walivyokuwa mwanzoni.

  Watu wenye matatizo ya magonjwa ya ngozi kama ugonjwa wa mbalanga (psoriasis), ugonjwa unaosababisha vipele vyekundu usoni na shingoni (acne), au ugonjwa wa kuambukiza unaorejea kila mara ambao madaktari hushauri kutotumia sukari na mafuta kwenye vyakula vyao. Ni uzuri gani kutokula kwa wakati wa muda maalum, na kuzipa nafasi tundu za ngozi kujisafisha wenyewe na vile vile kuwa huru na madhara ya ongezeko la sukari na mafuta.

  Baraka kwa Wavutao Sigara:


  Kwa yeyote anayejaribu kuacha kuvuta au kunywa, funga inaweza kuwa ni baraka kwa mwili wake. Kwa kuacha tumbaku, ulevi na chakula kinacholiwa kwa wakati, mtu huusadia mwili kurudi katika hali yake ya kawaida.

  Mara mwili "unaposuguliwa ukawa safi" ndani, mvutaji na mnywaji hujihisi yu hai na huwa na tahadhari na kutokwa na hamu ya kurejea tena kwenye tabia yake mbaya.

  Hamu zaidi au karibia sawa ya kula huja kutokana na funga, na chakula cha kawaida tu humfanya mtu akione kina ladha zaidi. Utumiaji mkubwa wa pilipili (pepper), viungo (spices), haradali (mustard), na nyanya zilosagwa na viungo (ketchup), vyote hivi havihitajiki tena kukifanya chakula kilete hamu ya kula ikiwa mtu atafunga.

  Mapumziko ya Moyo:


  Ikiwa wewe ni miongoni mwa wagonjwa wa moyo, utabaini kwamba funga inashusha mzigo wa moyo na mzunguko wa damu. Ikiwa una upungufu wa kupumua, funga inakuza hali yako ya kupumua na kwa kuondosha chumvi na maji mwilini, hupunguza tissue edema. Hali hii inafanya uwezekano wa kulala kuwa mwepesi na bila ya kutumia mito mingi.

  Madhara:


  Kuna matatizo madogo madogo yanaweza kutokea wakati wa kufunga. Mtu anayefunga huenda akaumwa na kichwa; ikiwa ni hivyo, basi anahitaji kufunga. Matatizo mengine ya funga ni, kuhisi kunyong'onyea, moyo kupiga piga, kusinzia mchana, kawaida ni matatizo madogo tu, na yanatoweka kwa kupumzika kidogo.

  Ikiwa mtu anataka kukuza mpangilio wake wa kula kwa kuacha kula nyama, mchuzi wenye viungo vikali, keki tamu sana, na sukari inayohifadhika mwilini, basi na afunge, atakuwa kakimbilia kwenye njia ya mabadiliko. Baada ya mtu kula sana vyakula

  hivi na kwa muda kiasi, huwa hawezi tena kuipata afya wala ladha ya chakula halisi (ambacho hakikuongezewa vitu vya kuchangamsha kinywa). Kinywa chake kinakuwa kishageuka vibaya kiasi ya kwamba hawezi tena kuburudika na ladha ya matunda mazuri, mkate wa ngano nzima, na mboga mboga.

  Funga hii hii pia inatuhakikishia faida zaidi kuliko dawa, kwa tumbo linalolishwa kwa vibaya linagundua mapumziko ambayo kwa muda mrefu yalikuwa yanahitajika. Njaa ya kweli inaweza kukidhiwa na chakula halisi.

  Kwa kujiongezea imani ya kiroho jaribu funga. Utabaini kwamba inakupeleka karibu na Muumba katika Du'aa. Inakufanya uwe na tabia madhubuti ya nidhamu yako mwenyewe na mazoea ya unyenyekevu wa kukikataa chakula chako mwenyewe.

  Faida maradufu ni zile za kujihisi uko katika siha nzuri, macho maangavu, ubongo wenye kutanabahi, kuruka haraka kwenye hatua nyingine na mafanikio makubwa katika kazi yako. Kila mara husemwa: "Mtu mwenye bidii kwa ajili ya mafanikio huwa na tegemeo". Njaa kidogo tu inaweza kukupa ile bidii kwa haraka.

  Jaribu funga kwa kujiweka vyema kiroho na kimaumbile!
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu, hebu nitiririkie faida za daku tafadhali.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Mkuu King'asti Mtume wa Mwenyeezi Mungu Mtume Muhammad Rehema za Allah ziwe juu yake na amani Amesema hivi katika hadithi yake:  ((تسحروا فإن في السحور بركة )) رواه البخاري ومسلم((Kuleni daku kwani katika huko kula daku, kuna baraka)) [Al-Bukhaariy na Muslim].
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  nikifunga nakabiliwa na hamu kali sana ya kushiriki zinaa, na pia muda wote napatwa na jinamizi la ngono, je funga yangu ina thwawabu?
   
 8. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mwanangu hizo ni hadithi za miaka 2000 iliyopita. Unene ni suala la mtu binafsi na anavyokula. Sumu gani hizo zaidi ya kuwa za kufikirika. Hiiyo etc ni gonjwa gani mwanangu?
   
 9. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nawe unafunga pia?
   
 10. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Atleast zinasaidia kuweka some organs in resting, habari ya unene si lazima kufunga kunapunguza unene kuna watu ni opposite.
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Hahaha! Mbona kuntilia shaka? Lol, wanionaje ustaadhat mie!
   
 12. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nilikuwa nataka nikukaribishe kwenye mahanjumati
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Mie nampenda sana mtume.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Nikaribishe tu. Tunaanzia futari hadi daku, narudi home alfajiri kumalizia sala. Sasa nije leo?
   
 15. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada, vipi kuhusu wale wanaobadili timetable ya kula. Badala ya kula mchana wanakula usiku mpaka kuvimbiwa. Kuna madhara gani wanayapata. Maana wanakula utadhani wapo shifti ya usiku. Full night kutafuna.
   
 16. Hayajamani

  Hayajamani JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 883
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwa maoni yangu kufunga kunaweza kuwa na faida kiroho na kimwili kama yafuatayo yatazingatiwa;

  Kiroho: inategemea una concept gani kichwani! Ni mambo ya kiimani, ikimaanisha mambo ambayo hayapo na labda hayajawahi kuwepo ila kuna tarajio la kuwepo baadae. Kila mtu ana imani yake na anaamini hayo mambo ambayo hayajawahi kuwepo wala kuja kwake mimi siwezi kuelezea.

  Kimwili: Kama tutaepuka kula kwa wingi wanga (starch), colesterol sana, carbohydrate na vingine. Pia kufanya mazoezi kwa ukawaida na kuepuka maisha ya kivivu. Hasa wakati wa usiku sio vizuri kula vyakula hivyo vya wanga na sukari kwa wingi sababu, miili yetu inapumzika hivyo havi burn-out. Kubadilisha ratiba kwa kuacha kula mchana wakati mwili ndio upo active zaidi na kula vyakula vingi usiku hasa nafaka kama nafaka, viazi, ndizi, tende na sukari nyingi. Tena kula zaidi (quantitative and qualitative) hakutakuwa na suluhisho la kiafya. Usiku tutakula zaidi then tutalala, au kukaa na kusikiliza mahubiri, kupiga soga hivyo miili yetu itabadilisha utaratibu na tutanenepa zaidi na kuwa vulnerable kwa magonjwa kama kisukari, BP na kiarusi.

  Hivyo tufuate kanuni za kiafya tuache ushabiki wa kiitikadi na kujaribu kujidanganya kwa kutafuta kanuni za kitaalamu ambazo hazipo kusapoti imani zetu. Hivyo basi kufunga ni kwa ajili ya afya ni kujisulubu kidogo kwa kula kidogo mchana na usiku kuacha kula nafaka, sukari, bia ila labda maji matunda kiasi na mboga za majani. Tusiyajaze matumbo yetu usiku vyakula vilivyojaa spices, starch, sugar n.k.
   
 17. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nakusubiri basi na uji wa mchele wa kufungulia vinginevyo surprise
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Huna funga unakaa na njaa tu bora ule kuliko kuwa wewe unafunga kisha unakuwa na hamu ya kushiriki zinaa Mkuu Kiranja Mkuu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Kama unampenda mtume muhammad Rehema za Allah ziwe juu yake na Amani, mfuate maamrisho yake King'asti
   
 20. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  haya wakuu shule nimeisoma ila inhitaji utafiti zaidi wala si huu
   
Loading...